600 Kufanikiwa ama Kushindwa Kunategemea Njia Atembeayo Mwanadamu

1 Ukweli unatoka katika ulimwengu wa mwanadamu, na bado ukweli katika mwanadamu unapitishwa na Kristo. Unaanzia kwa Kristo, yaani, kutoka kwa Mungu mwenyewe, na hiki si kitu ambacho mwanadamu anaweza kufanya. Ilhali Kristo hutoa ukweli tu; Yeye haji kuamua ikiwa mwanadamu atafanikiwa katika harakati yake ya kufuata ukweli. Hivyo, kinachofuata ni kuwa mafanikio au kushindwa kwa kweli yote yanategemea harakati ya mwanadamu. Mafanikio au kushindwa kwa mwanadamu kwa kweli kamwe hakuna uhusiano na Kristo, lakini kwa mbadala kunategemea harakati yake. Ikiwa njia unayopitia katika kutafuta ni ya kweli, basi una matumaini ya mafanikio. Kama njia unayopitia katika kufuatilia ukweli ni mbaya, basi wewe milele hutaweza kufanikiwa. Iwapo utafanywa mkamilifu ama utatolewa katika mashindano inategemea na harakati yako mwenyewe, ambayo pia ni kusema kuwa mafanikio au kushindwa kunategemea njia ambayo mwanadamu anapitia.

2 Wale ambao wanatafuta kumpenda Mungu hawapaswi kutafuta faida zozote za kibinafsi au lile ambalo wanatamani binafsi; hii ndiyo njia sahihi kabisa ya ufuatiliaji. Kama kile ambacho unatafuta ni ukweli, kile ambacho unatenda ni ukweli, na kile ambacho unafikia ni badiliko katika tabia yako, basi njia unayopitia ni sahihi. Iwapo utafutacho ni baraka za mwili, na kile unachoweka katika vitendo ni ukweli wa dhana zako mwenyewe, na iwapo hakuna mabadiliko katika tabia yako, na wewe si mtiifu kabisa kwa Mungu katika mwili, na bado unaishi kwenye mashaka, basi unachotafuta bila shaka kitakupeleka kuzimu, kwa kuwa njia ambayo unatembea ni njia ya kushindwa. Iwapo utafanywa mkamilifu ama utatolewa katika mashindano inategemea na harakati yako mwenyewe, ambayo pia ni kusema kuwa mafanikio au kushindwa kunategemea njia ambayo mwanadamu anapitia.

Umetoholewa kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 599 Kuishi kwa ajili ya Kutimiza Wajibu Wako Kuna Maana

Inayofuata: 601 Njia za Petro na Paulo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp