Jinsi Mtu Anavyopaswa Kuchukulia Wajibu Wake

24/01/2021

Na Zheng Ye, Korea ya Kusini

Muda mfupi baada ya kuwa muumini, niliwaona ndugu ambao walikuwa viongozi wakifanya mikutano na kushiriki juu ya ukweli mara nyingi, na wengine walikuwa na wajibu ambao ulihitaji ustadi, kama vile kutengeneza video, au kuimba na kucheza. Niliwapenda sana na nilidhani kuwa hilo lilikuwa jambo la kustahi. Kuhusiana na wale waliofanya wajibu wa kuwa wenyeji au kushughulikia maswala ya kanisa, wajibu huo haukuwa wa maana na haukuwa wa utaalamu, kwa hivyo hawangejipatia sifa kamwe. Nilidhani kuwa katika siku za usoni, ningependa wajibu ambao ungefanya nionekane kuwa mzuri. Miaka miwili baadaye nilipewa wajibu wa kuandika. Nilifurahi sana, hasa wakati ambapo, kila nilipokwenda kanisani kutoa mwongozo juu ya kazi ya uandishi, ndugu wote walikuwa wema kwangu na walinitazama kwa kusifu. Nilifurahishwa sana nami mwenyewe, na nikahisi kwamba wajibu wangu ulivutia zaidi kuliko wa wengine. Mnamo 2018, nilipelekwa katika eneo lingine kutekeleza wajibu wangu. Nilipokuwa huko, wakati mmoja ndugu alipogundua wajibu wangu ulikuwa gani, alianza kuzungumza nami kuuhusu. Kuona jinsi alivyoniheshimu kulinifurahisha sana, na nilihisi kwamba kutekeleza wajibu huo kwa kweli kulikuwa heshima.

Nilikuwa katika hali ya kujisikia siku zote na kujishauwa wakati huo. Nilikuwa nikipigania heshima na faida katika wajibu wangu na kutouchukulia kwa makini. Niliachishwa kazi miezi michache baadaye kwa sababu sikuwa nikifanikisha chochote. Hiyo iliniacha nikiwa nimefadhaika sana na hasi kidogo, kwa hivyo kiongozi alishiriki nami juu ya mapenzi ya Mungu, na akasema, “Nyumba ya Mungu inahitaji watu wafanye kazi kama wasaidizi wa jukwaa wa filamu zetu. Unaweza kufanya hivyo. Bila kujali wajibu wako ni upi, lazima ufuatilie ukweli na utie juhudi za mchwa katika kutekeleza wajibu wako vizuri.” Ndiyo. Sikujua kabisa wajibu huo ulihusu nini, lakini nilijua kuwa nilipaswa kutii tu, kwa sababu kiongozi alikuwa amepanga hayo. Baada ya kuwa mwandalizi wa jukwaa kwa muda niligundua kwamba kazi nyingi sana ilikuwa kazi ngumu ya kusogeza kila aina ya vitu vya kutumia katika mandhari ya filamu kila mahali. Hakukuwa na ujuzi wowote uliohusika. Ilihusisha kutembea kwingi na kazi za pembeni. Niliwaza, “Hapo awali, wajibu wangu wa uandishi ulihitaji nitumie ubongo wangu. Ulikuwa wa heshima na kustahiwa. Kuhamisha vyombo hivi vyote ni kazi ngumu ya kimwili. Ni chafu na inachosha. Je, ndugu watanidharau?” Nilisononeka nilipofikiria hilo na nilihisi upinzani mdogo kuhusu kufanya wajibu huu. Kuanzia wakati huo na kuendelea, nilifanya kazi shingo upande, na kuukwepa nilipoweza. Wakati mwingine tulipokosa chombo cha kutumia kwa uigizaji na kulazimika kuazima kutoka kwa ndugu, nilimfanya mtu mwingine akiazime, nikiogopa kwamba iwapo ningefanya hivyo mwenyewe, kina ndugu ambao walinijua wangegundua kuwa nilikuwa nimebadilishwa kutoka katika wajibu wangu wa zamani, na kwamba sasa nilikuwa nikifanya kazi za pembeni ya katika mandhari ya filamu. Kisha wangefikiri nini kunihusu? Sikutaka pia kupata ujuzi uliofaa, nikiogopa kwamba iwapo ningejifunza zaidi, ningefanya wajibu huo milele, na siku yangu ya kujitokeza isingekuja. Wakati mwingine tulipokuwa kwenye mandhari ya filamu, mwelekezi aliniomba niandae vifaa vya uigizaji kwa njia maalum. Hii daima ilinifanya nihisi nisiye na raha sana, kana kwamba ilikuwa aibu kwangu. Nilifikiria jinsi ambavyo hapo awali, katika wajibu wangu wa uandishi, wengine waliniheshimu na kufuata mwongozo wangu, lakini sasa mimi ndiye niliyekuwa nikiambiwa la kufanya. Kulikuwa kushushwa cheo kwa kweli. Wakati mmoja, ndugu mmoja aliniagiza niende nje kuchukua mabua kwa ajili ya mandhari ya filamu. Sikutaka kabisa kufanya hivyo. Niliwaza, “Kuenda nje kufanya jambo hilo kunaaibisha sana. Kina ndugu wakiniona nikifanya hilo, hakika watafikiri mimi ni mtu aliyeshindwa, anayefanya jambo la aina hiyo katika umri mdogo sana.” Lakini kwa kuwa kazi hiyo ilihitaji kufanywa kwa ajili ya wajibu wangu, nilingoja tu hadi wakati ambapo hakukuwa na mtu yeyote karibu na nikajipa ujasiri wa kuifanya. Nilimwona ndugu mmoja akija nilipokuwa nikikusanya mabua. Alikuwa amevalia viatu vya ngozi na soksi nyeupe—alionekana safi kabisa. Mimi, kwa upande mwingine, nilikuwa mchafu toka utosini hadi kidoleni. Nilivunjika moyo na kufadhaika ghafla, nikiwaza, “Sisi ni wa umri sawa, lakini anafanya wajibu mzuri na safi, wakati ambapo naweza tu kufanya kazi chafu kama kukusanya mabua. Tofauti kubwa kama nini! Aibu iliyoje! Nitarudi kumwambia kiongozi kwamba sitaki kufanya wajibu huu tena, na nimsihi anipe wajibu mwingine.”

Baada ya kurudi nilihisi mgongano moyoni mwangu kwa kweli, nikijiuliza iwapo nilipaswa kumwambia kiongozi jambo. Iwapo singemwambia, ningelazimika kuendelea kufanya wajibu huo, lakini iwapo ningeongea na kusema sikutaka kuufanya, huko kungekuwa kutelekeza wajibu wangu. Kwa kuzingatia hilo, nilificha hisia zangu na sikusema chochote. Muda mfupi baadaye, kiongozi alipanga wasaidizi wa jukwaa na wa waigizaji wahudhurie mikutano pamoja. Sikufurahia hilo hata kidogo. Waliweza kujipatia heshima na kufurahia kuonekana huku mimi nikifanya kazi za pembeni. Hatukuwa kwenye kiwango sawa kabisa. Je, si kukusanyika pamoja kungeonyesha waziwazi hali yangu duni? Kila mtu alihusika kwa dhati katika mikutano, lakini sikutaka kushiriki chochote. Nilipokuwa mikutanoni pamoja na waigizaji, nilihisi kama nilisaidia tu kuwafanya waonekane kuwa bora. Jambo hili lilisikitisha. Kadiri muda ulivyoendelea, giza lililokuwa katika roho yangu liliongezeka na sikutaka hata kuhudhuria mikutano tena. Nilikumbuka mara nyingi wakati niliokuwa nikifanya wajibu wa uandishi, nilipokuwa nikisalimiwa kwa shauku na ndugu na kuthaminiwa na kiongozi. Tangu nilipoachishwa wajibu huo, nilikuwa nikifanya tu kazi za pembeni, na hakuna aliyenistahi tena. Nilivunjika moyo na kutaabika, nikizidi kuhisi kama mtu wa hali ya chini na asiyepatana na watu. Nilikuwa mwenye huzuni kila wakati, na sikuhisi vizuri kabisa. Nilipunguka uzito mwingi haraka sana. Jioni moja, nilipokuwa nikitembea peke yangu, sikuweza kabisa kuzuia maumivu yangu tena. Huku nikilia, nilimwomba Mungu, “Ee Mungu! Hapo zamani, nilikuwa nimeazimia kufuatilia ukweli na kutekeleza wajibu wangu ili kukuridhisha, lakini sasa kwa kuwa hakuna nafasi ya kujionyesha katika wajibu wangu, mimi huhisi kuwa duni kuliko wengine kila wakati. Mimi ni hasi na dhaifu sana, na nahisi kana kwamba nimekaribia kukusaliti wakati wowote. Mungu, sitaki kuendelea kuwa hasi, lakini sijui la kufanya. Tafadhali niongoze kutoka katika hali hii.”

Baada ya hapo, nilisoma haya katika maneno ya Mungu: “Wajibu hutokeaje? Kuongea kwa mapana, wajibu hutokea kama matokeo ya kazi ya Mungu ya usimamizi ya kuwaletea binadamu wokovu; kuongea mahsusi, kazi ya Mungu ya usimamizi inapoendelea kati ya wanadamu, kazi mbali mbali huibuka ambazo zinahitaji kufanywa, na zinahitaji watu washirikiane na kuzikamilisha. Hili limesababisha kuibuka kwa majukumu na misheni ya watu kutimiza, na majukumu na misheni hizi ndio wajibu ambao Mungu huwapa wanadamu(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Bila kujali wajibu wako ni upi, usibague kati ule wa juu na wa chini. Tuchukulie kwamba unasema, ‘Ingawa kazi hii ni agizo kutoka kwa Mungu na ni kazi ya nyumba ya Mungu, nikiifnya, watu wanaweza kunidharau. Wengine wanapata kufanya kazi ambayo inawafanya watokezee. Je, kazi hii ambayo nimepewa, ambayo hainifanyi nitokezee lakini inanisababisha nifanye kazi kwa bidii pasipo kuonekana, inawezaje kuitwa wajibu? Huu ni wajibu ambao siwezi kukubali; huu sio wajibu wangu. Wajibu wangu laziwa uwe ule unaonifanya nitokezee mbele ya wengine na uniruhusu nijipatie jina—na hata nisipojijengea jina au kutokezea, bado lazima nifaidike kutoka kwa wajibu huo na niwe huru kimwili.’ Je, huu ni mtazamo unaokubalika? Kuwa mwenye kuchaguachagua si kukubali kile kinachotoka kwa Mungu; ni kufanya uchaguzi kulingana na upendeleo wako mwenyewe. Huku si kukubali wajibu wako; ni kukataa wajibu wako. Mara tu unapojaribu kuchaguachagua, huwezi tena kuwa na kukubali kwa kweli. Kuchaguachagua kama huko kumechanganywa na upendeleo na matamanio yako ya binafsi; unapozingatia masilahi yako mwenyewe, sifa yako, na kadhalika, mtazamo wako kuelekea wajibu wako sio mtiifu. Huu hapa ni mtazamo kuelekea wajibu: Kwanza, huruhusiwi kuuchambua, au kufikiria ni nani aliyekupa wajibu huo; badala yake, unapaswa kuupokea kutoka kwa Mungu, kama wajibu wako na kama kile unachopaswa kufanya. Pili, usibague kati ya ule wa juu na ule wa chini, na usijishughulishe na asili yake—iwe unafanywa mbele ya watu au pasipo watu kuona, uwe unakufanya utokezee au la. Usifikirie kuhusu mambo haya. Hizi ndizo sifa mbili za mtazamo ambao watu wanapaswa kuchukulia wajibu wao(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kusoma haya kulinionyesha kuwa nilikuwa na maoni na mtazamo mbaya kwa wajibu wangu. Mungu anatutaka tutekeleze wajibu wetu, na ni sawa na sahihi tuufanye. Hatutakiwi kuwa na chaguo katika jambo hilo. Lakini niliacha upendeleo wangu unizuie, nikitaka tu wajibu ambao unapendwa na kuheshimiwa. Nilipinga na kukataa kitu chochote kilichokuwa hakionekani na watu au cha kawaida. Sikutii sheria na mipango ya Mungu. Nilikuwa hata mzembe, hasi na nilikataa kufanya kazi, na nilikuwa nikimpinga Mungu. Nilikumbuka nilipokuwa mgeni katika imani. Niliwahusudu viongozi, na ndugu ambao walikuwa wakiigiza. Nilidhani wajibu huo ulikuwa na uzito sana na ulipendwa na wengine, na kwamba watu waliofanya kazi duni za kimwili hawakuwa na ujuzi halisi muhimu. Wajibu wa aina hiyo ulikuwa duni, na watu waliudharau, niliwaza. Kwa kuwa nilikuwa nimepotoshwa katika kufikiri kwangu, nilikuwa nimeainisha wajibu katika madaraja tofauti, kwa hivyo nilipoanza kufanya kazi kama msaidizi wa jukwaa nilidhani kuwa nilikuwa nikifanya tu kazi duni za pembeni na hilo lingeharibu sifa na hadhi yangu. Nilipinga kabisa hilo na sikutaka kutii. Sikuwajibikia wajibu wangu na sikutaka kujifunza ujuzi ambao nilipaswa kujifunza. Nilifikiria hata kukubali kushindwa na kumsaliti Mungu. Niliona kuwa nilijali tu kuhusu upendeleo wangu wa binafsi katika wajibu wangu, na kwamba nilifikiria tu majivuno na heshima yangu, na masilahi yangu. Nilikosa kabisa utiifu wa kweli, sembuse kuyafikiria mapenzi ya Mungu au kutekeleza wajibu wangu vizuri. Mtazamo wangu ulikuwa wa kuudhi na kuchukiza sana kwa Mungu! Kugundua hili kulinifadhaisha, na nilijisuta.

Baadaye nilisoma maneno haya ya Mungu: “Wanadamu ni viumbe walioumbwa. Je, kazi za viumbe walioumbwa ni nini? Hili linagusa utendaji na wajibu wa watu. Wewe ni kiumbe aliyeumbwa; Mungu amekupa kipawa cha uimbaji. Anapokutumia kuimba, unapaswa kufanya nini? Unapaswa kukubali kazi hii ambayo Mungu amekuaminia na uimbe vizuri. Mungu anapokutumia kueneza injili, unakuwa nini kama kiumbe aliyeumbwa? Unakuwa mwinjilisti. Anapokuhitaji uongoze, unapaswa kuchukua agizo hili; kama unaweza kutimiza wajibu huu kulingana na kanuni za ukweli, basi hii itakuwa kazi nyingine unayotumikia. Watu wengine hawaelewi ukweli wala kuufuatilia; wanaweza tu kufanya juhudi. Kwa hivyo, kazi ya viumbe hao walioumbwa ni nini? Ni kufanya juhudi na kutoa huduma(“Ni kwa Kutafuta Ukwelitu Ndiyo Mtu Anaweza Kujua Matendo ya Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kutoka katika maneno ya Mungu, nilijifunza kwamba wajibu wowote ambao mtu hufanya katika nyumba ya Mungu, uwe unaonekana ni wa kusifika au la, kuna majina tofauti na kazi za wajibu tu, lakini jukumu lao la binafsi linabakia kuwa lile lile. Utambulisho na kiini cha asili cha mtu havibadiliki—atakuwa kiumbe daima. Nilikuwa kiumbe katika wajibu wangu wa uandishi, na bado nilikuwa kiumbe katika wajibu wangu wa kuandaa jukwaa. Hakuna utawala msonge katika wajibu ndani ya nyumba ya Mungu, na yote hupangwa kulingana na kile kinachohitajika, na kulingana na kimo, ubora wa tabia na nguvu ya mtu binafsi. Bila kujali ni wajibu gani, mapenzi ya Mungu ni kwamba tufanye wajibu wetu kwa moyo wote kwa kweli, kwamba tusidhoofike katika ufuatiliaji wetu wa ukweli, tukitatua tabia zetu potovu na kufanya wajibu wetu pia. Kama inavyosema katika maneno ya Mungu, “Shughuli si za aina moja. Kuna mwili mmoja. Kila mmoja hufanya kazi yake, kila mmoja kwa nafasi yake na kufanya kadiri ya uwezo wake—kila cheche ya shauku mwako wa mwanga—kutafuta ukomavu katika maisha. Ni hivyo ndivyo nitakavyoridhika(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 21). Kiongozi wa kanisa alinipangia nifanye wajibu wa mwandalizi wa jukwaa kwa kuwa hiyo ndiyo ilihitajika katika kazi hiyo na sipaswi kuwa mwangalifu katika kuchagua au kuzua fujo kulingana na upendeleo wangu mwenyewe, lakini napaswa kutii sheria na mipango ya Mungu. Ninapaswa kuandaa vitu vya kutumiwa jukwaani inayohitajika katika program na kutimiza wajibu wangu katika kila onyesho linaloshuhudia Mungu. Hii ndiyo ilikuwa kazi yangu. Mtazamo wangu ulibadilika kidogo baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu na nikaacha yale yaliyokuwa yamenisumbua kwa muda mrefu sana. Pia niliweza kukabili wajibu wangu kwa usahihi. Kuanzia wakati huo, nilitafuta kwa bidii vifaa na habari ya marejeo ili kufanya kazi kulingana na ujuzi, na nilipokuwa mikutanoni pamoja na waigizaji, sikulinganisha tena wajibu wetu, lakini badala yake nilitoa hisia zangu juu ya uasi na upotovu wangu. Nilifanya ushirika kuhusu ufahamu wote niliokuwa nao. Katika wajibu wangu baada ya hapo, wakati mwingine uwoga wangu wa kudharauliwa ulitokeza, na nikagundua kuwa nilikuwa nikiweka wajibu katika tabaka la juu au cha chini tena, kwa hivyo nilimwomba Mungu haraka na kuacha mawazo yangu yasiyofaa, kulenga wajibu wangu, na kutilia umuhimu kumridhisha Mungu. Nilihisi mtulivu na mwenye upungufu wa mawazo sana baada ya kutenda kwa njia hii kwa muda. Sikuhisi tena kuwa kushughulikia mandhari ya filamu na kuhamisha vyombo vya kutumia jukwaani ulikuwa wajibu wa chini. Badala yake nilihisi kuwa Mungu alikuwa amenikabidhi jukumu. Nilikuwa na heshima na kuonea fahari kuweza kufanya wajibu huu, na kufanya wajibu wangu katika utungaji wa filamu ya nyumba ya Mungu.

Nilidhani kuwa nilikuwa nimeongezeka kimo kiasi baada ya kufunuliwa kwa njia hiyo, kwamba ningeweza kutii mipango ya Mungu katika wajibu wangu na singekuwa hasi na mwasi tena kwa sababu wajibu wangu haukuwa wa kipekee. Lakini wakati uliofuata nilipokutana na hali ambayo sikupenda, tatizo hilo la zamani lilitokea tena.

Miezi michache baadaye kulipokuwa msimu wa shughuli nyingi kwa wakulima, kulikuwa na ndugu wengine ambao walikuwa wamekwenda zao kueneza injili na hawakuweza kurudi mapema wakati wa mavuno. Kiongozi aliniuliza iwapo ningewasaidia katika kazi yao ya shamba. Niliwaza, “Hii inaweza kuwapa amani wale ndugu ili waweze kulenga kazi ya injili, na itakuwa na faida kwa kazi ya nyumba ya Mungu. Napaswa kukubali jukumu hili.” Lakini nilipofika shambani, niliona kwamba ndugu wengine waliokuwapo kule walikuwa katika miaka yao 40 au 50. Hakukuwa na mtu hata mmoja aliyekuwa katika miaka yake ya 20, kama mimi. Sikufurahi sana. Wakati huo huo, ndugu mmoja alikuja na kuniuliza, huku akishangaa, “Ndugu, unapataje wakati wa kuja kufanya kazi shambani? Je, hufanyi wajibu wako wa kuandika?” Uso wangu ulianza kuwasha mara moja, na nilijibu haraka, “Nimekuja tu kusaidia kwa muda.” Baada ya yeye kuondoka, niliwaza, “Atafikiri nini kunihusu? Je, atafikiri kwamba kuja kufanya kazi ya aina hii katika umri wangu kunamaanisha sina ubora wowote wa tabia au talanta halisi, na kwamba nipo hapa tu kwa sababu siwezi kuchukua wajibu muhimu? Huko ni kushushwa cheo kwa kweli!” Nilizidi kukerwa. Ingawa nilikuwa nikifanya kazi kimwili, nilizongwa na mawazo kuhusu jinsi ndugu walivyonifikiria kule, na iwapo wangenidharau. Nilifanya kazi kwa njia isiyo ya dhati. Nilipofika nyumbani, niliwaona ndugu wengine wakiwa mbele ya kompyuta wakifanya wajibu wao, na ghafla nikahisi kana kwamba nilikuwa kwenye daraja la chini. Niliwaza, “Wajibu wa watu wengine ni bora kuliko wangu. Kwa nini nalazimika kwenda kufanya kazi kwa bidii shambani? Kwa vyovyote vile, angalau nimefika katika chuo kikuu, na nilijitahidi katika masomo yangu. Je, huko hakukuwa kutoroka hatima ya mkulima ya kufanya kazi shambani siku nzima? Sitaenda kesho.” Nilijua kuwa sikustahili kufikiri kwa njia hiyo, lakini nilihisi kukosewa sana, nikifikiri kwamba kunilazimisha nifanye kazi shambani kulikuwa kutumia vibaya talanta yangu na kulikuwa aibu kwangu. Nilizidi kuchanganyikiwa nilipokuwa nikifikiria hayo, kwa hivyo nilimwomba Mungu, “Mungu, ninahisi kuwa kufanya kazi kwa bidii na kutokwa na jasho nikifanya kazi ya shamba ni wajibu duni ambao wengine watadharau. Sitaki kuufanya tena. Najua mawazo yangu juu ya hili si sahihi, lakini siwezi kujizuia. Ninataabika kwa kweli. Tafadhali nitie nuru na Uniongoze ili nielewe mapenzi Yako na kuyatii.” Baada ya ombi langu, nilisoma haya katika maneno ya Mungu: “Kutii kwa kweli ni nini? Wakati wowote ambapo Mungu anafanya jambo lolote linalokuendea vizuri, na kukuruhusu uhisi kwamba kila kitu ni cha kiridhisha na kinachostahili, na umeruhusiwa kutokeza, unahisi kwamba hili ni jambo la fahari mno, na unasema, ‘Shukrani kwa Mungu’ na unaweza kutii utaratibu na mipango Yake. Hata hivyo, kila unapotumwa mahali pasiposifika ambapo huwezi kutokezea, na ambapo hakuna anayekutambua, basi unaacha kuhisi furaha na unaona vigumu kutii. … Kutii wakati hali zinafaa kwa kawaida huwa rahisi. Ikiwa unaweza pia kutii katika hali ngumu—zile ambazo mambo hayakwendei vizuri na unasononeshwa, ambazo hukufanya uwe dhaifu, ambazo zinakufanya uteseke kimwili na sifa yako iharibike, ambazo haziwezi kuridhisha majivuno na majisifu yako, na zinazokufanya uteseke kisaikolojia—basi kweli una kimo. Je, hili si lengo mnalopaswa kuwa mnafuatilia? Ikiwa mna azimio kama hilo, lengo kama hilo, basi kuna tumaini(Ushirika wa Mungu).

Nilihisi aibu nilipofikiria maneno ya Mungu. Yalikuwa yamefichua kabisa hali yangu mwenyewe. Wakati ambapo nilidhani kwamba ningejionyesha nilipokuwa nikifanya wajibu wangu wa uandishi, nilifurahia sana kuukubali na kutii, na nilitekeleza wajibu wangu kwa shauku. Lakini nilipokuwa nikisaidia shambani, na majivuno na heshima yangu viliathiriwa, nilifadhaika na sikuwa radhi kuufanya. Hasa nilipowaona ndugu wengine wakifanya kazi kwenye kompyuta zao, nilihisi kana kwamba sikuwa hodari kama wao. Nilipoteza usawa wangu, nikifikiri kwamba kwa kuwa nilikuwa na elimu nilipaswa kufanya wajibu wa heshima ambao ulihitaji ujuzi. Nilipinga na kulalamika, na sikutaka kuendelea kufanya kazi ya shamba. Katika wajibu wangu, sikufikiria yale ambayo yangefaidi nyumba ya Mungu, wala sikujali mapenzi Yake. Badala yake, nilifikiria majivuno yangu mwenyewe mara kwa mara. Nilikuwa mbinafsi sana na mwenye kustahili dharau. Sikuwa nikijiona kama mshiriki wa nyumba ya Mungu hata kidogo. Muumini wa kweli anayedhukuru mapenzi ya Mungu huchukulia kufanya wajibu wake kama jukumu la binafsi, akianza kutekeleza wajibu kwa bidii kila anapohitajika, hata kama ni mgumu, unaochosha, au kuhatarisha sifa au maslahi yake. Mradi ni mzuri kwa kazi ya kanisa, yeye huwa na ari ya kuufanya vizuri. Ni watu kama hao pekee wanaomiliki ubinadamu, na huunga mkono nyumba ya Mungu. Niliifikiria kazi yangu ya hivi karibuni ya mavuno ya majira ya majani kupukutika. Ndugu wengine walihitaji msaada, na watu wengine kadhaa wangeufanya wajibu huu pia, kwa hivyo ni kwa nini Mungu alifanya wajibu huu uje kwangu? Si kwamba niliongeza thamani fulani katika kazi hiyo. Lakini Mungu alikuwa akifunua mtazamo wangu kwa wajibu wangu kwa kunifanya nifanye kazi chafu na ya kuchosha ili niweze kutambua upotovu na uchafu wangu ninapokuwa nikifanya wajibu huo, kisha nitafute ukweli ili kutatua tabia yangu potovu. Lakini sikuelewa nia njema ya Mungu. Bado nilikuwa mwenye machagu katika wajibu wangu na kila wakati nilikuwa na upendeleo na matakwa yangu mwenyewe. Sikuweza kutii taratibu na mipango ya Mungu, lakini nilikuwa mwasi na nilimpinga Mungu. Nilimsononesha sana! Nilielewa kwamba mapenzi ya Mungu yalikuwa kufunua na kuitakasa tabia yangu potovu kupitia hali hiyo, na kurekebisha mtazamo wangu kuhusu wajibu wangu. Huu ulikuwa upendo wa Mungu. Haijalishi iwapo ninapewa kazi chafu, inayochosha, au isiyovutia. Mradi inafaidi kazi ya kanisa, ninapaswa kuikubali bila masharti, kutii, na kuifanya kwa bidii. Huko pekee ndiko kuwa mtu mwenye dhamiri na mantiki. Nilipofahamu haya, nilipata utulivu polepole.

Sikuweza kujizuia kutafakari juu yangu mwenyewe: Kwa nini nilikuwa mpinzani na mwenye kufadhaika nilipolazimika kufanya wajibu wa kawaida? Kwa nini sikuwa nimeweza kuukubali na kutii? Katika kutafuta kwangu, nilisoma maneno haya kutoka kwa Mungu: “Shetani huwapotosha watu kwa kupitia masomo na ushawishi wa serikali za kitaifa na walio mashuhuri na wakuu. Upuuzi wao umekuwa uzima wa mwanadamu na asili. ‘Kila mtu kivyake na ibilisi achukue ya nyuma kabisa’ ni msemo wa kishetani unaojulikana sana ambao umeingizwa ndani ya kila mtu na umekuwa maisha ya watu. Kuna maneno mengine ya falsafa ya kuishi ambayo pia ni kama haya. Shetani hutumia utamaduni mzuri wa kila taifa kuwaelimisha watu, akisababisha wanadamu kuanguka ndani na kumezwa na lindi kuu lisilo na mipaka la uharibifu, na mwishowe watu wanaangamizwa na Mungu kwa sababu wanamtumikia Shetani na kumpinga Mungu. … Bado kuna sumu nyingi za kishetani maishani mwa watu, katika mienendo yao na shughuli zao na wengine; hawana ukweli wowote hata kidogo. Kwa mfano, falsafa zao za kuishi, njia zao za kufanya vitu, na kanuni zao zote zimejazwa sumu za joka kuu jekundu, na zote zinatoka kwa Shetani. Hivyo, vitu vyote vinavyopita katika mifupa na damu ya watu ni vitu vyote vya Shetani(“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalinisaidia kuelewa kwamba kuwa mwasi na kutoridhika katika wajibu wangu kulikuwa kwa sababu nilikuwa nimetiwa kasumba na kupotoshwa na sumu za Shetani kama vile “Kila mtu kivyake na ibilisi achukue ya nyuma kabisa,” “Wenye ubongo hutawala wenye misuli,” na “Ni werevu zaidi au wapumbavu zaidi pekee ambao hawabadiliki kamwe,” na kwa sababu nilikuwa nikitafuta kujitokeza, kuwa bora kuliko wengine. Nilikumbuka nilipokuwa shuleni. Walimu na wazazi wangu waliniambia kila mara nitie bidii ili niweze kuingia katika chuo kikuu kizuri na kukwepa maisha ya mkulima, kwamba ingekuwa njia pekee ya kupata mbele. Hiyo ndiyo sababu nilisoma kwa bidii tangu nilipokuwa mchanga, nikitumai kwamba ningepata shahada nzuri na kupata kazi yenye heshima kama mwangalizi au msimamizi—kazi nzuri ambayo wengine wangeheshimu. Baada ya kuwa muumini, bado nilitathmini wajibu katika nyumba ya Mungu kwa macho ya mtu ambaye si muumini, nikiainisha wajibu katika kiwango cha juu au chini. Nilidhani kuwa kiongozi au kufanya kitu kilichotegemea ujuzi kulistahiki, na ndugu wangeheshimu wajibu kama huo, wakati ambapo wajibu mgumu usioonekana na watu ulikuwa duni na ungedharauliwa. Niliona kwamba sumu hizi za kishetani zilikuwa asili yangu, zikitawala mawazo yangu, zikinifanya nifuatilie sifa na hadhi kwa upumbavu, nikitaka kila wakati kuwa mtu wa kipekee. Jambo lilipotishia heshima na hadhi yangu, nilikuwa hasi na mpinzani. Sikuweza kabisa kukubali hali yangu na kufanya wajibu wangu kama kiumbe. Nilikosa dhamiri na mantiki kabisa. Nilijua kuwa iwapo ningeendelea kuishi kulingana na sumu hizi za kishetani, bila kutafuta ukweli, na bila kufanya wajibu wangu kama ambavyo Mungu anataka, mbali na kushindwa kupata ukweli na uzima, ningemchukiza Mungu na kuondolewa. Baada ya kugundua yote haya niliamua kuukana mwili wangu na kumridhisha Mungu. Sikutaka kuishi tena kulingana na sumu za Shetani. Nilikwenda kufanya kazi shambani tena siku iliyofuata.

Baadaye nilisoma maneno kadhaa kutoka kwa Mungu. “Ninaamua hatima ya kila mtu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anataka huruma, bali kulingana na ikiwa anao ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako). “Mwishowe, ikiwa watu wanaweza kupata wokovu au la halitegemei ni wajibu upi wanaotimiza, lakini linategemea ikiwa wameelewa na wamepata ukweli, na ikiwa wanaweza kutii mipango ya Mungu na kuwa kiumbe wa kweli aliyeumbwa. Mungu ni mwenye haki, na hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Yeye huwapima wanadamu wote. Kanuni hii haiwezi kubadilika, na lazima ukumbuke hili. Usifikirie kutafuta njia nyingine, au kufuatilia kitu kisicho halisi. Viwango ambavyo Mungu anahitaji kutoka kwa wote wanaopata wokovu hubadilika kila wakati; vinasalia vile vile bila kujali wewe ni nani(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Niliweza kuona tabia ya haki ya Mungu ndani ya maneno Yake. Mungu haamui matokeo na hatima ya mtu kwa msingi wa wajibu anaoufanya, kiasi cha kazi ambayo amefanya, au kiasi ambacho amechangia. Yeye huangalia iwapo mtu anaweza kutii sheria na mipango Yake na kufanya wajibu wa kiumbe, na ikiwa hatimaye ataweza kupata ukweli na kubadilisha tabia yake ya maisha. Bila kufuatilia ukweli katika imani yangu, basi bila kujali wajibu wangu ungeonekana kuwa mzuri au wa kuvutia kwa wengine jinsi gani, singeweza kamwe kupata ukweli, sembuse kupata kibali cha Mungu na wokovu Wake kamili. Hakika. Nilifikiria mpinga Kristo ambaye kanisa letu lilikuwa limemfukuza. Alikuwa ametekeleza wajibu kiasi muhimu na alikuwa amefanya kazi kama kiongozi, na washiriki wengine wapya wa kanisa walimheshimu sana. Lakini hakufuatilia ukweli au mabadiliko ya tabia katika wajibu wake, badala yake alishindania heshima na hadhi na akashikilia njia ya mpinga Kristo. Alifanya uovu wa kila aina na kuvuruga kazi ya nyumba ya Mungu. Hiyo ndiyo sababu mwishowe alifukuzwa. Niliona pia kwamba kulikuwa na ndugu wengine waliokuwa wakifanya wajibu wa kawaida, ambao haukuonekana kama wa kipekee, lakini walifanya tu wajibu wao kimyakimya bila malalamiko yoyote. Walipokabiliwa na matatizo, walitafuta ukweli na mapenzi ya Mungu. Walikuwa na nuru na mwongozo wa Roho Mtakatifu katika wajibu wao, nao walizidi kufanya vyema katika kazi yao. Walizidi kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu. Hii ilinionyesha kuwa katika imani, kupata ukweli hakuhusiani na wajibu wa mtu. Bila kujali ni wajibu gani anaoufanya mtu, kufuatilia ukweli na mabadiliko ya tabia ni muhimu. Hiyo ni kweli. Hiyo ndiyo njia ya pekee sahihi ya kuchukua. Sasa, kiongozi akiniagiza nifanye kazi kama msaidizi wa jukwaa au kibarua wa shamba, yote ni sheria na mipango ya Mungu, na ndiyo ninayohitaji katika kuingia kwangu maishani. Ninapaswa kuukubali na kuutii siku zote zote. Katika wajibu wangu, napaswa kutafuta ukweli, kutenda maneno ya Mungu, na kufuata kanuni za ukweli. Jambo hilo pekee ndilo linaambatana na mapenzi ya Mungu. Kugundua haya yote kulininiacha nikihisi huru. Kiongozi alinipa wajibu zaidi wa kawaida baadaye, ambao niliukubali kwa utulivu. Nilijitolea hata kuwasaidia ndugu katika kazi ya nyumbani katika wakati wangu wa ziada. Nilipotenda kwa njia hiyo niligundua kuwa iwapo nilikuwa nikisaidia katika kusafisha, kupanda miti, au kuchimba mtaro, kulikuwa na somo la kujifunza siku zote. Mungu hakunichukia kwa sababu nilikuwa nikifanya kazi ya kimwili. Mradi nilitia bidii, nilitafuta ukweli, na kutia maneno ya Mungu katika vitendo, niliweza kuvuna mavuno katika jambo lolote.

Baada ya kupitia haya niligundua kwa kweli kwamba bila kujali wajibu wangu, ni kile ambacho Mungu alikuwa amepanga, na ndicho nilichohitaji katika kuingia kwangu maishani. Ninapaswa kukubali kila wakati na kutii, kutekeleza wajibu wangu na majukumu yangu, na kutafuta ukweli na mabadiliko ya tabia katika mchakato huu wote. Hata ingawa nilikuwa daima nikiainisha wajibu katika madaraja tofauti, na nilikuwa nimepinga nilipokabiliwa na wajibu ambao sikuupenda, nikijawa na uasi na kumpinga Mungu, bado hakunitendea kulingana na makosa yangu. Badala yake, Alinielekeza hatua kwa hatua kwa maneno Yake, Akiniwezesha kuelewa ukweli na kujua majukumu na misheni ya kiumbe. Alibadilisha mitazamo yangu iliyopotoka ili niweze kushughulikia wajibu wangu ipasavyo na nianze kumtii. Huu ulikuwa upendo wa Mungu. Shukrani ziwe kwa Mungu!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kuzaliwa Upya

Yang Zheng Mkoa wa Heilongjiang Nilizaliwa katika familia maskini ya vijijini iliyokuwa nyuma kimaendeleo katika kufikiri kwao. Nilikuwa...

Kupima kwa Sura Ni Upuuzi Tu

Yifan Jiji la Shangqiu, Mkoa wa Henan Katika siku za nyuma, mimi mara nyingi niliwapima watu kwa sura zao, nikiwachukua watu wachangamfu,...

Maneno ya Mungu Yanaoongoza Njia

Na Xiaocheng, Shaanxi Maneno ya Mungu yanasema: “Kusudi la Mungu katika kuwafunua watu sio kuwaondoa, bali ni kuwafanya wakue” (“Ni kwa...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp