Maneno ya Mungu Yameniamsha

14/01/2018

Miao Xiao Mji wa Jinan, Mkoa wa Shandong

Katika siku zilizopita, nilikuwa daima nikifikiri kuwa Mungu aliposema “kibaraka na msaliti anayekikimbia kiti kikuu cheupe cha enzi” Alikuwa anaashiria wale wanaoikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho lakini ambao baadaye wanarudi nyuma. Kwa hivyo, wakati wowote nilipoona ndugu wakijiondoa katika njia hii kwa sababu yoyote ile, moyo wangu ungejawa na dharau kwao. Huyo, kibaraka na msaliti mwingine anatoroka kutoka kwa kiti kikuu cheupe cha enzi ambaye atapokea adhabu ya Mungu. Wakati uo huo, nilijihisi nikiwa nikitenda ifaavyo kwa kukubali hukumu ya Mungu na nilikuwa siko mbali na kukubali ukombozi wake Mungu.

Siku moja, nilipokuwa nikitenda ibada ya kiroho, niliona maneno yafuatayo ya Mungu kwenye maandiko “Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli”: “Kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu. Usipouchukulia ukweli huu kuwa muhimu na kila mara kufikiria kuuepuka au kutafuta njia nyingine isipokuwa ukweli, basi Ninasema kuwa wewe ni mtenda dhambi mkubwa. Iwapo una imani kwa Mungu, lakini hutafuti ukweli au mapenzi ya Mungu, wala hupendi njia inayokuleta karibu na Mungu, basi Nakwambia kuwa wewe ni yule anayejaribu kuepuka hukumu, na kwamba wewe ni kibaraka na msaliti anayekikimbia kiti kikuu cheupe cha enzi. Mungu hatawasamehe waasi wowote wanaotoroka machoni Pake. Wanadamu wa aina hii watapokea adhabu kali zaidi. Wale wanaokuja mbele za Mungu ili wahukumiwe, na zaidi ya hayo wametakaswa, wataishi milele katika ufalme wa Mungu(Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kutafakari maneno haya, hatimaye nilielewa kwamba: Inatukia kwamba vibaraka na wasaliti wanaotoroka kutoka kiti kikuu cheupe cha enzi hayazungumzii wale wanaorudi nyuma katika njia hii tu. La maana zaidi, ni kwamba yanarejelea wale wanaomfuata Mungu lakini hawaudhamini ukweli huu, watu ambao daima wanaukwepa ukweli huu, wanaotafuta njia mpya kando na njia ya kweli, na wasio tayari kujikabidhi kwa kuadibu na hukumu ya Mungu na kutafuta kutakaswa na Mungu. Chini ya nuru na mwongozo wa Mungu, nilianza kutafakari juu ya tabia yangu mwenyewe: Sasa Mungu anaonyesha maneno Yake kumhukumu mwanadamu, na kutakasa vitu kutoka kwa mwanadamu visivyolingana na Yeye kupitia mateso na usafishaji. Lakini nikikabiliwa na kuadibu na hukumu, mateso na usafishaji wa Mungu, mimi kila mara hujaribu kutoroka, nikitumaini kwamba Mungu ataondoa hali hizi upesi. Je, huku sio kuepuka ukweli na kutafuta njia ya kuuhepa ukweli? Wakati watu au maswala yanayoletewa na Mungu hayaambatani na dhana zangu binafsi, ama ninapojipata katika hali mbaya, hata kama mawasiliano ya ndugu zangu yanaweza kutatua matatizo yangu, na kutatua kutoelewa kwangu kumhusu Mungu, mimi bado hupinga na kukataa kusikiliza. Je, hivi sivyo, Mungu asemavyo, kutotafuta ukweli na kutopenda njia inayonileta karibu na Mungu? Ninaposhughulikiwa na kupogolewa kwa sababu ya njia ya uzembe ambayo mimi hufanya kazi yangu, mimi kila mara huwa natafuta visingizio ili kujieleza. Je, hiki sio kiini kinachokataa kuukubali ukweli? Mara nyingi mimi hujikubali katika maisha halisi. Hata wakati najua kwamba ni ukweli, mimi hukataa kuusaliti mwili wangu ili nitende ukweli. Je, huku sio kutokubali hukumu tu, bali pia ni kutotafuta kutakaswa? … Sasa kwa kuwa natafakari kuhusu hili, nalielewa hata kwa wazi zaidi: Wale ambao Mungu husema hukimbia kutoka kwa kiti kikuu cheupe cha enzi haiashirii waliotoka kanisani tu. La muhimu hata zaidi, inarejelea mioyo yetu kukataa kukubali ukweli na kutokubali kujikabidhi kwa hukumu ya Mungu. Ni sasa tu ambapo ninaanza kuhisi wasiwasi na hofu. Japo sijaliwacha kanisa, wakati wowote nilipokabiliwa na shida daima nilikataa kukubali ukweli na kuepuka hukumu ya Mungu. Je, mimi siye hasa yule kibaraka na msaliti anayekikimbia kiti cha hukumu ya Mungu? Ilhali nilikuwa nimesadiki kwamba wale wanaoiacha kanisa pekee ndio vibaraka na wasaliti wanaokikimbia kiti cha enzi cha Mungu, huku nilikuwa karibu sana kupokea wokovu wa Mungu. Ninaona kwamba kuelewa kwangu kwa neno la Mungu kuliegemea upande mmoja sana na ulikuwa wenye kina kifupi, na kwamba ufahamu wangu wa kazi ya Mungu ulikuwa umepungukiwa sana. Sasa, wale wanaokubali kwa dhati kuadibu na hukumu ya Mungu na wale ambao tabia zao zimefikia mabadiliko pekee ndio watakaopokea wokovu wa Mungu. Badala yake, nilikuwa ninaishi katika fikira zangu mwenyewe, bila kuwa na njaa ya ukweli, bila kuyawajibikia maisha yangu mwenyewe na kutokuwa na hisia ya hatari au haraka hata kidogo. Nikiendelea hivi, je, sitakuwa hasa kiumbe wa adhabu ya Mungu hasa.

Kwa sababu ya kutoa nuru kwa maneno ya Mungu, nimeamka kutoka kwa dhana na mawazo yangu, nikigundua kwamba mimi si mtu ambaye yuko tayari kukubali kuadibu na hukumu ya Mungu. Kumenifanya pia nione ya kwamba niko katika ukingo wa hatari. Kutoka sasa kuendelea, nitaupa moyo wangu wote kwa Mungu, nijikabidhi kwa kuadibu na hukumu Yake, na nifanye kila niwezalo kuutafuta ukweli na mabadiliko katika tabia, ili hivi karibuni niweze kutakaswa na nifanywe mkamilifu na Mungu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kurudi kwenye Njia Sahihi

Chen Guang, Marekani Mwenyezi Mungu anasema, “Kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp