521 Ni Yule Anayefuatilia Ukweli tu Ndiye Anayeza Kufanywa Mkamilifu na Mungu

1 Kuhusiana na masuala ya kila siku, kunayo yale ambayo watu wanayaona kuwa makubwa sana na muhimu, na mengine yanaonekana kuwa mambo madogo madogo tu. Mara nyingi watu huyaona masuala haya makubwa kuwa ndiyo muhimu zaidi, na wanayachukulia kwamba yametumwa na Mungu. Hata hivyo, kwenye mkondo wa masuala haya makubwa kujitokeza, kutokana na kimo finyu cha binadamu, na kutokana na kiwango cha binadamu kisichotosha, mara nyingi binadamu haendani sawa na nia za Mungu, hawezi kupata ufunuo wowote, na hawezi kufaidi maarifa yoyote halisi yenye thamani. Kuhusu masuala madogo, haya yanapuuzwa tu na binadamu, kuachwa kuponyoka kidogokidogo. Hivyo basi, wamepoteza fursa nyingi sana za kuchunguzwa mbele ya Mungu, kujaribiwa na Yeye. Je unafaa kuwapuuza watu, masuala na hali hizi siku zote ambazo Mungu anakupangilia wewe, inamaanisha kwamba kila siku, hata kila wakati, siku zote unakana ukamilifu wa Mungu kwako, na uongozi wa Mungu.

2 Je unafaa kuwapuuza watu, masuala na hali hizi siku zote ambazo Mungu anakupangilia wewe, inamaanisha kwamba kila siku, hata kila wakati, siku zote unakana ukamilifu wa Mungu kwako, na uongozi wa Mungu. Kila Mungu anapopanga hali hizi kwako wewe, Yeye anakuangalia kwa siri, Anauangalia moyo wako, Anaziangalia fikira na hali zako, Anaangalia namna unavyofikiria wewe, Anaangalia namna unavyochukua hatua. Kama wewe ni mtu asiyejali—mtu ambaye hajawahi kujali kuhusu njia ya Mungu, neno la Mungu, au ukweli—basi hutajali, hutatilia maanani kile ambacho Mungu anataka kukamilisha, na yale ambayo Mungu anakuhitaji wewe kufanya wakati Anapopanga hali hizi kwako wewe. Hutajua pia namna ambavyo masuala haya ya kila siku yanavyohusiana na ukweli au nia za Mungu.

3 Baada ya kukabiliwa na majaribio mara kwa mara, humkuzi Mungu katika moyo wako, na hushughulikii zile hali ambazo Mungu anakupangia wewe kama zilivyo—kama majaribio ya Mungu au mitihani ya Mungu. Badala yake unakataa fursa ambazo Mungu amekupa wewe moja baada ya nyingine, na unaziacha kutokomea mara kwa mara. Je huu si kutotii kwa kiwango cha juu na binadamu? Wakati watu wanapokataa majaribio, mitihani, ambayo Mungu anawapa, wakati wanapoikwepa, kunao mwelekeo mmoja tu ambao Mungu anao kwa watu kama hawa. Mungu husukumia mbali aina hii ya watu kutoka kina cha moyo Wake. Huu ndio uamuzi wa mwisho wa Mungu kwa mtu ambaye hajawahi kutembea katika njia ya Mungu, ambaye hajawahi kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Umetoholewa kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 520 Mungu Atawabariki Wale Wanaofuatilia Ukweli kwa Dhati

Inayofuata: 522 Ishi Katika Maneno ya Mungu ili Uwe na Kazi ya Roho Mtakatifu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp