Maneno ya Mungu Yaliondoa Dhana Zangu
Nilipokuwa nikihubiri injili nilikutana na viongozi wa dini ambao walisema uongo ili kupinga na kuvuruga, na kuwaita polisi. Hili lilisababisha wale niliokuwa nikihubiria kutothubutu kuwasiliana nasi, na wale ambao walikuwa tu wameikubali injili kutoweza kuwa na imani katika kazi ya Mungu. Nilipofanya kazi kwa bidii sana lakini matokeo yalikuwa duni, nilifikiri: kazi ya Kiinjili ni ngumu sana kutekeleza. Lingekuwa jambo la kustaajabisha sana kama Mungu angeonyesha miujiza kiasi na kuwaadhibu wale ambao husema uongo pamoja na wale ambao kwa uzito kabisa humpinga Mungu kuwaonyesha wale ambao wamedanganywa. Basi si kazi ya injili ingetekelezwa kwa haraka zaidi? Haingekuwa vigumu sana kwetu kuhubiri injili…. Ndiyo maana tumaini hili lilikuja moyoni mwangu kila wakati nilipokutana na aina hizi za matatizo. Baadaye, nilisoma kitabu cha mifano ya adhabu na wakati wa ushirika nikasikia ushahidi wa baadhi ya ishara na maajabu ya Mungu, na nilifurahi sana moyoni mwangu. Nilitumaini hata zaidi kwamba Mungu angefanya mambo fulani katika maeneo ambayo nilifanyia kazi ili kwamba mashaka ya kazi yetu ya injili yangeweza kutatuliwa kwa haraka zaidi. Lakini bila kujali jinsi nilivyotarajia, bado sikuona Mungu akifanya miujiza yoyote hapa au kuwaadhibu watu waovu. Watu wa dini walikuwa bado wanampinga Mungu kabisa, na matatizo katika kazi ya kiinjili yalikuwa bado ni makubwa. Nikawa hasi juu ya hili: Kwa nini Mungu hafungui njia kwa ajili yetu? Ingewezekana kuwa imani yetu haitoshi?
Baadaye, wakati wa sala zangu nikaona maneno haya ya Mungu: “Sasa, kama Mungu angetekeleza ishara na maajabu ya miujiza, basi, bila kulazimika kuanza kazi yoyote kubwa, Angemlaani tu mtu kufa kwa kinywa Chake Mwenyewe, mtu huyo angekufa papo hapo, na kwa njia hii kila mwanadamu angeridhishwa; lakini hili halingetimiza lengo la Mungu katika kuwa mwili. Kama Mungu angefanya hili kweli, binadamu hawangeweza kamwe, kwa akili zao za kufahamu, kuamini kuweko Kwake, haungeweza kamwe kuamini kweli, na zaidi ya hayo ungedhania kwamba shetani ni Mungu. Hata la muhimu zaidi, binadamu hawangeijua tabia ya Mungu kamwe: Je, hiki si kipengele kimoja cha maana ya Mungu kuwa ndani ya mwili? Kama binadamu hawawezi kumjua Mungu, basi daima itakuwa Mungu asiye dhahiri, Mungu wa miujiza, ambaye Ana utawala mkubwa katika ufalme wa binadamu: Hili halingekuwa suala la fikira za mwanadamu kummiliki mwanadamu? Au, kulitamka hili tena kwa dhahiri zaidi, Shetani, ibilisi, hangekuwa ana utawala mkubwa? ‘Kwa nini Nasema Narejesha mamlaka Yangu? Kwa nini Nasema kwamba kupata mwili kuna maana nyingi sana?’ Wakati ambapo Mungu hupata mwili, huo ndio wakati ambapo Hurejesha mamlaka Yake; pia ni wakati ambapo uungu Wake hujitokeza moja kwa moja kufanya kazi Yake. Hatua kwa hatua, kila mwanadamu huja kumjua Mungu wa vitendo, na kwa ajili ya hili nafasi inayoshikiliwa na Shetani ndani ya moyo wa mwanadamu hukandamizwa kabisa huku nafasi ya Mungu ikikuzwa” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 6). Wakati nikijaribu kuyaelewa maneno ya Mungu, moyo wangu ghafla ukachangamka: Inaonekana kwamba madhumuni ya kazi ya Mungu katika mwili sio kutumia mamlaka Yake kuwaogopesha watu ili kiutii, lakini ni kuifungua kabisa tabia Yake kwa wanadamu kupitia kazi halisi na maneno, na kwa njia hii kufukuza picha iliyo katika mioyo ya wanadamu ya Mungu asiye yakini. Ni kuwaruhusu watu kulegeza vikwazo vya mawazo yao, kutambua kwa kweli tabia na kazi ya Mungu, kuwaruhusu watu kuwa na ukweli na ufahamu, na hivyo kuwashinda na kuwachuma. Kazi ya Mungu kwa kweli ni ya vitendo mno, na hekima Yake ni isiyoeleweka kwa wanadamu! Hebu ifikirie kwa manini—kazi hii ambayo Mungu anafanya haingezaa matunda kama ingefanywa kupitia ishara na maajabu. Kama tu vile katika Enzi ya Sheria, Mungu aliwaonyesha Waisraeli miujiza mingi sana na kuwaadhibu wengi sana wa wale waliomkataa Yeye, lakini Waisraeli bado hawakumtambua Mungu na hatimaye walienda kufa jangwani. Katika Enzi ya Neema, Mungu pia alionyesha ishara nyingi mno na maajabu kati ya Wayahudi, lakini bado walimsulubisha akiwa hai kwa sababu hawakumtambua Yeye. Hili lote lasema kwamba ishara za Mungu na maajabu vyaweza tu kuwaogofya watu kwa muda mfupi, lakini sio msingi wa imani yao kwa Mungu. Hata hivyo, ingawa nimemfuata Mungu hadi sasa, sijawa na ufahamu hata chembe wa asili ya Mungu, na nimeelewa hata machache ya malengo na umuhimu wa kazi ya Mungu katika mwili. Mimi bado nimeamini katika mamlaka Yake na kwamba yeyote ambaye humpinga Mungu ataadhibiwa, hivyo nimefuatilia kikamilifu kuona ishara za Mungu na maajabu. Si aina hii ya imani hasa kama Mafarisayo, wakiishi katikati ya hali ya mashaka, wakiamini katika Mungu wa miujiza wakati ule ule wakimpinga Mungu wa vitendo? Kama ukimbizaji wangu wa Mungu ungeendelea kwa njia hii, ningewezaje kulingana na Mungu wa kweli? Kwa kweli ilikuwa ni hatari sana! Baada ya hapo, Niliona zaidi ya maneno ya Mungu: “Ni vigumu kabisa kwa Mungu kutekeleza kazi yake katika nchi yenye joka kuu jekundu, lakini ni kupitia ugumu huu ndipo Mungu Hupiga hatua katika kazi Yake ili kudhihirisha hekima Yake na matendo Yake ya ajabu. Mungu Huchukua fursa hii kuwakamilisha watu hawa wa kikundi hiki. Kwa ajili ya mateso ya watu, tabia yao na hulka ya kishetani ya watu katika nchi hii najisi, Mungu Anafanya kazi Yake ya kutakasa na ushindi, ili, kutokana na hili, apokee utukufu na kuwapata wale wote wanaoshuhudia matendo Yake. Huu ndio umuhimu wa kujitoa kwa Mungu kwa ajili ya kikundi hiki cha watu. Ina maana kuwa Mungu hufanya kazi ya ushindi kupitia wale wanaompinga. Kufanya vile tu ndiko kunaweza kudhihirisha nguvu kuu za Mungu. Kwa maneno mengine, ni wale tu walio katika nchi najisi ndiyo wanaostahili kuurithi utukufu wa Mungu na ni hili tu ambalo litafanya nguvu kuu za Mungu kuwa maarufu. Ndiyo maana Nasema kuwa utukufu wa Mungu unapatikana katika nchi najisi na kwa wale wanaoishi humo. Haya ndiyo mapenzi ya Mungu. Hii ni kama tu ilivyokuwa katika kazi ya Yesu; Angetukuzwa tu kati ya Mafarisayo waliomdhihaki. Isingelikuwa mateso na usaliti wa Yuda, Yesu asingelidhihakiwa na kudharauliwa, na hata zaidi kusulubiwa, na hivyo asingelipokea utukufu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?). Kwa wakati huu, kutoka kwa maneno ya Mungu nilikuwa na ufahamu zaidi kwamba bila kujali ni kazi gani Mungu hufanya, yote ina maana. Akikamilisha kazi ya kufichua miujiza kiasi au kugawa adhabu kiasi, ina maana, ina kanuni. Asipokamilisha kazi ya kufichua miujiza au kugawa adhabu, basi ina hata zaidi ya hekima ya Mungu. Sasa, Mungu hayatumii mamlaka Yake kuwaondoa wale wanaosema uongo au kumpinga Yeye kwa uzito; kuna zaidi ya ukarimu wa Mungu. Mungu hutumia matatizo haya kutuwezesha kuonja shida za kazi Yake mwenyewe, hivyo kutambua wema na uzuri wa Mungu. Mungu pia hutumia matatizo haya kukamata ushahidi wa watu wakifanya mema au maovu, na hatimaye kuwapa hatima inayofaa ili tuwe na uhakika kabisa, ili tuweze kuona haki na utakatifu wa Mungu. Zaidi ya hayo, Mungu hutumia matatizo haya kufichua kwamba nimepungukiwa na ukweli wa maono, kwamba asili yangu ni vivu sana, oga, jinga, na ya kipumbavu, na kwamba kwa njia ya mateso yangu, jitihada, na ushirikiano na Mungu, Atatutolea ufahamu , imani, upendo, hekima, na ujasiri, na hata zaidi Atatupa ukweli wa kazi ya Mungu, na hivyo kutukamilisha, kutupata. Kazi ya Mungu kwa kweli ni yenye busara, ya ajabu sana! Lakini mimi ni kipofu sana—sina ufahamu wa umuhimu wa kazi ya Mungu na nia Zake nzuri. Yote ninayoogopa ni mateso ya kimwili na sitaki kushirikiana na Mungu. Mimi kwa kweli ni muumini ambaye hatekelezi kazi ya kufaa na ambaye husherehekea katika faraja!
Shukrani iwe kwa kunurishwa kwa maneno ya Mungu ambayo yalinipa utambuzi kiasi wa madhumuni na hekima katika kazi ya Mungu katika mwili na pia yakaniruhusu kuona kwamba imani yangu katika Mungu ilikuwa ikiishi katika hali ya mashaka, kwamba kutomtambua Mungu ni hatari sana! Kuanzia siku hii kwendelea, ninahiari kujiandaa na ukweli wa maono, kufuatilia kuwa mtu anayeitambua kazi ya Mungu na tabia, kwa kweli kumiliki hiari ya kuteseka, kutekeleza wajibu wangu kwa lile linalowezekana ili kuufariji moyo wa Mungu.
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?