Jitiishe Mwenyewe ili Kufundisha Wengine Nidhamu
Nilikuwa na ubia wa kazi wa karibu na dada mmoja mzee katika masuala ya jumla. Baada ya kufanya kazi naye kwa muda fulani, nikamwona kuwa mzembe katika kazi yake na kwamba hakukubali ukweli. Kikwelikweli, nilikata kauli kumhusu. Hatua kwa hatua, uhusiano wa kawaida kati yetu ulipotea, hatukuweza kupatana vizuri, na hatukuweza kuwa mbia katika kazi. Nilihisi kuwa lilikuwa ni kosa lake hasa kwamba uhusiano wetu ulifikia kiwango hiki, na hivyo nilijaribu kufikiria njia za aina zote za kuzungumza naye ili apate kujijua. Lakini majaribu yangu yote ya kuzungumza naye yalikuwa bure au hata kuwa na athari za mkabala. Hatimaye tukaachana, kama masuala yetu hayajatatuliwa. Hili lilinifanya kuamini hata zaidi kuwa hakuwa mtu ambaye hukubali ukweli. Baada ya hapo, kanisa lilinipangia kukaa na familia mwenyeji tofauti. Baada ya muda mfupi, niligundua matatizo mengi pia yalikuwa na ndugu wa kiume na wa kike wa familia mwenyeji, na mimi tena “nikajitahidi” kuwasiliana nao, lakini jitihada zangu zote hazikufaa, na wakaanza kuwa na chuki dhidi yangu. Nikiwa nimekabiliwa na hali hizi, nilikuwa na wasiwasi sana na kukanganyika: Mbona watu ninaokutana nao hawakubali ukweli? Mpaka siku moja, nikapata chanzo cha tatizo wakati nilipotatizika kazini.
Siku moja, kiongozi huyo akanipangia nimtumie mpango wa kazi, na nikamuaminisha huyo dada mzee kumpelekea. Nani angejua kwamba wiki moja baadaye, hicho kifurushi kingerejeshwa kwangu kama hakijafunguliwa. Nikiwa nimekabiliwa na hali hii, nilishtuka na kumlaumu yule dada mzee kwa sababu ya kushughulikia vibaya jambo hilo, jambo lililosababisha kifurushi kutopelekwa kwa kiongozi. Hakukuwa pia na mawasiliano yoyote kutoka kwa kiongozi kwa siku chache baada ya hili, na nilikuwa ninaanza kuwa na wasiwasi: Kwa kawaida ikiwa kitu kinakosa kutumwa au kinatumwa kama kimechelewa, kiongozi atapiga simu kuuliza kuhusu hali hiyo. Kwa nini hajawasiliana nami wakati huu? Anajaribu kunizuia kutekeleza wajibu wangu? Nikaanza kuwa na hofu zaidi na zaidi—mawazo yangu yalijaa wasiwasi na majuto. Sikuweza kujizuia kuanguka mbele ya Mungu, “Mungu, najihisi mgonjwa sana na kuwa na mgongano moyoni mwangu. Mpango wa kazi umerudishwa kwangu kama haujafunguliwa. Sijui kinachoendelea, na sijui ni kipengele gani changu kitakachokamilishwa katika kukumbwa na hali hii. Tafadhali niongoze na kunipa nuru na kunisaidia kuelewa mapenzi Yako.” Mara baada ya sala, mojawapo ya virai vya Mungu kiliendelea kunijia kichwani mwangu, “Wakati wowote unapofanya kitu chochote, hicho huenda mrama, au kugonga ukuta. Hii ni nidhamu ya Mungu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji). Niligundua kwa ghafla kuwa masuala niliyokuwa nimeyakabili wakati wa kazi, kuwa mbia kubaya na dada mzee, na maoni ya ndugu wa kiume na wa kike wa familia mwenyeji; si hizi zilikuwa ni njia za Mungu za kunishughulikia kupitia hali zangu? Nilimwita Mungu kwa ukimya, “Lazima kwanza utatue matatizo yote ndani yako kwa kumtegemea Mungu. Komesha tabia zako potovu na kuwa na uwezo wa kuelewa kweli hali zako mwenyewe na kujua jinsi unapaswa kufanya mambo; endelea kushiriki chochote ambacho hukielewi. Haikubaliki kwa mtu kutojijua. Uponye ugonjwa wako mwenyewe kwanza, na kwa njia ya kula na kunywa maneno Yangu zaidi, kutafakari maneno Yangu, ishi maisha na fanya mambo kwa mujibu wa maneno Yangu; haijalishi ukiwa nyumbani au mahali pengine, unapaswa kumruhusu Mungu atwae nguvu ndani mwako” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 22). “Wakati jambo linakukumba, ni lazima kuwa mtulivu, na mtazamo unaofaa, na ni lazima kufanya chaguo. Unapaswa kujifunza kuutumia ukweli kutatua jambo lile.Katika wati wa kawaida, kuna maana gani ya wewe kuelewa ukweli fulani? Haiko hapo tu ili kujaza tumbo lako, na sio tu hapo kukupa kitu cha kusema, wala hauko hapo kwa ajili ya kutatua shida za wengine. Lililo muhimu zaidi, matumizi yake ni kutatua matatizo yako mwenyewe, shida zako mwenyewe—ni baada tu ya kutatua shida zako binafsi ndipo utaweza kutatua shida za wengine” (“Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalikuwa kama mwako wa umeme. Ndiyo, wakati mambo yanapotokea tunapaswa kwanza kujijua, na kutumia ukweli kutatua matatizo ndani yetu. Kwa kuboresha hali yetu, sisi hutatua matatizo yetu, na hivyo kufanya iwezekane kutatua matatizo ya watu wengine. Lakini sikujijua wakati mambo yalipotokea, na niliwakazia macho wengine, nikiwalalamikia wakati wowote ilipowezekana. Wakati uratibu haukuwa sawa, nilimuona mtu mwingine kuwa sababu, na nilijaribu kutafuta njia za kuwasiliana naye, kumfanya ajifunze mafundisho yao na kujijua. Wakati ndugu wa kiume na wa kike wa familia mwenyeji hawakuwa tayari kunisikiliza nikiwasiliana, niliamini ni kwa sababu hawakuwa wakifuatilia ukweli, na hawakuweza kuukubali ukweli. Wakati utaratibu wa kazi ulirejeshwa kwangu bila kufunguliwa, nilibadilisha lawama na wajibu kwa wengine. Haya yote yalipotokea, nilishindwa kuchunguza ni upotovu upi nilioufichua, na ni ukweli upi nilipaswa kuuingia. Ilikuwa ni kama sikuwa na upotovu, na nilifanya kila kitu sawa. Badala yake, nilitoa madai kwa wengine kulingana na viwango vyangu, na kama mtu hakuweza kufikia kiwango changu au alikataa kuyakubali mawasiliano yangu, basi nilifikia uamuzi kwamba huyo mtu ni lazima hakuwa akitafutilia ukweli na kuukubali ukweli. Kwa kweli nilikuwa mwenye kiburi mno na sikuwa na maarifa yangu mwenyewe. Sikuwa na maarifa kuhusu upotovu nilioufichua, wala sikutafuta ukweli ili kutatua matatizo yangu mwenyewe, lakini daima niliwapata wengine na kosa. Ningewezaje kuwa mbia kwa upatanifu na kuelewana na wengine? Ni hapo nilipogundua: Sababu yangu kutoelewana na yeyote si kwa sababu hawatafuti ukweli, au kukubali ukweli, lakini kwa sababu mimi sina maarifa yangu mwenyewe, na huwa sisisitizi matumizi ya ukweli kutatua matatizo yangu mwenyewe.
Baada ya kutambua yote haya, nilianza kuzingatia kuingia kwangu mwenyewe na kutatua matatizo yangu mwenyewe kwanza wakati mambo yalipotokea. Wakati wa kuwasiliana na ndugu wa kiume na wa kike hatimaye, kulikuwa na vijenzi vya maarifa yangu mwenyewe katika mawasiliano yangu. Huu ndio wakati nilipopata ndugu zangu wa kiume na wa kike kuwa wamebadilika. Walianza kuonyesha maarifa kiasi ya upotovu wao wenyewe, na hatua kwa hatua tulikuza ubia kwa upatanifu. Kama nimekabiliwa na ukweli huu, hatimaye niliweza kuona kwamba wakati masuala yanapotokea, ni muhimu mno kujijua na kutatua matatizo ya mtu mwenyewe kwanza. Ni hapo tu tunapoweza kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wetu wa kawaida, kuwa na ubia kwa upatanifu na wengine, na kufaidi kutokana na uzoefu wetu wa maisha.
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?