Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

239 Niliona Upendo wa Mungu katika Kuadibu na Hukumu

1

Ee Mungu! Ingawa nimevumilia mamia ya majaribio na mateso,

na hata nimekuwa karibu na kifo,

mateso hayo yameniruhusu kukujua Wewe kwa kweli na kupata wokovu mkuu.

Kama adabu Yako, hukumu na nidhamu vingeondoka kutoka kwangu,

basi ningeishi gizani, chini ya himaya ya Shetani.

Ee Mungu! Ninakusihi, nakuomba usichukue faraja yangu kubwa kutoka kwangu,

hata kama ni maneno machache tu ya uhakikisho.

Nimefurahia upendo wako, na leo hii siwezi kuwa mbali na Wewe;

jinsi gani, Nieleze, singeweza kukupenda Wewe?

2

Mwili wa binadamu una faida gani?

Kama adabu Yako na hukumu ingeniwacha,

ingekuwa kana kwamba Roho Wako alikuwa ameniacha,

ni kama Wewe Haukuwa tena pamoja nami.

Kama Wewe utanipa ugonjwa, na kuchukua uhuru wangu, naweza kuendelea kuishi,

lakini adabu Yako na hukumu vikiondoka kutoka kwangu,

sitakuwa na njia ya kuendelea kuishi.

Ee Mungu! Ninakusihi, nakuomba usichukue faraja yangu kubwa kutoka kwangu,

hata kama ni maneno machache tu ya uhakikisho.

Nimefurahia upendo wako, na leo hii siwezi kuwa mbali na Wewe;

jinsi gani, Nieleze, singeweza kukupenda Wewe?

3

Kama ningekuwa bila adabu Yako na hukumu,

ningepoteza upendo Wako, upendo ambao ni mkuu sana mpaka sina maneno ya kuueleza.

Bila Upendo wako, ningeishi chini ya himaya ya Shetani,

na singeweza kuuona uso wako mtukufu.

Jinsi gani, Nieleze, ningeweza kuendelea kuishi?

Giza kama hili, maisha kama haya, singeweza kuvumilia.

Mimi kuwa na wewe ni kama kukuona Wewe, hivyo ni jinsi gani ningeweza kukuacha?

Ee Mungu! Ninakusihi, nakuomba usichukue faraja yangu kubwa kutoka kwangu,

hata kama ni maneno machache tu ya uhakikisho.

Nimefurahia upendo wako, na leo hii siwezi kuwa mbali na Wewe;

jinsi gani, Nieleze, singeweza kukupenda Wewe?

4

Nimemwaga machozi mengi ya huzuni kwa sababu ya upendo Wako,

ilhali daima nimehisi kuwa maisha kama haya ni ya maana zaidi,

yenye uwezo mwingi wa kuniimarisha, yenye uwezo zaidi wa kunibadilisha,

na yenye uwezo zaidi wa kunifanya nifikie ukweli ambao lazima viumbe wawe nao.

Ee Mungu! Ninakusihi, nakuomba usichukue faraja yangu kubwa kutoka kwangu,

hata kama ni maneno machache tu ya uhakikisho.

Nimefurahia upendo wako, na leo hii siwezi kuwa mbali na Wewe;

jinsi gani, Nieleze, singeweza kukupenda Wewe?

Iliyotangulia:Ni Watu Waaminifu Pekee Walio na Mfano wa Binadamu

Inayofuata:Kutoenda Mbali na Maneno ya Mungu

Maudhui Yanayohusiana