268 Jinsi Shetani Atumiavyo Mitindo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu

1 Suala la mwisho ni jinsi Shetani kutumia kwa manufaa yake mitindo ya kijamii kumpotosha mwanadamu. Tunataka tu kuzungumza kuhusu mawazo ambayo mitindo ya kijamii inaleta kwa watu, jinsi inasababisha watu kutenda duniani, malengo ya maisha na mtazamo ambao inaleta kwa watu. Hii ni muhimu sana; inaweza kudhibiti na kushawishi hali ya akili ya mwanadamu. Moja baada ya nyingine, hii mitindo yote inabeba ushawishi mwovu unaoendelea kumpotosha mwanadamu, kumfanya kuendelea kupoteza dhamiri, ubinadamu na mantiki, na unaoshukisha maadili yao na ubora wao wa tabia zaidi na zaidi, hadi kwa kiwango ambamo tunaweza hata kusema wengi wa watu sasa hawana uadilifu, hawana ubinadamu, wala hawana dhamiri yoyote, wala akili yoyote.

2 SShetani hutumia hii mitindo ya kijamii kuvuta watu hatua moja baada ya nyingine hadi katika kiota cha mashetani, ili watu walionaswa katika mitindo ya kijamii bila kujua wanatetea pesa na tamaa za mwili, na pia kutetea uovu na ukatili. Punde mambo haya yameingia moyoni mwa mwanadamu. Mwanadamu anakuwa ibilisi Shetani! Hii ni kwa sababu ya mwelekeo kisaikolojia upi katika moyo wa mwanadamu? Mwanadamu huanza kupenda uovu na ukatili. Hawapendi uzuri ama wema, wala hata amani. Watu hawako radhi kuishi maisha rahisi ya ubinadamu wa kawaida, lakini badala yake wanataka kufurahia hadhi ya juu na utajiri mkubwa, kufurahia raha za mwili, na kutumia juhudi zote kuridhisha miili yao, bila vizuizi, hakuna vifungo vya kuwashikilia nyuma, kwa maneno mengine kufanya chochote wanachotaka.

3 Hivyo wakati mwanadamu ametumbukizwa katika mitindo ya aina hii, maarifa ambayo mmefunzwa yanaweza kuwasaidia kuwa huru? Kwa njia hii, mwanadamu anakuwa mwovu zaidi na zaidi, mwenye kiburi, mwenye kushusha hadhi, mwenye ubinafsi, na mwenye kijicho. Hakuna tena upendo kati ya watu, hakuna tena upendo wowote kati ya wanafamilia, hakuna tena uelewa wowote miongoni mwa jamaa na marafiki; mahusiano ya binadamu yamejawa ukatili. Kila mtu anataka kutumia mbinu katili kuishi miongoni mwa wanadamu wenzake; wanakamata riziki zao kwa kutumia ukatili; wanashinda vyeo vyao na kupata faida zao wenyewe kwa kutumia ukatili na wanafanya chochote watakacho kwa kutumia njia mbovu na katili. Si ubinadamu huu unatisha?

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 267 Shetani Huyadhibiti Mawazo kwa Umaarufu na Mali

Inayofuata: 269 Mungu Anautafuta Moyo Wako na Roho Yako

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp