Watu Wasio na Hila Sio Lazima Wawe Waaminifu

14/01/2018

Cheng Mingjie Jiji la Xi’an, Mkoa wa Shaanxi

Mimi hujiona kuwa mtu wa aina ya kuwa wazi na mchangamfu. Mimi huzungumza na watu kwa njia ya waziwazi; chochote ninachotaka kusema, mimi husema—mimi sio aina ya mtu wa kuzungukazunguka. Katika kuingiliana kwangu na watu mimi huwa ni mwaminifu na wazi kiasi. Mara kwa mara, mimi hudanganywa na kudhihakiwa kwa sababu ya kuwaamini wengine kwa urahisi. Ilikuwa tu baada ya kuanza kwenda kanisani nilipopata mahali ambapo ningepaita pangu. Nilijiwazia mwenyewe: “Katika siku za nyuma kutokuwa na hila kwangu kumenifanya mwenye kuweza kudhuriwa na udanganyifu wa wengine; lakini katika kanisa Mungu anataka watu waaminifu, kwa hivyo mimi si lazima niwe na wasiwasi tena juu ya kuwa maasumu.” Nilihisi faraja hasa niliposikia kwamba Mungu anawapenda wale waaminifu na sahili, na kwamba ni waaminifu tu watakaopata wokovu wa Mungu. Nilipoona jinsi ndugu zangu wa kiume na wa kike walivyokuwa na majonzi walipoanza kutambua asili yao ya udanganyifu lakini hawakuweza kuibadilisha, nilihisi kufarijika hata zaidi kwamba, kuwa mwaminifu na waziwazi, isingenibidi kupitia majonzi kama hayo. Siku moja, hata hivyo, baada ya kupokea ufunuo kutoka kwa Mungu, hatimaye niligundua kwamba sikuwa mtu mwaminifu niliyedhani nilikuwa.

Siku moja, nikasikia Mungu akisema katika ushirika wake: “Watu ambao ni waaminifu wanamiliki ukweli, wao si watu wa kuhuzunisha, wanyonge, wajinga, ama wenye mioyo mikunjufu. … Na hivyo, usiliweke taji hili juu ya kichwa chako, ukifikiri kwamba wewe ni mwaminifu kwa sababu unateseka katika jamii, unabaguliwa na kusumbuliwa na kudanganywa na kila mtu unayekutana naye. Hii si sahihi hata kidogo. … Kuwa mwaminifu si kama wanavyofikiria watu: Watu si waaminifu tu kwa sababu wao ni wanyofu na wanashughulika kwa udhahiri. Watu wengine kiasili wanaweza kuwa wazi sana katika njia wanayozungumza, lakini kuwa kweli hakumaanishi wako bila udanganyifu. Udanganyifu ni motisha ya watu, na tabia yao. Wakati watu wanaishi katika dunia hii chini cha ushawishi wa Shetani, haiwezekani kwa wao kuwa waaminifu; wanaweza kuwa wadanganyifu zaidi tu(“Vitendo vya Msingi Kabisa vya Kuwa Mtu Mwaminifu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalikuwa mfano kamili wa hali yangu. Kwa hakika, daima nilifikiri kuwa kwa sababu huwa sizungumzi kwa kurudiarudia na mara nyingi huchukiwa na wengine, kwamba hili kwa namna fulani linamaanisha hakuna sehemu yangu ambayo ni danganyifu au ya hila. Matokeo yake yakiwa, sikuhusisha mimi binafsi kamwe na ufafanuzi wa Mungu wa udanganyifu na hila katika mwanadamu, badala yake nikijiweka taji kama mfano kamili wa uaminifu. Nilidhani kuwa kila mtu mwingine alikuwa mdanganyifu na kwamba mimi kwa namna fulani nilikuwa tofauti, kwamba nilikuwa nimezaliwa na uaminifu huu wa asili. Kufikiria kwangu kulimchukiza Mungu. Wakati huu, nilikumbuka kifungu kingine cha maneno ya Mungu: “Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu. … Kama maneno yako yamejaa visingizio na udhibitisho usio na thamani, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye huko radhi kabisa kuweka ukweli katika matendo. Kama wewe una siri nyingi usizotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—yaani, ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hataweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi. Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mwaminifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu). Maneno ya Mungu yalinifanya nielewe kwamba kwa kweli kile Mungu humaanisha kwa uaminifu, ni mtu ambaye hutoa moyo wake kwa Mungu bila wazo kwa maendeleo yake binafsi au mipango ya baadaye. Hakuna kufanya biashara na Mungu, hakuna kudai baada ya malipo: Mtu mwaminifu huishi ili kumridhisha Mungu. Mtu mnyofu ni mwaminifu mno kwa Mungu na huwa hajaribu kamwe kumdanganya Yeye. Katika kutimiza majukumu yao ana bidii na huwa haajaribu kamwe kuepuka kufanya jambo kwa kusingizia au kufanya kitu kwa namna isiyo ya dhati. Waaminifu hujionyesha wazi katika vitu vyote mbele ya Mungu, na pia wako tayari kushiriki masuala yao ya faragha na matatizo yao ya binafsi na ndugu zao wa kiume na wa kike. Watu waaminifu huwa hawasimulii hadithi zilizohafifishwa, huwa wanasema waziwazi. Watu waaminifu hushikilia ukweli na ni wema. Kwa upande wangu, sikujua hasa maana ya kuwa mtu mwaminifu. Katika kushutumu kwangu kwa kidunia kwa vitu, “mtu mwaminifu” wa Mungu alikuwa kile tunachokitaja katika ulimwengu wa kidunia kama “mtu maasumu.” Sikujua hata kidogo kwamba “mtu mwaminifu” wa Mungu na “mtu mwaminifu” wangu walikuwa tofauti. Jinsi nilivyokuwa mjinga, jinsi nilivyokuwa mpuuzi!

Shetani amempotosha mwanadamu kwa miaka elfu kadhaa: Sote hukua katika mazingira yaliyojaa kinyaa na uovu wa Shetani. Maneno na tabia zetu, jinsi tunavyojiendesha katika jamii, yote yako chini ya amri ya Shetani. “Fikiria kabla ya kutamka na kisha uzungumze kwa kujizuia,” “Kila mtu ajitetee mwenyewe bila kujali jaala ya wengine,” “Nena bila msimamo,” misemo hii maarufu sana ya Shetani tayari imejiingiza kwa pamoja katika sehemu za wanadamu zisizofikika: ni sehemu muhimu ya maisha yetu hata inapotuongoza kwa udanganyifu na hila. Kutokana na ukweli kwamba wanadamu wote wanaumizwa na udanganyifu na hila, ni nini kilichonifanya nifikirie kuwa kwa namna fulani sikuweza kudhurika, au nilikuwa mwaminifu kiasili? Mimi husema kwa wazi na bila kuwapotosha watu kwa sababu mimi ni mtu wa kusema kweli na dhahiri. Mara nyingi mimi hudanganywa na wengine kwa sababu mimi ni mjinga na mpumbavu, lakini hii haimaanishi kwamba mimi kwa kweli ni ni mtu mwaminifu. Ninapofikiri nyuma, ni mara ngapi nimetumia hila na uongo ili kuhifadhi sifa yangu na hadhi? Ni mara ngapi nimezama katika wasiwasi juu ya matumaini yangu ya baadaye badala ya kumwamini Mungu kwa moyo safi na mmoja? Niliogopa kwamba kwa kutoa kila kitu kwa ajili ya Mungu, kwamba ningeachwa bila kitu, hivyo siku zote nilitaka ahadi kutoka kwa Mungu, hakikisho kwamba siku moja ningeingia katika ufalme Wake. Ni kwa njia hiyo tu ningeweza kutafuta ukweli kikamilifu bila wasiwasi. Ni mara ngapi sikuwa mwaminifu kwa Mungu, nikihangaika juu ya hasara na faida ndogo katika mchakato wa kutimiza majukumu yangu? Na ni mara ngapi nilifanya na kuvunja maazimio, nikisema “maneno yenye kuvutia lakini matupu” ili kujipendekeza kwa Mungu? Ni mara ngapi niliepuka kuwasiliana kwa dhatina ndugu zangu wa kiume na wa kike na kushiriki matatizo yangu binafsi na masuala ya faragha nao kwa hofu ya kwamba wangeniangalia kwa dharau? Ni mara ngapi nilisema yale tu niliyoamini yangenizalia manufaa ya binafsi, nikiwa mwangalifu na kuwa mwenye shaka na wengine? … Kuangalia nyuma, ilionekana kuwa mawazo yangu, maneno na vitendo vyote vilijawa na udanganyifu na ulaghai. Matokeo yake yakiwa, fikra yangu ya imani, michango yangu, kuingiliana kwangu na wengine na Mungu na utimizaji wa wajibu wangu vyote vilikuwa vimeambukizwa udanganyifu. Unaweza kusema kuwa nilikuwa nikiishi kila wakati kwa mujibu wa kiini cha udanganyifu. Mimi si mtu mwaminifu hata kidogo.

Asante Mungu kwa kunipatia nuru, kwa kunionyesha kwamba watu waaminifu sio tu wale wa kusema kweli na maasumu, bali wamilikio ukweli na ubinadamu. Asante pia kwa kunionyeshea kwamba mimi si mwaminifu kwa ufafanuzi wa Mungu, lakini ni mtu anayeteswa na asili ya udanganyifu ya Shetani, udanganyifu ambao Mungu ameufichua. Ewe Mungu, tangu sasa kuendelea nitajiwekeza ktika kuwa mtu mwaminifu. Ninaomba Uniweke wazi na uniruhusu kuwa na ufahamu wa kina wa asili yangu mwenyewe ya udanganyifu, ili nipate kujidharau, kuunyima mwili wangu, na hivi karibuni niwe mtu mwaminifu anayemiliki ukweli na ubinadamu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mabadiliko ya Mwigizaji

Mwenyezi Mungu anasema, “Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda...

Kuishi Mbele za Mungu

Na Yongsui, Korea ya Kusini Mwenyezi Mungu anasema, “Ili kuingia katika uhalisi, mtu lazima apindue vitu vyote kuelekea maisha halisi....

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp