51 Binadamu na Mungu Washiriki katika Furaha Kamili ya Muungano

1 Nimeanza kazi Yangu kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wa ulimwenguni; watu wa ulimwengu huamka ghafla, na kutembea wakizunguka kiini, ambayo ni kazi Yangu, na “Ninaposafiri” ndani yao, wote huepuka utumwa wa Shetani, na hawateswi katikati ya mateso ya Shetani. Kwa sababu ya majilio ya siku Yangu, watu hujaa furaha, huzuni ndani ya mioyo yao hutoweka, mawingu ya huzuni angani hugeuka kuwa oksijeni katika hewa na kuelea hapo, na wakati huu, Nafurahia furaha ya umoja na mwanadamu.

2 Vitendo vya mwanadamu hunipa kitu cha kufurahia, na hivyo Sisikitishwi tena. Na, kuandamana na majilio ya siku Yangu, vitu vya dunia amabavyo vina nguvu, vitu vyote duniani huwa hai tena, na vinanikubali Mimi kama asili ya kuwepo kwao, kwa sababu Mimi Husababisha vitu vyote kuangaza na uzima, na hivyo, pia, Navisababisha kutoweka kimyakimya. Hivyo, vitu vyote husubiri amri kutoka kwa kinywa Changu, na hupendezwa na yale ambayo Ninafanya na kusema.

3 Kati ya vitu vyote, Mimi ni Aliye Juu Zaidi—lakini Mimi pia Naishi miongoni mwa watu wote, na kutumia matendo ya watu kama maonyesho ya uumbaji Wangu wa mbingu na dunia. Wakati watu wanatoa sifa kubwa mbele Yangu, Mimi Husifiwa miongoni mwa vitu vyote, na hivyo maua duniani huwa mazuri zaidi chini ya jua kali, nyasi hustawi zaidi, na mawingu angani huonekana samawati zaidi.

4 Kwa sababu ya sauti Yangu, watu hukimbia huku na kule; leo nyuso za watu katika Ufalme Wangu zimejaa furaha, na maisha yao yanakua. Ninafanya kazi miongoni mwa wateule Wangu wote, na Siruhusu kazi Yangu kutiwa doa na mawazo ya binadamu, kwani Mimi binafsi hutekeleza kazi Yangu Mwenyewe. Ninapofanya kazi, mbingu na dunia na kila kitu ndani yake hubadilika na kufanywa upya, na wakati Ninapokamilisha kazi Yangu, mwanadamu hufanywa upya kabisa, haishi tena katika huzuni kwa sababu ya kile Ninachouliza, kwani sauti za furaha zinaweza kusikika kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wa dunia, na Mimi Huchukua nafasi hii kutoa miongoni mwa wanadamu baraka ambazo Mimi huwapa.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 33” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 50 Jina la Mwenyezi Mungu Lashuhudiwa katika Mataifa Yote ya Dunia

Inayofuata: 52 Msifu Mungu Ambaye Amerudi Akiwa Mshindi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp