145 Watakatifu Katika Enzi Zote Wanazaliwa Upya

Kiambata: Watakatifu katika enzi zote wanazaliwa upya! Watakatifu katika enzi zote wanazaliwa upya!

1 Tukifikiria shida na kifungo cha watakatifu katika enzi zote, hatuwezi kujizuia kulia. Wamepitia kila namna ya mateso na dhiki kati ya mwanadamu, wamekanyagwa na kukashifiwa. Wamevumilia machungu na udhalilishaji kwa vizazi, mapigo mengi, mapigo mengi ya mjeledi, uharibifu mwingi sana na mateso, kupigwa mawe na mauaji, pia. Miaka mingi sana katika giza, bila jua.

2 Kunatokea Jua la haki kutoka mashariki. Linaangaza katika ulimwengu mzima, vyote vinafanywa upya mara moja, na kubadilishwa. Hali nzuri mpya inaenea katika nchi nzima. Tunakuja katika nchi nzuri ya Kanaani, mioyo yetu imejazwa na furaha na hatuna wasiwasi tena. Harufu nzuri ya manukato inaenea ulimwenguni kote, inaelea ndani ya mioyo yetu. Furaha maalum inaijaza mioyo yetu, kana kwamba sisi tuko katika mbingu ya tatu. Tunaonja uzuri wa Mungu, tunapata joto la Mungu, kuna furaha kubwa mioyoni mwetu. Mioyo yetu daima itakuwa ya Mungu, Yeye ndiye mfalme wa mioyo yetu, Yeye ndiye mfalme wa mioyo yetu.

3 Kristo wa siku za mwisho ameonyesha ukweli, Ameleta njia ya uzima wa milele. Maneno Yake yanatuhukumu, yanatusafisha, kututakasa, kutubadilisha. Tumeteseka mamia ya majaribio na usafishaji, na kupata utamu katika machungu. Neno la Mungu limekuwa maisha yetu, na tunaishi upya. Tunatakaswa na Mungu, tunawekwa huru kutoka kwa upotovu wa Shetani, mioyo yetu huru zaidi ya awali. Tumepata wokovu wa Mungu, na tumezaliwa tena kutoka kifo. Mwenyezi Mungu ametuokoa, tumezaliwa tena, tumezaliwa tena.

Iliyotangulia: 143 Maneno Katika Mioyo ya Wakristo

Inayofuata: 147 Kuna Kundi Kama Hili la Watu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki