263 Siri Moyoni Mwako
1 Kunayo siri kubwa moyoni mwako, ambayo hujawahi kuifahamu kamwe, kwa sababu umekuwa ukiishi katika ulimwengu bila mwanga. Moyo wako na roho yako vimepokonywa na yule mwovu. Macho yako yamezuiwa kwa giza yasione, na huwezi kuliona jua angani wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu, na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yakitiririka kutoka katika kiti cha enzi.
2 Umepoteza kila kitu ambacho kilipaswa kuwa chako kwa haki, kila kitu ambacho Mwenye uweza alikupa. Umeingia katika bahari ya mateso isiyokuwa na mwisho, bila nguvu ya kukuokoa, bila matumaini ya kurudi ukiwa hai, na yote unayofanya ni kupambana na kusonga kila siku.… Tokea wakati huo, hungeweza kuepuka kuteswa na yule mwovu, uliwekwa mbali na baraka za mwenye Uweza, mbali na kukimu kwa mwenye Uweza, unatembea katika njia ambayo huwezi kurejea nyuma tena. Kuitwa mara milioni hakuwezi kusisimua moyo wako na roho yako. Unalala fofofo mikononi mwa yule mwovu, ambaye amekushawishi katika ulimwengu usio na mipaka, bila mwelekeo na bila alama za barabarani.
3 Tokea hapo, umepoteza hali yako ya asili ya kutokuwa na hatia na utakatifu wako, na kuanza kujificha kutokana na utunzaji wa mwenye Uweza. Ndani ya moyo wako, yule mwovu anakuelekeza katika kila jambo na anakuwa uhai wako. Humwogopi tena, kumwepuka, au kumshuku; badala yake, unamchukulia kama Mungu aliye moyoni mwako. Unaanza kumtukuza na kumwabudu, na nyinyi wawili mnakuwa msiotengana kama mwili na kivuli chake, kila akitoa nafsi yake kwa mwingine katika uzima na mauti. Hujui lolote kabisa kuhusu mahali ulikotoka, kwa nini ulizaliwa, au kwa nini utakufa.
4 Unamtazama Mwenye uweza kama mgeni; hujui mwanzo Wake, sembuse yale yote ambayo Amekutendea. Kila kitu kitokacho Kwake kimekuwa cha kuchukiza kwako. Huvitunzi wala kujua thamani yavyo. Unatembea kando na yule mwovu, kuanzia siku ile ulipoanza Mwenye uweza alianza kukukimu. Wewe na yule mwovu mmepitia maelfu ya miaka ya dhoruba na tufani pamoja, na pamoja naye, mnampinga Mungu ambaye alikuwa chanzo cha uhai wako. Hujui lolote kuhusu kutubu, sembuse kwamba umefikia ukingo wa kuangamia.
5 Unasahau kwamba yule mwovu amekujaribu na kukutesa; umesahau asili yako. Kwa njia hii, yule mwovu amekuwa akikuharibu, hatua baada ya hatua, hata mpaka leo. Moyo wako na roho yako vimekufa ganzi na vimeoza. Umeacha kulalamika juu ya maudhi ya dunia ya wanadamu, na huamini tena kwamba dunia si ya haki. Bado hujali sana kama Mwenye uweza yupo. Hii ni kwa sababu ulimchukulia yule mwovu kuwa baba yako wa kweli kitambo, na huwezi tena kutengana naye. Hii ndiyo siri iliyo moyoni mwako.
Umetoholewa kutoka katika “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” katika Neno Laonekana katika Mwili