775 Tafuta Kumpenda Mungu Bila Kujali Mateso Yako Ni Makubwa Vipi

Utajua kweli jinsi kazi ya Mungu ni ya thamani leo.

1 Leo, watu wengi sana hawana ufahamu huo. Wao huamini kwamba mateso hayana thamani, wao hukanwa na ulimwengu, maisha yao ya nyumbani yamesumbuliwa, wao si wapendwa wa Mungu, na matazamio yao ni matupu. Kuteseka kwa watu wengine hufikia kiwango fulani, na fikira zao hugeukia kifo. Huu si upendo wa kweli kwa Mungu; watu kama hao ni waoga, hawana ustahamilivu, wao ni wadhaifu na wasio na nguvu! Mungu ana hamu ya mwanadamu kumpenda Yeye, lakini kadri mwanadamu anavyompenda Yeye, ndivyo kuteseka kwa mwanadamu huwa kwingi zaidi, na kadri mwanadamu anavyompenda Yeye, ndivyo majaribio ya mwanadamu huwa makubwa zaidi. Ikiwa unampenda Yeye, basi kila aina ya mateso yatakufika—na ikiwa humpendi, basi labda kila kitu kitaendelea kwa urahisi kwako, na kila kitu kinachokuzunguka kitakuwa kitulivu kwako.

2 Unapompenda Mungu, utahisi kwamba mengi kandokando yako hayawezi kushindikana, na kwa sababu kimo chako ni kidogo sana utasafishwa; aidha, huwezi kumridhisha Mungu, na daima utahisi kwamba mapenzi ya Mungu ni ya juu sana, kwamba hayawezi kufikiwa na mwanadamu. Kwa sababu ya haya yote utasafishwa—kwa sababu kuna udhaifu mwingi ndani yako, na mengi yasiyoweza kuridhisha mapenzi ya Mungu, utasafishwa ndani. Lakini lazima muone kwa dhahiri kwamba utakaso hutimizwa tu kupitia usafishaji. Hivyo, katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana.

Umetoholewa kutoka katika “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 774 Maonyesho ya Petro ya Upendo kwa Mungu

Inayofuata: 776 Petro Alishikilia Imani na Upendo wa Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp