Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

934 Lazima Utafute Mapenzi ya Mungu Katika Vitu Vyote

1 Punde tu watu wanapokuwa na haraka wakati wakiutimiza wajibu wao, hawajui jinsi ya kuuzoea; punde tu wanaposhughulika na mambo, hali yao ya kiroho inakuwa na matatizo; hawawezi kudumisha hali yao ya kawaida. Inawezekanaje kuwa hivi? Unapoombwa kufanya kazi kidogo, haufuati ukawaida, unakosa mipaka, husogei karibu na Mungu na unajitenga mbali na Mungu. Hili linadhibitisha kwamba watu hawajui jinsi ya kuwa na uzoefu. Haidhuru nini ufanyalo, unapaswa kwanza kuelewa kwa nini unalifanya, asili ya jambo hilo ni ipi, Ikiwa unafanya kitu kutimiza wajibu wako, basi unapaswa kutafakari: Nitalifanyaje hili? Nitatimizaje wajibu wangu vyema ili nisiwe nafanya kwa uzembe tu? Unapaswa kusogea karibu na Mungu katika jambo hili.

2 Kusogea karibu na Mungu kunamaanisha kutafuta ukweli katika jambo hili, kutafuta njia ya kutenda, kutafuta mapenzi ya Mungu, kutafuta jinsi ya kumridhisha Mungu. Haihusu kufanya taratibu za kidini au tendo lionekanalo kwa nje; inafanywa kwa kusudi la kutenda kulingana na kweli baada ya kutafuta mapenzi ya Mungu. Unapotimiza wajibu wako au kushughulikia kitu, unapaswa daima kufikiri: Ninapaswaje kutimiza wajibu huu? Kusudi la Mungu ni lipi? Sogea karibu na Mungu kupitia unachofanya; kwa hufanya hivyo unazitafuta kanuni na ukweli wa matendo yako pamoja na nia za Mungu, na hutapotea kutoka kwa Mungu katika chochote utendacho. Mtu wa aina hii tu ndiye anayemwamini Mungu kwa kweli. Sasa wakati mambo mengine yajapo kwa watu, wanafanya shingo zao kuwa ngumu tu na kutenda kulingana na nia zao binafsi. Mtu wa aina hii hana Mungu ndani yake, ana yeye binafsi tu moyoni mwake na hawezi tu kuuweka ukweli katika matendo kwa vitu afanyavyo.

3 Kutofanya vitu kulingana na ukweli ni kufanya vitu kulingana na mapenzi yako, na kufanya vitu chini ya mapenzi yako ni kumwacha Mungu; yaani Mungu hayupo ndani ya moyo wako. Mawazo ya binadamu kwa kawaida yanaonekana mazuri na sahihi kwa watu, na yanaonekana kana kwamba hayawezi kukiukaukweli kwa kiasi kikubwa sana. Watu huhisi kwamba kufanya mambo kwa jinsi hii kutakuwa kuweka ukweli katika matendo; wanahisi kwamba kufanya mambo kwa jinsi hiyo kutakuwa kumtii Mungu. Hakika, hawamtafuti Mungu kwa kweli au kumwomba Mungu kulihusu; hawajitahidi kulifanya vizuri kulingana na mahitaji ya Mungu, ili kuridhisha mapenzi Yake. Hawamiliki hali hii ya kweli; hawana hamu kama hiyo. Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo watu hufanya katika matendo yao. Unamwamini Mungu, lakini humweki Mungu moyoni mwako. Hii sio dhambi vipi? Je, hujidanganyi mwenyewe? Ni aina gani za athari ambazo unaweza kuvuna ukiendelea kuamini jinsi hiyo? Isitoshe, umuhimu wa imani unaweza kuonyeshwa vipi?

Umetoholewa kutoka katika “Kutafuta Mapenzi ya Mungu ni Kwa Ajili ya Kutenda Ukweli” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia:Tafuta Kuwa Yule Anayemwabudu Mungu kwa Kweli

Inayofuata:Kipimo cha Mungu cha Kupima Mema na Maovu

Maudhui Yanayohusiana

 • Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu

  I Kama washiriki wa jamii ya wanadamu, kama wafuasi wa Kristo wa dhati, ni wajibu wetu, jukumu letu kutoa akili zetu na miili yetu kwa kutimiza agizo …

 • Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa

  1 Kwa kuwa Mungu alimwokoa mwanadamu, Atamwongoza; kwa kuwa Anamwokoa mwanadamu, Atamwokoa na kumpata kabisa; kwa kuwa anamwongoza mwanadamu, Atamfiki…

 • Tilia Maanani Majaliwa ya Binadamu

  1 Mungu anawahimiza watu wa makabila yote, nchi zote na hata nyanja: Sikilizeni sauti ya Mungu na kuona kazi Yake; tilia maanani jaala ya binadamu; mf…

 • Upendo wa Kweli

  1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha kutoka kwa ne…