Baada ya Kubadilishwa na Mtu Mwingine
Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu hufanya kazi ndani ya kila mtu, na bila kujali mbinu Yake ni ipi, ni watu, vitu au masuala ya aina gani ambayo Yeye hutumia kufanya huduma, au maneno Yake yana sauti ya aina gani, Ana lengo moja tu la mwisho: kukuokoa. Kabla ya kukuokoa, Anahitaji kukubadili, hivyo utakosaje kuteseka kidogo? Ni lazima upate kuteseka. Kuteseka huku kunaweza kuhusisha mambo mengi. Wakati mwingine Mungu huwainua watu, mambo, na vitu ambavyo viko karibu nawe ili kwamba uweze kujitambua, vinginevyo unaweza kushughulikiwa moja kwa moja, kukupogolewa, na kufunuliwa. Kama vile tu mtu aliye juu ya meza ya upasuaji–lazima upitie maumivu kiasi kwa ajili ya matokeo mazuri” (“Ili Kupata Ukweli, Lazima Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo, na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Kutofaulu na kuanguka mara nyingi si jambo baya; na kufunuliwa pia si jambo baya. Iwe umeshughulikiwa, kupogolewa, au kufunuliwa, lazima ukumbuke hili wakati wote: Kufunuliwa hakumaanishi kuwa unashutumiwa. Kufunuliwa ni jambo zuri; ni fursa bora zaidi kwako kupata kujijua. Kunaweza kuuletea uzoefu wako wa maisha mabadiliko ya mwendo. Bila hilo, hutamiliki fursa, hali, wala muktadha wa kuweza kufikia ufahamu wa ukweli wa upotovu wako. Kama unaweza kujua vitu vilivyo ndani yako, vipengele hivyo vyote vilivyofichika ndani yako ambavyo ni vigumu kutambua na ni vigumu kufukua, basi hili ni jambo zuri. Kuweza kujijua mwenyewe kweli ndiyo fursa bora zaidi kwako kurekebisha njia zako na kuwa mtu mpya; ni fursa bora kwako kupata maisha mapya. Mara tu unapojijua mwenyewe kweli, utaweza kuona kwamba ukweli unapokuwa maisha ya mtu, ni jambo la thamani kweli, na utakuwa na kiu ya ukweli na kuingia katika uhalisi. Hili ni jambo zuri sana! Kama unaweza kunyakua fursa hii na ujitafakari mwenyewe kwa bidii na kupata ufahamu wa kweli kujihusu kila unaposhindwa au kuanguka, basi katikati ya uhasi na udhaifu, utaweza kusimama tena. Mara tu unapovuka kilele hiki, basi utaweza kuchukua hatua kubwa mbele na kuingia katika uhalisi wa ukweli” (“Ili Kupata Ukweli, Lazima Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo, na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kupitia maneno ya Mungu, ninaweza kuona kwamba bila kujali jinsi Mungu anavyofanya kazi ndani ya mtu, iwe ni kuhukumiwa na kusafishwa, kupogolewa na kushughulikiwa au kubadilishwa katika wajibu wake, yote hufanywa ili kumfanya ajitafakari na kujijua kusudi tabia yake iweze kubadilika.
Nilipokuwa muumini kwa miezi michache tu, nakumbuka kwamba ushirika uliotolewa na kiongozi mmoja, Dada Zhao, ulitia nuru sana na ulikuwa na uwezo wa kutatua matatizo ya kiutendaji. Nilivutiwa naye sana na niliwaza, “Itakuwa vyema sana nitakapofika wakati ambapo nitaweza kuwa kama Dada Zhao na kusuluhisha matatizo ya kina ndugu kupitia ushirika juu ya ukweli!” Kwa muda fulani, kila niliposikia kuhusu mtu akichaguliwa kama kiongozi au shemasi nilifadhaika sana na kutamani siku ambayo ningechaguliwa kama yeye. Baada ya hapo, nilianza kula, kunywa na kutafakari maneno ya Mungu kwa bidii na nikaandika shajara ya ibada. Nilishiriki katika kazi zote za kanisa kwa shauku.
Miaka michache baadaye, nilichaguliwa kama kiongozi wa kanisa. Mimi na Dada Liu tuliwajibikia kazi ya kanisa. Kila nilipoona matatizo katika kazi ya kanisa au kina ndugu walipopata matatizo katika wajibu wao, nilimtafuta Dada Liu ili kuyajadili na kutafuta ukweli wa kuyatatua. Baada ya miezi kadhaa, tulianza kupata matokeo halisi katika kazi ya kanisa, na kiongozi wangu aliniomba nishiriki kile nilichokuwa nikijifunza na kila mtu katika mikutano ya wafanyakazi. Nilifurahi sana nilipoona jinsi kiongozi huyo alivyonithamini na jinsi kina ndugu walivyonistahi. Kufumba na kufumbua, nilianza kujionyesha katika mikutano. Nilishiriki kila mara juu ya jinsi nilivyowanyunyizia na kuwasaidia kina ndugu, jinsi nilivyotatua matatizo, jinsi nilivyoteseka katika wajibu wangu, gharama niliyolipa na jinsi kazi ya kanisa ilivyofanikiwa, hatua kwa hatua. Hii iliwasababisha kina ndugu wengine wanistahi na wanipende, kwa hivyo walipokabiliwa na matatizo hawakulenga kuomba na kutafuta ukweli, lakini badala yake, walikuja kwangu moja kwa moja. Nilizidi kuhisi kwamba nilikuwa na sifa zilizostahili za kiongozi. Nilidhani kwamba mafanikio yaliyopatikana katika kazi ya kanisa hasa yalitokana na bidii yangu mwenyewe, kwa hivyo nilianza kumdharau Dada Liu kidogo na sikusikiliza mapendekezo yake. Mimi pekee ndiye niliyefanya uamuzi katika kazi ya kanisa. Nilipoona kwamba Dada Liu alihisi kwamba alizuiwa nami kidogo, sikutafakari juu yangu mwenyewe na hata nilijisifu katika mkutano: “Hata ingawa mimi na Dada Liu tunawajibikia kazi ya kanisa, amekuwa hasi na dhaifu katika wajibu wake, kwa hivyo lazima nihangaikie jambo hili na nilipe gharama. Ninamwonea Dada Liu wasiwasi sana. Mambo yakiendelea hivi, nahofia kwamba kazi ya kanisa itaathirika.” Kina ndugu walisema kwamba nilikuwa mwaminifu na niliubeba mzigo katika wajibu wangu. Nilifurahi sana niliposikia haya na nilifurahia kuungwa mkono na kupendwa nao.
Siku chache baadaye, dada mmoja aligundua tatizo langu lilikuwa lipi na akanionya, “Dada, nimegundua kwamba siku hizi hujakuwa ukifanya ushirika sana kuhusu uzoefu wako wa vitendo, kama vile wewe huonyesha upotovu au uasi wa aina gani unapokabiliwa na tatizo fulani, jinsi unavyojitafakari na kujijua au jinsi unavyotafuta ukweli ili kutatua mambo na jinsi unavyobadilika mwishowe. Sijawahi kusikia ukizungumza juu ya mambo hayo. Mara nyingi, wewe hushiriki juu ya jinsi unavyotatua matatizo ya watu wengine na jinsi unavyoteseka, jambo ambalo huwafanya wengine wakustahi na wakusifu mno. Huko kwenye njia inayofaa. Usipoteze wakati wowote—tafakari juu yako mwenyewe!” Lakini sikuweza kusikia yale aliyokuwa akisema hata kidogo. Niliwaza, “Ushirika wangu wote unahusu uzoefu wangu halisi wa binafsi. Kina ndugu wananipenda kwa sababu ninaweza kutatua matatizo kwa kutumia ukweli. Unawezaje kusema kwamba wengine wananisifu sana na kwamba siko kwenye njia sahihi? Ulisema hivyo kwa sababu tu unanionea wivu, siyo?” Wakati huo, nilikuwa nimetawaliwa na sifa na hadhi na moyo wangu ulikuwa mgumu na uliokufa ganzi. Baada ya muda, nilizidi kuhisi giza ndani yangu na sikuweza tena kuelewa au kutatua hali za wengine au matatizo katika wajibu wao. Niliishia kuachishwa wajibu wangu kama kiongozi kwa sababu sikuweza kufanya kazi ya vitendo.
Baada ya hapo, nilihisi kwamba sikuwa na nguvu hata kidogo na sikutaka kuukabili ukweli. Nilianza kuwa hasi sana kiasi kwamba sikutaka hata kuhudhuria mikutano. Nilihisi aibu sana kiasi kwamba sikutaka kuwakabili kina ndugu. Hapo awali, mimi ndimi niliyekuwa nikiongoza mikutano na kutoa ushirika kwa wengine, lakini sasa mimi ndimi niliyekuwa nikiupokea. Nilionea wasiwasi jinsi ambavyo wengine wangeniona. Kadiri nilivyozidi kufikiria hayo, ndivyo nilivyozidi kufadhaika. Sikuweza kuwa makini kwenye mikutano na wakati mwingine hata nilisinzia. Nilikuwa dhaifu na hasi sana na nilihisi kwamba nilikuwa nimeachwa na Mungu. Sikuweza kujizuia kulia na nikampigia Mungu magoti na kumwomba: “Ee Mungu! Nateseka sana. Sitaki kuishi katika hali ya aina hii. Mungu, naomba mwongozo na wokovu Wako. Niko tayari kutafakari juu yangu mwenyewe na kujijua kwa dhati.”
Nilitazama video ya usomaji wa maneno ya Mungu baada ya kuomba. Mwenyezi Mungu anasema, “Katika kutafuta kwenu, mna dhana, matumaini, na siku za baadaye nyingi sana za kibinafsi. Kazi ya sasa ni ili kushughulikia tamaa yenu ya hadhi na tamaa zenu badhirifu. Matumaini, hadhi, na dhana yote ni mifano bora kabisa ya tabia ya kishetani. … Sasa nyinyi ni wafuasi, na mmepata ufahamu fulani wa hatua hii ya kazi. Hata hivyo, bado hamjaweka kando tamaa yenu ya hadhi. Wakati hadhi yenu iko juu mnatafuta vizuri, lakini wakati hadhi yenu iko chini hamtafuti tena. Baraka za hadhi daima ziko katika fikira zenu. Kwa nini watu wengi hawawezi kujiondoa katika uhasi? Je, si jibu bila shaka ni kwa sababu ya matarajio ya kuvunja moyo? … Kadiri unavyotafuta zaidi kwa njia hii, ndivyo utakavyovuna kidogo zaidi. Kadiri ilivyo kubwa zaidi tamaa ya mtu ya hadhi, ndivyo itabidi washughulikiwe kwa uzito zaidi na ndivyo watakavyozalimika kupitia usafishaji mkubwa. Watu kama hao hawana thamani kabisa! Lazima wshughulikiwe na wahukumiwe vya kutosha ili waachane na mambo haya kabisa. Mkifuatilia kwa njia hii mpaka mwisho, hamtavuna chochote. Wale ambao hawafuatilii uzima hawawezi kubadilishwa, na wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na uingiaji, lakini badala yake unalenga tamaa badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kumkaribia Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme?” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mbona Huna Hiari ya Kuwa Foili?).
Maneno ya Mungu yalifichua kabisa nia na mawazo yangu kuhusu kufuatilia hadhi katika imani yangu. Nilikumbuka nilipoanza kuwa muumini. Niliwapenda sana viongozi na nilitamani sana siku ambayo ningekuwa kiongozi na kuheshimiwa. Nilipokuwa kiongozi, nilifanya wajibu wangu kuanzia alfajiri hadi jioni na nilifurahia kuufanya bila kujali ulichosha vipi. Nilipohisi kwamba nilithaminiwa na kiongozi na kuheshimiwa na kina ndugu, nilizidi kutiwa hamasa. Katika mikutano, nilijionyesha kila wakati, nikionyesha jinsi nilivyokurupuka huku na kule nikifanya kazi, jinsi nilivyoteseka na hata nilimshushia hadhi Dada Liu na nikajiinua ili watu wanisifu mno. Baada ya Kubadilishwa kama kiongozi na sikuwa na hadhi yoyote, niliingia katika hali ya uhasi ambayo sikuweza kuondokana nayo. Nilipokabiliwa na ukweli, niliona kwamba sikuwa nikifuatilia ukweli au kufanya wajibu wangu katika imani yangu, bali nilikuwa nikifuatilia hadhi. Nilipokuwa na hadhi, nilikuwa na motisha, lakini bila hadhi, nilirudi katika hali hasi. Hata niliamua kwamba sikuwa na matumaini. Niliona jinsi tamaa yangu ya hadhi ilivyokuwa mbaya. Ufuatiliaji wa aina hiyo ungewezaje kunisababisha nipate ukweli na wokovu wa Mungu? Nilikuwa nikifikiri kwamba nilikuwa hodari sana na kwamba nilielewa ukweli kiasi na nilistahili kuwa kiongozi. Sikuwahi kufikiri kwamba ningekuwa hasi sana baada ya kubadilishwa na mtu mwingine. Wakati huo ndipo nilipoona kwamba sikuwa na uhalisi wa ukweli au kimo chochote. Niliwanenea watu maneno na mafundisho matupu tu. Sikujijua kabisa—sikujitambua hata kidogo. Nisingeachishwa wajibu wangu, nisingetafakari juu yangu wala kujijua, bali ningekuwa nikifuatilia hadhi, bado nikiwa kwenye njia ya kumpinga Mungu. Hiyo ingezuia tu kazi ya nyumba ya Mungu na kudhuru kuingia uzimani kwa ndugu zangu. Hatimaye niligundua kwamba kubadilishwa kama kiongozi kulikuwa hukumu ya Mungu yenye haki na ulinzi wa Mungu. Mungu alikuwa akiishughulikia tamaa yangu ya hadhi na kunifanya nione kwamba nilikuwa kwenye njia isiyofaa ili niweze kutubu Kwake. Nilihisi huru nilipotambua haya.
Baada ya hapo, nilisoma maneno mengine zaidi ya Mungu yaliyofunua ufuatiliaji wa watu wa sifa na hadhi na nakumbuka vifungu kadhaa. “Watu wengine hususan humpenda Paulo sana. Wanapenda kwenda na kuhutubu na kufanya kazi, wanapenda kukutana pamoja na kuzungumza; wanapenda watu kuwasikiza, kuwaabudu, na kuwazingira. Wanapenda kuwa na hadhi katika mawazo ya wengine, na wanafurahia wakati wengine wanathamini mifano yao. Hebu tuchanganue asili yao kutoka kwa tabia hizi: Je, asili yao ni ipi? Kama kweli wanatenda kwa njia hii, basi hilo linatosha kuonyesha kuwa wao ni fidhuli na wenye majivuno. Hawamwabudu Mungu hata kidogo; wanatafuta hadhi ya juu zaidi, na wangependa kuwa na mamlaka juu ya wengine, kuwamiliki, na kuwa na hadhi akilini mwao. Huu ni mfano bora wa Shetani Vipengele vya asili yao vinavyojitokeza ni ufidhuli na majivuno, kutokuwa radhi kumwabudu Mungu, na tamaa ya kuabudiwa na wengine. Tabia kama hizi zinaweza kupa mtazamo dhahiri sana juu ya asili yao.” “Wengine wakiweza kutumia vyeo vyao kushuhudia mara kwa mara kuhusu wao wenyewe, kujiongezea zaidi umaarufu wao, na kushindana na Mungu kwa ajili ya watu na hadhi. Wanatumia mbinu na njia mbalimbali kuwafanya watu kuwaabudu, kujaribu mara kwa mara kuwa na ufuasi mkubwa wa watu na kutaka kuwadhibiti watu hao. Baadhi hata hupotosha kimakusudi watu na kuwafanya kufikiria kwamba wao ni Mungu ili waweze kuchukuliwa kama Mungu. Hawawezi katu kuwaambia watu kwamba wamepotoshwa, kwamba pia wao wamepotoka na wana kiburi, na hivyo basi hawafai kuwaabudu, na kwamba haijalishi watafanya vyema kiasi kipi, haya yote ni kutokana na utukuzaji wa Mungu na kile wanachostahili kufanya kwa kweli. Kwa nini hawasemi mambo haya? Kwa sababu wana hofu kuu ya kupoteza nafasi yao ndani ya mioyo ya watu. Hii ndiyo maana watu kama hao hawamtukuzi Mungu katu na katu hawamshuhudii Mungu” (Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I).
Maneno ya Mungu yalinifichulia kwamba watu hufuatilia sifa na hadhi daima na hawamtukuzi au kumshudia Mungu. Badala yake, wao hujionyesha kila wakati na huwafanya wengine wawasifu mno na kuwazingira kwa sababu ya tabia zao za kishetani na hili hulaaniwa na kuadhibiwa na Mungu. Je, Paulo hakuwa mfano mzuri wa hayo? Alipenda kuwa na hadhi na mamlaka na alizingatia sana cheo chake na ufahari wake. Katika nyaraka zake, alitoa ushuhuda mara nyingi wa kazi alizokuwa amefanya, jinsi alivyoteseka kwa ajili ya Bwana na akasema kwamba alikuwa mkuu kuliko mitume wengine. Bidii yake na gharama aliyolipa hayakuwa ya kufuatilia ukweli au kufanya wajibu wa kiumbe, bali yalikuwa ya kukidhi malengo yake ya kupita kiasi, kupendwa na wengine na mwishowe kutuzwa na kuvikwa taji. Hii ndiyo sababu tabia yake ya maisha haikubadilika hata kidogo baada ya kufanya kazi kwa bidii kwa miaka mingi, na mwishowe alipoteza mantiki yake kwa sababu ya kiburi chake, akishuhudia kwamba kwake, kuishi alikuwa Kristo. Alikuwa na ndoto ya mchana ya kuchukua nafasi ya Bwana Yesu ili watu wamfuate na kumwiga. Aliikosea sana tabia ya Mungu. Paulo alikuwa na asili ya kishetani ambayo ilikuwa yenye kiburi na majivuno sana. Kila kitu alichofanya kilikuwa cha kutosheleza malengo yake za kupita kiasi na yote yalimchukiza Mungu. Alikuwa kwenye njia ya mpinga Kristo ya kumpinga Mungu, jambo ambalo lilishutumiwa na kulaaniwa na Mungu. Kwa mintarafu yangu, nilipopata mafanikio machache katika wajibu wangu, nilisema kwamba nilimshukuru Mungu kwa mwongozo Wake, lakini moyoni mwangu, nilijisifu. Nilikuwa nikiiba utukufu wa Mungu bila haya na kujionyesha mara kwa mara, nikijigamba juu ya jinsi nilivyokurupuka huku na kule na kuteseka, na matatizo niliyokuwa nimetatua ili wengine wanisifu mno. Nilipoona kwamba Dada Liu alianza kuwa hasi na dhaifu, nilimsaidia na kumuunga mkono kijuujuu, lakini moyoni mwangu, nilimhukumu na kumdharau. Hata nilimshushia hadhi katika mikutano huku nikijiinua, nikiwataka kina ndugu wanistahi na wanisikilize. Dada mmoja aliona tatizo langu na akanionya kutokana na upendo, lakini nilikataa kwa ukaidi kukubali hayo. Hata nilidhani kwamba alikuwa akinidunisha na alinionea wivu. Niliona jinsi nilivyokosa mantiki kabisa. Katika wajibu wangu, sikuzingatia kufanya ushirika juu ya ukweli ili kumtukuza na kumshuhudia Mungu, lakini badala yake, nilijionyesha na kulinda hadhi yangu mara kwa mara ili niheshimiwe. Niliona jinsi nilivyokuwa mwenye kiburi na majivuno kiasili. Nilikuwa nikiishi kwa kudhihirisha kabisa asili ya kishetani na nilikuwa nikitembea kwenye njia ya mpinga Kristo ya kumpinga Mungu ambayo Paulo aliitembea. Nilijua kwamba nisingetubu, ningehukumiwa na kuondolewa na Mungu. Wazo hili lilinitia hofu. Nilikuja mbele za Mungu upesi kumwomba, nikiwa tayari kufuatilia ukweli na kutubu kwa Mungu. Baada ya hapo, nilikula na kunywa maneno ya Mungu zaidi na nikatafakari juu yangu mwenyewe na kujijua. Nilichunguza nia na dhamira za matendo yangu. Nilipokabiliwa na matatizo, nililenga kutenda maneno ya Mungu na hali yangu ikawa bora pole pole.
Mwezi mmoja baadaye, kiongozi mmoja alinipangia wajibu wa mapokezi na sikufurahia sana jambo hili mwanzoni. Nilipokuwa kiongozi, watu wengine walinipokea, lakini sasa nilikuwa niwapokee wengine. Ilikuwa tofauti sana! Lakini baadaye nikawaza, “Je, bado sifuatilii sifa na hadhi? Kuwapokea kina ndugu kunaweza kuonekana kama si kitu cha pekee, lakini huo ni wajibu wangu na ni jukumu langu. Sipaswi kuwa na chaguo au madai yangu mwenyewe, bali napaswa kutii sheria na mipango ya Mungu.” Na kwa hivyo, nilikubali. Siku mbili baadaye, kiongozi aliwaleta kina dada kadhaa nyumbani kwangu. Nilitambua mara moja kwamba nilikuwa nimefanya wajibu wangu na kina dada hawa wawili hapo awali. Nilishikwa na aibu mara moja na nilifedheheka sana, kana kwamba nilikuwa kwenye tabaka la chini zaidi kuwaliko. Tulitaniana kisha nikaingia jikoni kuandaa chakula. Nilipokuwa nikipika, nilikumbuka wakati ambapo nilikuwa nikifanya wajibu wangu pamoja na kina dada hao. Nilikuwa nikiongoza mikutano na kuwapa ushirika. Sikuwahi kudhani kwamba wangekuwa viongozi sasa wakati ambapo nilikuwa nyumbani nikifanya wajibu wa mapokezi. Nilifadhaika sana. Kisha nikagundua kwamba nilikuwa nikilenga sifa na hadhi tena, kwa hivyo nilikimbia kumwomba na kumwita Mungu kisha nikakumbuka kifungu hiki cha maneno Yake: “Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda kwa wajibu kile ambacho ameaminiwa na Muumba. Naye binadamu lazima asitende mambo nje ya mipaka yake au kufanya mambo zaidi ya uwezo wake au kufanya mambo ambayo ni ya kuchukiza Mungu. Binadamu ni lazima asijaribu kuwa mkubwa, au wa kipekee, au zaidi ya wengine, wala asitafute kuwa Mungu. Hivi ndivyo watu hawafai kutamani kuwa. Kutamani kuwa mkubwa au wa kipekee ni jambo la upuuzi. Kutafuta kuwa Mungu ndilo hata jambo la aibu zaidi; linaudhi na linastahili kudharauliwa. Kile cha kupongezwa, na ambacho viumbe vinastahili kushikilia kuliko chochote kile ni kuwa viumbe vya kweli; hii ndiyo shabaha pekee ambayo watu wote wanafaa kufuatilia” (Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I). Nilipokuwa nikitafakari maneno ya Mungu, nilielewa kwamba Mungu hataki watu wa hali ya juu na mashuhuri, bali Anataka viumbe wa kweli. Iwapo una hadhi au la, kuweza kutii sheria na mipango ya Mungu, kuwa mtu mwaminifu na kuendelea kutekeleza wajibu wako ndiko tu hukidhi mapenzi ya Mungu. Mungu aliamua kabla niwe unyasi mdogo na sikuwa na budi kunyenyekea bila kutafuta kuwa mti mkubwa, kufanya kazi yangu vizuri kama unyasi mdogo na kufanya wajibu wangu vizuri. Nilikumbuka nilipokuwa kiongozi. Ilionekana kama kulikuwa na utukufu ndani ya jambo hilo, lakini sikuwa nimelenga kufuatilia ukweli. Badala yake, nilifuatilia sifa na hadhi kila wakati. Niliridhika mno, nilijidai, nikazidi kuwa mwenye kiburi na kuishi kwa kudhihirisha tabia ya kishetani na kumchukiza Mungu. Sasa nilikuwa nikifanya wajibu wa mapokezi, ambao haukuonekana wa maana sana, lakini kuweza kutekeleza jukumu na wajibu wangu kulinifanya niwe na amani na utulivu sana. Nilipofiria hayo kwa kina, sikuhisi tena kwamba kuwa mwenyeji kuliniweka kwenye tabaka la chini zaidi. Niliweza kutii kwa dhati.
Baada ya kula chakula cha mchana, sote watatu tulifanya mkutano. Nilizungumza katika ushirika juu ya yale niliyojifunza katika wajibu wangu wakati huo na walishiriki juu ya uzoefu wao wenyewe pia. Jambo hilo lilinikomboa sana na sikuhisi tena kwamba nilifungwa na sifa na hadhi. Huo ndio ulikuwa uzoefu wangu wa kuwa kiongozi na kisha kubadilishwa na mtu mwingine. Shukrani kwa Mungu!
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?