Kuna Njia ya Kumaliza Kiburi

13/01/2018

Xiaochen Jijini Zhengzhou, Mkoani Henan

Kiburi ni dosari yangu ya mauti. Nilikuwa mara kwa mara nikifichua tabia yangu ya kiburi, kila mara nikifikiri kuwa nilikuwa bora kuliko watu wengine. Hasa niliporekebisha ibara au kuwasiliana kuhusu kazi na mbia, kila mara nilikuwa mshupavu na sikusikiliza maoni mengine kwa ustaha. Kutoweza kwangu kushirikiana kwa upatano na wabia wangu mara nyingi kulisababisha matatizo kwa kazi. Ndugu walileta suala hili mara nyingi kwangu, na pia nilisoma mara kwa mara kuhusu Mungu akifichua asili ya watu yenye kiburi. Lakini kwa sababu sikuwa nimepata ufahamu wa kweli wa asili yangu na hali na pia singeweza kuuchukia kweli, wakati wowote nilipokutana na mazingira ya kufaa ningepoteza udhibiti. Baadaye, pia ningehisi kuchukizwa sana, lakini kwa sababu lile lilichofanyika limefanyika, yote niliyoweza kufanya ni kuzidi kujaribu kulielewa. Na hivyo lilifanyika tena na tena. Hilo lilinifanya nihisi aibu sana na nisiyejiweza.

Niliwahi kuona mara moja maneno yafuatayo ya Mungu wakati wa kutenda ibada ya kiroho: “Unatatua asili yako vipi? Kwanza, lazima uijue asili yako na lazima pia uelewe neno na mapenzi ya Mungu. Utahakikisha vipi basi, kwa kiwango kikubwa zaidi, kuwa utaepuka kutenda matendo mabaya, ukifanya tu yale ambayo yanalingana na ukweli? Kama uko tayari kufanya badiliko, basi lazima utafakari hili kwa uanglifu. Kwa kauli ya asili yako yenye dosari, aina gani za ufisadi inayoihusisha na namna gani za matendo inaweza kutenda, mtazamo upi basi unaweza kuchukuliwa na ni jinsi gani inaweza kuwekwa katika matendo ili kuidhibiti—hili ndilo swali muhimu. … Lin Zexu alikuwa mwepesi wa hasira. Kulingana na udhaifu wake mwenyewe aliandika chini wito ufuatao: ‘Idhibiti hasira yako.’ Huu ni mtazamo wa mwanadamu, hata hivyo unafanya kazi kwa kweli. Kila mtu ana kanuni zake za kufuata, kwa hivyo lazima pia wewe uweke kanuni kulingana na asili yako mwenyewe. Kanuni hizi ni muhimu, kuwa bila kanuni hizi hakukubaliki. Huu pia unafaa kuwa wito wako wa kumwamini Mungu na mfumo wako wa matendo(“Kutenda Ukweli na Kutatua Asili” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalinipa njia ya mara moja ningeweza kuchukua. Nilielewa: Ili kubadili tabia ya uasi, kwa upande mmoja unapaswa mara kwa mara kula na kunywa maneno kuhusu Mungu akifichua hali potovu ya mwanadamu, na kwa upande mwingine unastahili kusisitiza wito wa kudhibiti asili yako ili uweze kudhibiti kwa ufahamu ufunuo wa asili yako na hivyo ujitelekeze kutenda ukweli. Kwa hiyo, kwa mujibu wa vipengele vya upotovu wangu kama vile asili yangu ya kiburi, kujidai, na kutokuwa tayari kusikiliza maoni ya wabia, niliunda wito: “Ni jinsi gani kinyesi cha ng’ombe kinaweza kujivunia uvundo wake?” Wakati wowote nilipowasiliana kuhusu swali na wabia wangu, kwanza ningetumia wito huu kujionya, nikikumbuka imara kuwa asili yangu ni kinyesi cha ng’ombe na kwamba mwili wangu wote umepambwa na uvundo. Ningekumbuka pia jinsi nilivyokuwa nimesababisha matatizo mengi sana kwa kazi kwa sababu ya kiburi changu na ubinafsi, na kuwa hakuna haja ya kuwa na kiburi. Kwa njia hiyo, singedumisha kuwa kila mara nilikuwa sahihi kabisa, na pia lingenipa kipande kidogo cha moyo wa kutafuta, kunifanya niwe tayari kujinyenyekeza na kusikiliza maoni ya wengine. Wakati mwingine bado nilitaka kupinga maoni ya wengine, lakini mara tu nilipofikiria kuhusu wito, ningejitekeleza kwa ufahamu na kutenda ukweli wa uratibu patanifu.

Baada ya muda, niligundua kwa mshangao kuwa, niliponyenyekea, ningepata nuru fulani ya Roho Mtakatifu na mwanga kutoka kwa mawasiliano ya wabia wangu, na kuona baadhi ya vipengele vya upuuzi katika upokeaji wangu wa ukweli. Wakati uo huo, pia niligundua baadhi ya uwezo wa wengine, na nilikuwa tayari kuwategemea ili kunikamilisha. Pia sikufikiri kuwa nilikuwa bora zaidi kuliko watu wengine katika kila kitu na kushusha kichwa changu chenye kiburi pia. Kujitelekeza hakukuwa uchungu kama kulivyokuwa awali, na nilihisi kutoka moyoni kuwa kujinyenyekea na kusikiliza maoni ya wabia wangu bila majivuno yalikuwa mazuri sana, sio tu kunufaisha maendeleo ya maisha yangu bali pia kuboresha matokeo ya kazi yetu kupitia kufidia upungufu wa kila mmoja na kuja pamoja kama kitu kimoja.

Kwa njia ya uzoefu huu, nilionja utamu wa kutenda ukweli na kuona kuwa kuunda mwito kunaweza kunifanya kwa uangalifu kudhibiti ufunuo wa upotovu wangu, sio kupunguza tu makosa yangu bali pia kupata fursa zaidi ya kuelewa ukweli. Wakati uo huo, nilitambua pia kwamba ufunuo wa zamani wa asili yangu ya kiburi ulikuwa mbaya sana na wa kuchukiza. Asante Mungu kwa kuniongoza kujua mambo haya. Kuanzia sasa kuendelea, nitaunda miito ya kulingana na vipengele mbalimbali vya upotovu wangu na kujizuia mwenyewe ili niweze kutenda ukweli. Mimi pia mara kwa mara nitasoma neno la Mungu ili kujua kiini cha asili yangu mwenyewe ili nipate kujichukia mwenyewe na kujiondolea upotovu wangu haraka iwezekanavyo ili kumridhisha Mungu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kushikilia Wajibu Wangu

Na Yangmu, Korea ya Kusini Nilikuwa nikihisi wivu sana nilipowaona ndugu wakifanya maonyesho, wakiimba na kucheza kwa kumsifu Mungu....

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp