815 Unapaswa Kuyaelewa Mapenzi ya Mungu

1 Kile ambacho umerithi wakati huu, kimepiku walichorithi mitume na manabii na ni kikuu zaidi kuliko alichopokea Musa na Petro. Baraka haziwezi zikapokewa kwa siku moja au mbili; sharti zipatikane kwa kujitolea kwingi. Yaani, lazima uwe na upendo uliosafishwa, imani kuu, na ukweli mwingi ambao Mungu Anakuagiza uufikie; zaidi ya hayo, sharti uelekeze uso wako kwa haki wala usikubali kushindwa, na lazima uwe na upendo usiofikia kikomo kwa ajili ya Mungu. Azimio linahitajika kutoka kwako, na vilevile mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Upotovu wako lazima utibiwe, na lazima ukubali mipango ya Mungu pasipo kulalamika, na hata uwe mtiifu hadi kifo. Hicho ndicho unachopaswa kutimiza. Hili ndilo lengo la mwisho la kazi ya Mungu, na matakwa ya Mungu kwa watu wa kundi hili.

2 Anapokukarimia mengi, anakutaka wewe badala yake na kukufanyia matakwa yanayokufaa. Na kutokana na hili inaonekana ni kwa nini Mungu kila mara hufanya kazi ya hali ya juu na yenye mahitaji makali. Ndiyo maana unafaa kujawa na imani katika Mungu. Kwa ufupi, kazi yote ya Mungu hufanywa kwa ajili yako, ili kwamba uweze kupokea urithi Wake. Hii sio kwa ajili ya utukufu wa Mungu bali ni kwa ajili ya wokovu wako na kufanya kundi hili la watu walioteswa na nchi najisi kuwa wakamilifu. Sharti uelewe mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo Nawahimiza wale wote wasiojua, wasio na hisia na ufahamu: Usimjaribu Mungu wala kumpinga tena.

3 Mungu Ameshavumilia mateso yote ambayo mwanadamu hajaweza kupitia, na hapo awali Ameteseka na kudhihakiwa kwa niaba ya mwanadamu. Je, nini kingine ambacho huwezi kukiachilia? Je, ni nini muhimu zaidi kuliko mapenzi ya Mungu? Ni nini zaidi kuliko upendo wa Mungu? Ni kazi ambayo ina ugumu mara mbili zaidi kwa Mungu kufanya katika nchi najisi. Ikiwa mtu atatenda dhambi kimakusudi na akifahamu, kazi ya Mungu itaendelezwa kwa muda mrefu zaidi. Mungu Hafungwi na wakati; kazi Yake na utukufu Wake huchukua mstari wa mbele. Kwa hiyo, hata ikichukua muda mrefu, Hataacha kutoa dhabihu yoyote ikiwa ni kazi Yake. Hii ndiyo silika ya Mungu: Hatapumzika hadi pale kazi Yake itakapokamilika.

Umetoholewa kutoka katika “Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 814 Una Ufahamu Kuhusu Misheni Yako?

Inayofuata: 816 Kutoa Ushahidi kwa Mungu Ni Wajibu wa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp