547 Mungu Awaokoa Wale Wanaopenda Ukweli

1 Mambo yote yanayoinuka kila siku, makubwa ama madogo, ambayo yanaweza kutikisa uamuzi wako, kuumiliki moyo wako aukuzuilia uwezo wako wa kufanya wajibu wako, na kuendelea kwako mbele vinahitaji kushughulikiwa kwa bidii; lazima vichunguzwe kwa makini na ukweli wa vitu hivi utafutwe. Hivi ni vitu vyote ambavyo vinafanyika katika ulimwengu wa uzoefu. Watu wengine huacha kazi zao wakati kitu kibaya kinawafikia, na wanashindwa kusimama kwa miguu yao baada ya kila pingamizi. Watu hawa wote ni wapumbavu ambao hawapendi ukweli, na hawatapata faida i hata wakiishi maisha yao yote kwa imani. Watu wapumbavu kama hao watawezaje kufuata hadi mwisho?

2 Watu werevu na wale ambao wana ubora wa ndani wa kweli amabao wanaelewa masuala ya kiroho ni watafutaji wa ukweli; jambo likiwafanyikia mara kumi, basi mara nane kwa kumi pengine wataweza kupata ufunuo kiasi, kupata funzo fulani, kfikia nuru na kufanya maendeleo. Mambo yanapomfanyikia mpumbavu mara kumi—yule asiyeelewa masuala ya kiroho—haitamfaidi maishani hata mara moja, haitawabadilisha hata mara moja, na haitawasababisha waelewe asili yao hata mara moja, na huu ndio mwisho wao. Kila wakati kitu kinapowafanyikia, wanaanguka chini, na kila wakati wanapoanguka chini, wanahitaji mtu mwingine kuwasaidia kusimama tena, kuwabembeleza. Je, bado kuna sababu zinginezo kwa watu kama hawa wasio na maana kuokolewa?

3 Wokovu wa Mungu wa binadamu ni wokovu wa wale wanaopenda ukweli, wokovu wa sehemu ndani yao ambayo ina ari ya mapenzi na maazimio na sehemu yao inayotamani ukweli na haki mioyoni mwao. Azimio la mtu ni sehemu yao ndani ya mioyo yao inayotamani haki, wema na ukweli, na iliyo na dhamiri. Mungu hukoa sehemu hii ya watu, na kupitia hiyo Anabadili tabia yao potovu, ili waweze kuelewa na kupata ukweli, ili upotovu wao uweze kutakaswa na tabia ya maisha yao ikaweze kubadilishwa. Ikiwa ndani yako hakuna upendo wa ukweli ama hamu ya haki na mwanga wakati wowote unapokumbana na uovu, basi hakuna njia ya kuokolewa.

Umetoholewa kutoka katika “Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 546 Mungu Huwapenda Wale Wanaofuatilia Ukweli

Inayofuata: 548 Mungu Awapenda Wale Walio na Azimio

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp