326 Cha Kusikitisha Zaidi Kuhusu Imani ya Binadamu kwa Mungu

1 Jambo la kusikitisha mno kuhusu imani ya wanadamu kwa Mungu ni kuwa wanadamu wanatekeleza usimamizi wao wenyewe katikati ya kazi ya Mungu na hawasikilizi usimamizi wa Mungu. Udhaifu mkubwa wa mwanadamu unaegemea katika jinsi, wakati huo huo anatafuta kujitoa kwa Mungu na kumwabudu, mwanadamu anaunda hatima yake kamilifu na kuhesabu jinsi ya kupokea baraka kubwa zaidi na hatima iliyo bora zaidi. Hata kama watu watafahamu jinsi walivyo wa kuhurumiwa, wenye chuki na walivyo ovyo, ni wangapi hapo ambao wanaweza kuachana na ukamilifu na matumaini yao? Na ni nani anayeweza kusimamisha hatua zake na kuacha kujifikiria yeye mwenyewe?

2 Mungu Anawahitaji wale watakaojihusisha kwa karibu Naye kukamilisha usimamizi Wake. Anawahitaji wale ambao watatoa mawazo yao na mwili kwa ajili ya kazi Yake ya usimamizi ili kujitoa Kwake; Hawahitaji wale watakaoinua mikono yao na kuomba kutoka Kwake kila siku, na hata wale wanaotoa kidogo na kusubiri kulipwa kwa hilo tendo la kutoa. Mungu Anawadharau wale wanaotoa michango kidogo na kuridhika. Anawachukia wenye roho katili ambao hukataa kazi ya usimamizi Wake na hutaka tu kuongea kuhusu kwenda mbinguni na kupata baraka. Anachukia hata zaidi na wale ambao hufaidika na fursa inayowezeshwa na kazi Anayoifanya katika kuokoa wanadamu.

3 Hii ni kwa sababu hawa watu hawajawahi kushughulishwa na Anachotarajia kupata Mungu kutokana na kazi Yake ya usimamizi. Wanashughulishwa tu na jinsi wanavyoweza kutumia hiyo fursa iliyowezeshwa na kazi ya Mungu ili kupata baraka. Hawajali roho Yake Mungu, kwa kuwa wanajishughulisha na mustakabali na hatima yao. Wale ambao wanakataa kazi ya usimamizi wa Mungu na hawana hata tamanio dogo katika jinsi Mungu Anavyowaokoa wanadamu na mapenzi Yake, wote wanafanya wapendavyo kando na kazi ya usimamizi wa Mungu. Tabia yao haikumbukwi na Mungu, na haikubaliwi na Mungu, na hata haiangaliwi kwa fadhila ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 325 Imani ya Mwanadamu kwa Mungu ni Mbaya Kupindukia

Inayofuata: 327 Ubaya wa Mwanadamu Kujaribu Kumrishisha Mungu kwa Ajili ya Hatima Yake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp