Kiini cha Kutumia Mamlaka Vibaya Kwa Ajili ya Ulipizaji Kisasi wa Mtu Binafsi

14/01/2018

Zhou Li Mji wa Xintai, Mkoa wa Shandong

Wakati fulani kitambo, tulihitaji kuzichora wilaya katika eneo letu, na kwa msingi wa kanuni zetu kwa ajili ya uteuzi wa viongozi, kulikuwa na ndugu mmoja wa kiume aliyekuwa mtaradhia mzuri kiasi. Nilitayarisha kumchagua kuwa kiongozi wa wilaya. Siku moja nilipokuwa nikizungumza na ndugu huyu, alitaja kwamba alihisi kuwa nilikuwa mwenye nguvu sana katika kazi yangu, mkali sana, na kwamba katika mkusanyiko pamoja nami hapakuwa na furaha nyingi…. Niliposikia jambo hili, nilihisi kuwa nilikuwa nimedunishwa. Nilihisi vibaya sana; mara moja nikakuza maoni fulani ya ndugu huyu, na sikukusudia tena kumchagua kuwa kiongozi wa wilaya.

Niliporejea kwa familia wenyeji wangu, nilikuwa bado ninakerwa na singetulia. Wakati huo, niliwaza juu ya kifungu kutoka mahubiri: “Jinsi wale wanaohudumu kama viongozi wanavyowatendea ndugu wa kiume na wa kike ambao huwaona kuwa wenye kusumbua, ambao wanawapinga, na ambao wana maoni tofauti kabisa kuwaliko—hili ni suala la maana sana na linapaswa kushughulikiwa kwa tahadhari. Wasipoingia katika ukweli, kwa hakika watabagua na kuwakaripia watu kama hawa wanapokumbwa na aina hii ya suala. Aina hii ya hatua hasa ni dhihirisho la asili ya joka kubwa jekundu linalompinga na kumsaliti Mungu. Ikiwa wale wanaohudumu kama viongozi wanafuatilia ukweli, na kuwa na dhamiri na mantiki, watatafuta ukweli na kushughulikia suala hili kwa usahihi. … Kama watu, tunahitaji kuwa wa haki na wa kutopendelea. Kama viongozi, tunapaswa kushughulikia mambo kulingana na maneno ya Mungu ili kuwa mashahidi. Tukifanya mambo kulingana na mapenzi yetu wenyewe, tukiipa uhuru tabia yetu potovu, basi huo utakuwa ushinde wa kuogofya” (Ushirika Kutoka kwa wa Juu). Sikuweza kujizuia kulinganisha mitazamo yangu miwili tofauti kabisa tangu kabla na baada ya mazungumzo yangu na ndugu huyo. Mwanzoni nilikuwa tayari kumchagua kuwa kiongozi wa wilaya, lakini alisema mambo fulani yaliyonisababisha kupoteza heshima nilipozungumza naye, hivyo nilibadili maoni yangu juu yake mara moja na sikupanga tena kumchagua. Je, si huku kulikuwa kutumia nguvu yangu kulipiza kisasi cha ubinafsi? Je, kuna tofauti gani kati ya hili na joka kuu jekundu kubagua na kuchapa dhidi ya wale wanaopinga? Je, si aina hii ya kitendo ni ya kudharauliwa? Kanisa si sawa na jamii. Kanisa linahitaji kila ngazi ya viongozi wake kuwa watu wenye ubinadamu, wanaoupenda ukweli, na wanaoweza kuukubali ukweli. Halihitaji watu wanaojikomba, ambao hawana uhalisi wa ukweli. Lakini kile nilichokuwa nikikifanya kilikuwa kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu. Wakati wa kuchagua mtaradhia nilifikiria tu juu ya maslahi yangu mwenyewe na mradi tu yule mtu mwingine hakuniunga mkono, aliposema kitu ambacho hakikunipendeza, nilifanya ubaguzi dhidi yake na kumchukia. Je, si kutenda kwangu jinsi hii kulifichua kabisa asili ya joka kubwa jekundu likimpinga na kumsaliti Mungu? Je, si hili hasa lilikuwa kufichua tabia ya Shetani, “Wale wanaotii watasitawi; wale wanaopinga wataangamia”? Si kutenda jinsi hii kulikuwa kuwa mtumishi wa Shetani, kuivuruga kazi ya Mungu na kuwa adui Yake? Je, si moyo wangu ni mwovu sana? Kanisa lilikuwa karibu kumchagua mtu kwa nafasi fulani, na ndugu huyo alikuwa mtaradhia mzuri kwa nafasi ya kiongozi wa wilaya. Tathmini yake kwangu ilikuwa haikubaliki kwangu; Ningepaswa kutafuta ukweli juu ya jambo hili na kuyakubali maoni yake. Ningepaswa kujichunguza mwenyewe na kujijua mwenyewe, na kufidia upungufu katika kazi yangu. Hata hivyo, sio tu kwamba sikuangalia sababu ndani yangu, lakini niliipa uhuru asili ya Shetani ndani yangu kubagua na kulipiza kisasi kwake. Mimi ni mwenye kiburi sana, nikipungukiwa sana katika ubinadamu! Tabia hii yangu ni ya kuchukiza sana kwa Mungu! Kama ningeendelea kukupa uhuru asili ya aina hii ya upotovu, hatimaye ningekuwa nimekwisha kuharibika kama mtumishi mwenye kiburi wa uovu ambaye ni kipofu kwa Mungu. Kwa hakika nilikuwa katika hatari kubwa. Wakati huo singeweza kujizuia kutetemekea mawazo na matendo yangu, kujiona nimejaa sumu ya joka kubwa jekundu, kwamba yaliyofichuliwa yote yalikuwa ni uadui dhidi ya Mungu. Mungu kwa hakika huchukia hili, na huchukizwa nalo.

Ee Mungu, asante kwa nuru Yako ya haraka, kwa kuzuia tabia yangu ya ubaguzi, kwa kuniruhusu kuona vyema zaidi uso wangu wa Shetani ukitenda kama adui Yako. Kuanzia siku hii kwendelea, ninapenda kufuata mabadiliko katika tabia, na wakati ninapokutana na watu au vitu ambavyo havinipendezi, nitajifunza kujiweka kando, kuunyima mwili, na katika vitu vyote kuyalinda maslahi ya kanisa, kufanya kila linalowezekana ili kutimiza majukumu yangu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Ninapata njia ya kumjua Mungu

Xiaocao Mji wa Changzhi, Mkoa wa Shanxi Siku moja, niliona kifungu hiki kifuatacho cha neno la Mungu kwa maandishi “Namna Petro...

Mabadiliko ya Mwigizaji

Mwenyezi Mungu anasema, “Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp