Kutambua Kuwa Niliitembea Njia ya Mafarisayo

14/01/2018

Wuxin Mji wa Taiyuan, Mkoa wa Shanxi

Kitu ambacho tumezungumzia mara kwa mara katika ushirikiano wa awali ni njia ambazo zilitembewa na Petro na Paulo. Inasemekana kwamba Petro alizingatia kujijua mwenyewe na kumjua Mungu, na alikuwa mtu ambaye Mungu alimpenda, ilhali Paulo alizingatia tu kazi yake, sifa na hadhi yake, na alikuwa mtu ambaye Mungu alimdharau. Daima nimekuwa na hofu ya kuitembea njia ya Paulo, ambayo ndiyo sababu mimi kwa kawaida mara nyingi husoma maneno ya Mungu kuhusu uzoefu wa Petro ili kuona jinsi alivyopata kumjua Mungu. Baada ya kuishi hivi kwa muda, nilihisi kwamba nilikwishakuwa mtiifu zaidi kuliko hapo awali, hamu yangu ya sifa na hadhi ilikuwa imedidimia, na kwamba nilikuwa nimepata kujijua kidogo. Wakati huu, niliamini kwamba ingawa sikuwa kabisa kwa njia ya Petro, inaweza kusemwa kuwa nilikuwa nimegusa ukingo wake, na angalau ilimaanisha sikuwa naelekea kwa njia ya Paulo. Hata hivyo, ningeaibishwa na ufichuzi wa neno la Mungu.

Asubuhi moja, nilipokuwa nikifanya sala za kiroho, niliona maneno yafuatayo ya Mungu: “Kazi ya Petro ilikuwa utekelezaji wa wajibu wa kiumbe wa Mungu. Yeye hakufanya kazi katika nafasi ya mtume, lakini alifanya kazi huku akifuatilia upendo kwa Mungu. Mwendo wa kazi ya Paulo pia ulikuwa na harakati yake binafsi.… Hakukuwa na matukio ya kibinafsi katika kazi yake—yote yalikuwa kwa ajili yake mwenyewe, na hayakufanyika huku kukiwa na harakati ya mabadiliko. Kila kitu katika kazi yake kilikuwa shughuli, na hakukuwa na wajibu wowote au kujisalimisha kwa kiumbe cha Mungu. Wakati wa safari ya kazi yake, hakuna mabadiliko yaliyotokea katika tabia ya zamani ya Paulo. Kazi yake ilikuwa tu ya kufanya huduma kwa ajili ya wengine, na haikuwa na uwezo wa kuleta mabadiliko katika tabia yake. … Petro alikuwa tofauti: alikuwa mtu ambaye alikuwa amepitia upogoaji na ushughulikiaji na alikuwa amepitia usafishaji. Lengo na motisha za kazi ya Petro zilikuwa tofauti kimsingi na zile za Paulo. Ingawa Petro hakufanya sehemu kubwa ya kazi, tabia yake ilipitia mabadiliko mengi, na alichotafuta ni ukweli, na mabadiliko ya kweli. Kazi yake haikufanyika tu kwa ajili ya kazi yenyewe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea). Maneno ya Mungu yaligusa roho yangu na nikawa kimya: Petro alikuwa mtu ambaye alitimiza wajibu wake kama kiumbe aliyeumbwa. Alifanya kazi kupitia mchakato wake wa kutafuta kumpenda Mungu ukilinganisha na wajibu wake kama mtume. Lakini nilikuwa mtu anayetimiza wajibu wake kama kiumbe aliyeumbwa au kufanya tu kazi yangu kutoka katika nafasi ya hadhi? Wakati huu, nilifikiria nyuma kwa hali mbalimbali za zamani: Kanisa lilipokuwa na kazi nyingi za kushughulikia, ndugu wengine wangesema: Nyinyi kweli mmetwishwa mzigo wa kazi ya Mungu. Halafu ningeropoka: Sisi viongozi hatuna chaguo ila kushughulika nalo. Wakati mwingine, kwa familia wenyeji au mbele ya wafanyakazi wenzangu, ningependa kuufikiria mwili wangu wa maumbile na kujipumzisha mwenyewe, lakini tena ningefikiri: Hapana, mimi ni kiongozi, ni lazima niishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida na sio kuwa mpotovu. Wakati sikutaka kula na kunywa maneno ya Mungu, pia ningefikiri: Kama kiongozi, nisipokula na kunywa maneno ya Mungu, basi ni jinsi gani ningeweza kutatua matatizo ya watu wengine? Wakati mwingine ningeenda na mfanyakazi mwenza kwa familia mwenyeji aliyokuwa akikaa nayo, na nilipoona kwamba jinsi dada mwenyeji alinitendea haikuwa kwa shauku kama alivyomtendea mfanyakazi mwenza, ningekasirika: Huenda usijue mimi ni nani, lakini mimi ni kiongozi wake. Wakati mwingine, kwa sababu yoyote ile, singejihisi kuwasiliana na mwenyeji wa ndugu wa kike na wa kiume, lakini hata hivyo ningefikiri: Kama kiongozi, ningeonekanaje na watu nikija bila kuwasiliana nao? Kwa kuwa mimi ni kiongozi ni lazima niwasiliane na familia wenyeji. ... Hizi tabia mbalimbali zilinionyesha: nilikuwa nikifanya kazi kwa sababu ya hadhi. Kama ilikuwa ni kuwasiliana na watu, kuhudhuria mikutano, au kushughulikia mambo ya kawaida, yote ilikuwa ni kwa sababu tu nilikuwa kiongozi ndipo nilihisi kuwajibika kutimiza wajibu wangu kidogo na kufanya kazi kidogo. Sikuwa natimiza wajibu wangu kama kiumbe aliyeumbwa, na zaidi sikuwa nafanya kazi kupitia mchakato wangu wa kumpenda Mungu kama Petro alivyofanya. Kama mambo yangeendelea kama hapo awali, wakati siku inapokuja ambapo ninafukuzwa na kubadilishwa, labda singeweza kuendelea kutimiza kazi yangu kwa jinsi ninavyofanya sasa. Ni hapo tu ndipo nilipoona kwamba sikuwa mtu ambaye alitenda ukweli au aliyekuwa akiyafikiria mapenzi ya Mungu. Badala yake, nilikuwa mwovu aliyestahili dharau aliyefanya kazi tu kwa ajili ya sifa na hadhi. Ni vigumu kuwa na uaminifu kwa Mungu kufanya kazi jinsi nilivyofanya na ilikuwa ni uzembe tu. Hii ni kwa sababu sikuwa nataka kutenda ukweli na kuyafikiria mapenzi ya Mungu. Kama vile tu asemavyo Mungu, “Hakukuwa na matukio ya kibinafsi katika kazi yake—yote yalikuwa kwa ajili yake mwenyewe, na hayakufanyika huku kukiwa na harakati ya mabadiliko.” Huduma kama hiyo ingewezaje kuyaridhisha mapenzi ya Mungu? Paulo alikuwa akifanya kazi katika nafasi yake kama mtume; kazi yake ilijaa shughuli. Nilikuwa nikifanya kazi na kutumia yote katika cheo changu kama kiongozi. Ni jinsi gani nia hizo na madhumuni ya kuamini katika Mungu tofauti na zile za Paulo?

Wakati huu, nilianguka mbele ya Mungu: Ee Mungu! Asante kwa wokovu wa wakati ufaao, ambao ulinifanya niamke kutoka kwa mzubao wangu, kutambua hali yangu ya kweli, na kuona kwamba bado nilikuwa nikiitembea njia ya Paulo Mfarisayo. Kazi yangu na kutimiza wajibu wangu zilikuwa sawa na za Mafarisayo, ambazo lazima zilikuchukiza Wewe. Ee, Mwenyezi Mungu! Niko tayari kugeuza nia zangu mbovu na dhana chini ya uongozi wa neno Lako. Niko tayari kutimiza wajibu wangu kama kiumbe aliyeumbwa na kufuata mfano wa Petro kwa kufanya kile ninachopaswa kufanya kwa kupitia njia ya kumpenda Mungu, bila tena kufanya kazi katika nafasi yangu kama kiongozi, na kufanya kila ninaloweza kutafuta na kuendelea mbele kwelekea njia ya Petro!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Masumbuko Makali ya Milele

“Roho zote ambazo zimepotoshwa na Shetani ziko chini ya udhibiti wa miliki ya Shetani. Ni wale tu wanaomwamini Kristo ndio waliotengwa...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp