794 Wale Wanaojua Amri ya Mungu Watatii Utawala Wake

1 Mtu aliyepata maarifa ya ukuu wa Muumba baada ya kupitia miongo kadhaa ya maisha, ni mtu aliye na shukrani sahihi ya maana na thamani ya maisha; mtu aliye na kina cha maarifa kuhusu kusudi la maisha, aliye na hali halisi aliyopitia na anaelewa ukuu wa Muumba; na hata zaidi, mtu anayeweza kunyenyekea mbele ya mamlaka ya Muumba. Mtu kama huyo anaelewa maana ya uumbaji wa Mungu wa mwanadamu, anaelewa kwamba binadamu anafaa kumwabudu Muumba, kwamba kila kitu anachomiliki binadamu kinatoka kwa Muumba na kitarudi kwake siku fulani isiyo mbali sana kwenye siku za usoni.

2 Mtu kama huyo anaelewa kwamba Muumba hupangilia kuzaliwa kwa binadamu na ana ukuu juu ya kifo cha binadamu, na kwamba maisha na kifo vyote vimeamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba. Kwa hiyo, wakati mtu anapong’amua mambo haya, mtu ataanza kuweza kukabiliana na kifo kwa utulivu na kwa kawaida, kuweka pembeni mali yake yote ya dunia kwa utulivu, kukubali na kunyenyekea kwa furaha kwa yote yatakayofuata, na kukaribisha awamu ya mwisho ya maisha iliyopangiliwa na Muumba badala ya kutishika vivyo hivyo tu na kung’ang’ana dhidi ya kifo.

3 Ikiwa mtu anayaona maisha kama fursa ya kupitia ukuu wa Muumba na kujua mamlaka yake, ikiwa mtu anayaona maisha yake kama fursa nadra ya kutekeleza wajibu wake akiwa binadamu aliyeumbwa na kutimiza kazi yake maalum, basi mtu atakuwa ana mtazamo sahihi wa maisha, ataishi maisha yaliyobarikiwa na yanayoongozwa na Muumba, atatembea kwenye nuru ya Muumba, atajua ukuu wa Muumba, atakuwa katika utawala Wake, atakuwa shahidi wa matendo Yake ya kimiujiza na mamlaka Yake.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 793 Dhana na Fikira Hazitawahi Kukusaidia Kumjua Mungu

Inayofuata: 795 Uhuru Hupatwa kwa Kujua Amri ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp