46. Kurudi Uzimani Kutoka Ukingoni mwa Mauti

Na Yang Mei, China

Mnamo 2007 niliugua ghafla ugonjwa sugu wa figo. Waliposikia habari hizi, mama yangu na shemeji yangu ambao ni Wakristo, na marafiki wengine wa Kikatoliki walikuja kunihubiria injili. Waliniambia kuwa mradi nimgeukie Bwana, ugonjwa wangu ungeponywa. Lakini sikuamini katika Mungu hata kidogo. Nilidhani kwamba ugonjwa unaweza kuponywa tu kupitia matibabu ya kisayansi, na kwamba ugonjwa wowote ambao hauwezi kuponywa na sayansi haungeweza kuponywa. Hata hivyo, kulikuwa na nguvu yoyote duniani kuliko nguvu ya sayansi? Imani katika Mungu ilikuwa aina ya tegemeo la kisaikolojia tu, na nilikuwa mwalimu wa shule ya serikali yenye hadhi, mtu ambaye alikuwa ameelimika sana na mwenye heshima, kwa hivyo singeanza kumwamini Mungu kabisa. Hivyo, niliwakataza na nikaanza kutafuta matibabu ya dawa. Ndani ya miaka michache nilikuwa nimetembelea takribani kila hospitali kubwa katika kaunti yangu ya nyumbani na katika jimbo lote, lakini hali yangu bado haikuimarika. Kwa kweli, ilikuwa inazidi kuwa mbaya, lakini kwa ukaidi nilishikilia njia yangu mwenyewe ya kutazama hali hiyo na nikasisitiza kwamba sayansi ingeweza kubadilisha chochote, kwamba uponyaji wa ugonjwa ulikuwa mchakato ambao unachukua muda.

Mnamo mwaka wa 2010 dada kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu alikuja kunihubiria injili ya ufalme wa Mungu. Alisema kuwa Bwana Yesu alikuwa amerudi katika ulimwengu wa kawaida kutenda kazi mpya, ambayo ilijumuisha kutoa ukweli wa kuhukumu na kuwatakasa watu. Hii ilikuwa hatua ya kazi ya Mungu iliyoundwa kuwaokoa wanadamu kikamilifu, na pia ndiyo ilikuwa fursa ya mwisho ya wanadamu kuokolewa na Mungu. Bado sikuwa tayari kukubali yote haya, lakini kwa sababu ya mapungufu yote na kufadhaika ambako nilikuwa nimekutana nako kwa miaka michache iliyopita nikitafuta matibabu, mtazamo wangu haukuwa mgumu kama ilivyokuwa hapo awali na nilijiruhusu nishawishiwe kuchukua kitabu cha maneno ya Mungu kutoka kwa yule dada. Lakini, wakati huo, kwa hakika sikuamini kuwa maneno katika kitabu hicho yalikuwa ukweli ulioonyeshwa na Mungu. Bado niliendelea kushikilia msimamo kuwa sayansi pekee ndiyo inayoweza kubadilisha majaliwa yangu, na hivyo niliendelea kuamini kuwa ni dawa tu ndizo ambazo zingeweza kuimarisha hali yangu. Mwishowe, nilikuwa nameza dawa nyingi zaidi kila siku kuliko nilivyokuwa nakula chakula, na bado hali yangu haikuonyesha hata ishara ndogo ya kuimarika. Nilipoteza hesabu ya idadi ya wakati ambao dada huyo alifika nyumbani kwangu, lakini bado nilikataa kumwamini Mungu. Hili liliendelea kwa takribani mwaka mmoja.

Kisha siku moja, bila kutarajia, macho yangu yote yaliwaa na miguu yangu yote miwili ilikufa ganzi kiasi kwamba nilishindwa kutembea. Madaktari walisema kwamba dalili zangu zilitokana na sumu ya dawa kutokana na kumeza dawa nyingi kwa miaka kadhaa. Kwanza nilikaa katika hospitali ya kaunti kwa wiki moja kisha nilihamishiwa hadi hospitali ya jeshi huko Beijing ambako nilitibiwa kwa mwezi mmoja. Kisha nilihamishiwa hospitali ya dawa za kienyeji za Kichina huko Beijing kupokea matibabu ya TCM. Lakini miezi hii miwili ya matibabu haikufanya chochote kuimarisha hali yangu. Daktari wangu mkuu hata alimuuliza mkuu wa zamani wa idara ya nyurolojia hospitalini aje anitazame, lakini hakukuwa na nafuu hata kidogo katika hali yangu. Kisha nikamsikia mchumba wa mwanangu akimtaja daktari huko Yunnan ambaye alikuwa maarufu kwa kuweza kutibu hali ngumu na tata kama yangu. Baada ya baadhi ya ugumu na mizunguko, nilifanikiwa kupelekwa huko kwa kiti cha magurudumu. Lakini baada ya kutibiwa kwa takribani mwezi mmoja, sio tu kwamba hali yangu haikuimarika, lakini dawa nilizokuwa nikimeza kwa ajili ya macho na miguu yangu kwa kweli zilizidisha ugonjwa wangu wa figo. Nikihisi nisiyeweza kusaidiwa, na niliyekosa utulivu sana, niliamua kwenda nyumbani. Baada ya hapo, niliacha matibabu na dawa zote za macho na miguu ili nilinde figo zangu.

Katika kipindi hicho, nilihisi kwamba hakukuwa na tumaini kwangu kabisa. Mara nyingi nilifikiria juu ya jinsi ambavyo niliweka imani yangu yote katika sayansi lakini sayansi ilikuwa imethibitisha kuwa isiyoweza kufanikisha matibabu ya ugonjwa wangu. Baada ya tumaini lolote nililokuwa nalo kwamba sayansi inaweza kuniponya kupotea, nilihisi mwenye huzuni sana na kuvurugika kabisa. Sikujua jinsi ningeendelea na maisha. Katika ukungu wa uchungu na mateso, mawazo yangu mara nyingi yalikuwa ya kichaa: “Je, kwa nini nimeteseka na magonjwa mengi sana na kwa nini hayawezi kutibiwa na dawa? Niliamini katika sayansi na kuwa na imani katika sayansi, na nilijitahidi kutafuta matibabu bora, na bado hakuna kitu kilichofanya kazi. Kwa kweli, hali yangu ilizidi kudhoofika. Inawezekana kwamba sayansi haiwezi kuniokoa? Inawezekana kwamba kweli kuna Mungu katika ulimwengu huu? Je, majaliwa ya kila mtu kweli yamo mikononi mwa Mungu?” Haijalishi nilifikiria kiasi gani juu ya masuala haya, sikuweza kupata majibu yoyote. Katika kipindi hicho, niliishi katika uchungu na mateso kila siku, na kila nilipofikiria juu yangu kuwa mgonjwa asiyejiweza ningelia machozi kwa siri. Nilihisi kuwa nilikuwa naihusisha familia yangu sana na sikutaka kuwa mzigo kwao tena. Katika zaidi ya wakati mmoja nilitaka kujitia kitanzi lakini niliogopa kifo. Kwa hivyo niliishi kila siku kama ilivyokuja na kungojea mauti yanijie …

Siku moja, mume wangu aliona kitabu ambacho yule dada kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu alikuwa ameniachia na akakifungua. Aliona kichwa kifuatacho, “Je, Ulikuwa Unajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu,” ambacho mara moja kilichukua usikivu wake. Kwa hivyo alinisomea kifungu kifuatacho: “Kazi ya Mungu ni ile usiyoweza kuelewa. Kama huwezi kufahamu kama uamuzi wako ni sahihi wala kujua kama kazi ya Mungu inaweza kufaulu, basi mbona usijaribu bahati yako na kuona iwapo huyu mwanadamu wa kawaida ni wa msaada mkubwa kwako, na iwapo Mungu amefanya kazi kubwa(Neno Laonekana katika Mwili). Kifungu hiki kifupi kilikuwa kama shoti ya furaha moyoni mwangu! Mstari “basi mbona usijaribu bahati yako,” hasa, ulizidi kuonekana akilini mwangu. Ulikuwa kama mwale wa mwanga ulionang'aa juu ya moyo wangu uliokuwa wenye ukiwa, na ilionekana kama kwamba ningeona mwanga hafifu wa tumaini la kuishi. Kwa haraka nilimfanya mume wangu asome vifungu vingine viwili vya maneno ya Mungu, ambayo yalikuwa na ukweli juu ya Mungu kutumia neno Lake kuhukumu na kuwatakasa watu na kubadilisha tabia zao za maisha. Yote haya yalikuwa mapya kwangu, na hata ingawa sikuelewa kabisa umuhimu kamili wa kile kilichokuwa kikisemwa, nilihisi moyoni mwangu kwamba mafundisho haya yalikuwa tofauti na injili ya Bwana Yesu ambayo nilikuwa nimesikia kutoka kwa watu wengine. Walikuwa mara nyingi wameniambia kuhusu kupata neema, na kwamba kile nilichohitaji kufanya ni kumwamini Mungu na ugonjwa wangu ungetibiwa, jambo ambalo sikuamini. Lakini maneno ya Mwenyezi Mungu yalionekana kuwa ya vitendo zaidi, na kadiri nilivyoyasikia zaidi ndivyo nilivyotaka kusikia zaidi.

Baada ya hapo, nilimfanya mume wangu anisomee maneno kadhaa ya Mungu kila siku. Kwenye kitabu hicho ilisema kwamba watu wa dini wanaamini katika Mungu lakini hawamjui Mungu na hata wanampinga Mungu, na kwamba mara nyingi wao hutenda dhambi wakati wa mchana na wanaziungama usiku. Hii ilinishawishi zaidi kwa sababu mama yangu, na shemeji zangu wawili walikuwa Wakristo na njia waliyoishi ilikuwa kama maneno ya Mungu yalivyoeleza. Kwa kweli walitenda dhambi na kisha kuungama na kisha kuzitenda tena. Wakati huo ndipo nilikuwa na mwamko wa kiroho: Je, kweli hii ni sauti ya Mungu? Ikiwa sio Mungu, basi ni vipi kwamba mwandishi anauelewa ulimwengu wa kidini vizuri sana? Wasioamini hawaelewi, wakuu na watu maarufu hawana habari, na hata watu wa dini wenyewe hawatambui kuwa wanaamini katika Mungu lakini pia wanampinga Mungu. Kadiri nilivyofikiria zaidi kulihusu ndivyo nilivyohisi kwamba maneno katika kitabu hicho si vitu ambavyo watu wangeweza kuonyesha, na kwamba labda yalikuwa maonyesho ya mwili wa Mungu katika ulimwengu wa kawaida.

Siku chache tu baadaye, yule dada ambaye hapo awali alikuwa amenihubiria injili ya Mwenyezi Mungu alisikia kwamba nilikuwa nimerudi nyumbani baada ya kuwa hospitalini na akaja nyumbani kwangu, akiambatana na dada mwingine, kunihubiria injili tena. Wakati huu nilikuwa najua sauti ya dhamiri yangu ikiniambia: “Nimekuwa mgonjwa asiyejiweza lakini akina dada hawajaniacha kwa chukizo na hata wamekuja kunihubiria injili tena na tena. Hili ni jambo ambalo watu wa kawaida hawangeweza kufanya. Mtu yeyote mwingine angekuwa amenisahau zamani.” Akilini mwangu ilikuwa wazi kabisa kwamba upendo wa aina hii lazima uwe umetoka kwa Mungu, kwani hauwezi kupatikana kamwe katika ulimwengu wa kawaida. Kama msemo unavyosema, “Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki,” na siku hiyo nilipitia hili kwa kina. Kwamba familia yangu ilikaa nami ni kitu ambacho hawangeweza kukwepa, lakini kwa watu hawa, ambao hawakuwa na uhusiano wowote na mimi na ambao hawakuwa na nia mbaya au masharti, kuja mara kwa mara kwa zaidi ya mwaka mmoja ili wanihubirie injili na wajitolee kwa ajili ya mgonjwa asiyejiweza kama mimi, kulionyesha jinsi imani, upendo na uvumilivu wao ulivyokuwa wa kushangaza sana! Niliguswa sana na upendo wa Mungu, na tangu hapo sikuwa na sababu ya kuikataa injili ya Mungu tena. Kama matokeo, mimi na mume wangu tuliikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho.

Mnamo Juni 2011, mimi na mume wangu tulianza rasmi maisha yetu ya kanisa katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kwa sababu macho yangu hayakuwa yanaona vizuri sana kiasi cha kutosha kuniruhusu nisome peke yangu, kwa kawaida mume wangu alinisomea maneno ya Mungu, na wakati wa mikutano ya kanisa ndugu pia walinisomea maneno ya Mungu. Wakati mwingine nilipokuwa peke yangu nilikuwa pia nasikiza nyimbo. Baadaye, nilipata sababu ya ugonjwa na kuteseka kwangu katika maneno ya Mungu: “Uchungu wa kuzaliwa, kufa, magonjwa na uzee uliopo katika maisha yote ya mwanadamu ulitoka wapi? Ni kwa sababu ya nini ndio watu walikuwa na vitu hivi mwanzo? Je, mwanadamu alikuwa na vitu hivi alipoumbwa mara ya kwanza? Hakuwa navyo, sivyo? Hivyo, vitu hivi vilitoka wapi? Vitu hivi vilikuja baada ya wanadamu kujaribiwa na Shetani na miili yao ikasawijika. Uchungu wa mwili, mateso yake na utupu wake, na pia masuala yenye taabu sana ya dunia ya binadamu yote yalikuja baada ya wanadamu kupotoshwa na Shetani, kutoka wakati Shetani alipoanza kuwatesa watu; matokeo yalikuwa kwamba walisawijika zaidi na zaidi. Maradhi ya wanadamu yakawa makubwa zaidi na mateso yao yakawa makali zaidi. Watu zaidi walihisi utupu na tanzia ya dunia ya binadamu na vilevile kutoweza kwao kuendelea kuishi hapo, na walihisi matumaini madogo zaidi kwa dunia. Yote haya yalikuja baada ya kupotoshwa na Shetani. Kwa hiyo, mateso haya yaliletwa na Shetani kwa wanadamu, na yalikuja tu baada ya wao kupotoshwa na Shetani na wakasawijika. … Hii ndiyo maana haiwezekani kwako kuwa na magonjwa, matatizo na kuhisi mwenye kutaka kujitia kitanzi na wakati mwingine pia kuhisi huzuni ya dunia, au kwamba maisha hayana maana. Hiyo ni kusema, kuteseka huku bado kuko chini ya uongozi wa Shetani; ni mojawapo ya udhaifu wa kusababisha mauti wa mwanadamu(“Umuhimu wa Mungu Kuuonja Mateso ya Dunia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalikuwa sahihi katika kueleza jinsi mateso yaliyoletwa na maumivu ya ugonjwa yalikuwa makubwa sana hivi kwamba nilikuwa nimepoteza ridhaa yote ya kuishi na nilitaka kujitia kitanzi. Lakini maneno ya Mungu yalisema kwamba maumivu hayo yote ya magonjwa na mateso yalitokana na njia mbaya za Shetani. Mwanzoni, sikuelewa kabisa kwa nini Mungu alisema mambo haya, lakini baada ya kusoma maneno zaidi ya Mungu polepole nilikuja kuelewa ukweli huu.

Alasiri moja mume wangu alikuwa akinisomea maneno ya Mungu kama kawaida, na nikasikia maneno haya ya Mungu: “Kutoka wakati mwanadamu kwanza alikuwa na sayansi ya jamii, akili yake ilishughulishwa na sayansi na maarifa. Kisha sayansi na maarifa vikawa vyombo vya kutawala mwanadamu, na hapakuwa tena na nafasi ya kutosha kumwabudu Mungu, na hapakuwa tena na mazingira mazuri ya kumwabudu Mungu. Nafasi ya Mungu ikashuka hata chini zaidi moyoni mwa mwanadamu. Dunia moyoni mwa mwanadamu bila nafasi ya Mungu ni giza, tupu bila matumaini. … Sayansi, maarifa, uhuru, demokrasia, wasaa wa mapumziko, faraja, haya yote ni mapumziko ya muda, Hata na mambo haya, mwanadamu hataepuka kufanya dhambi na kuomboleza udhalimu wa jamii. Mambo haya hayawezi kupunguza tamaa ya mwanadamu na hamu ya kuchunguza. Kwa sababu mwanadamu aliumbwa na Mungu na kafara na uchunguzi usio na sababu wa mwanadamu vitamwongoza tu kwa dhiki zaidi. Mwanadamu daima atakuwa katika hali ya hofu isiyoisha, hatajua jinsi ya kuukabili mustakabali wa wanadamu, ama jinsi ya kuikabili njia iliyo mbele. Mwanadamu atakuja hata kuogopa sayansi na elimu, na kuhofia hata zaidi utupu ulio ndani yake sana(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote). Ni wakati niliposikia maneno haya ndipo mwishowe nilielewa kwa nini Mungu alisema kwamba magonjwa na mateso yote ya wanadamu yanatoka kwa Shetani: Shetani hutumia maarifa na sayansi kutupotosha. Shetani hutujaza na maoni yake ya upuuzi, kama vile “Mwanadamu aligeuka kutoka kwa sokwe,” “Hakujawahi kuwa na Mwokozi yeyote,” “Maarifa yanaweza kubadili majaliwa yako,” “Kudura ya mtu imo mkononi mwake mwenyewe,” “Sayansi huwaokoa watu,” na “Mwanadamu anaweza kuushinda ulimwengu.” Shetani amewatia wanadamu kasumba na falsafa, sheria, maoni na fikira hizi. Zimekaa ndani ya mioyo na roho za watu, na kuwalazimisha watu kuwa na imani potovu katika maarifa na kuiabudu sayansi. Watu wanajidanga kwamba wanaweza kubadilisha majaliwa yao na maarifa au kutumia sayansi kutatua kila shida ngumu. Watu wamechukua mawazo ya kipumbavu ya Shetani kuunda msingi wa maisha yao, na kwa hivyo wamechukuliwa kama mateka, wakiwa wamefungwa, na kudhibitiwa na Shetani. Watu wameanza kukataa yote yanayotokana na Mungu, kujiweka mbali na utunzaji na ulinzi wa Mungu. Shetani huwadhibiti kwa hila kama fundi wa kuchezesha vikaragosi anavyocheza na vikaragosi wake, na mimi nilikuwa mmoja tu wa mamilioni wanaoumizwa kwa njia hii. Nilipokuwa mgonjwa, nilitegemea sayansi initibu; niliiamini na kuiabudu sayansi kwa upofu. Nilidhani kwa kweli kwamba wataalamu katika hospitali maarufu, na mbinu zao zilizoendelea na vifaa vya kisasa vya matibabu, wangeweza kuuponya ugonjwa wangu. Lakini sio tu kwamba hali yangu ilishindwa kuimarika, kwa kweli niliishia karibu kufa. Vitu vya pekee ambavyo sayansi iliniletea vilikuwa ni matumaini kama ndoto na maumivu yasiyoweza kubadilika. Sayansi ilinisababisha nisimwamini Mungu, na kwa hivyo muda baada ya muda nilimwasi Mungu, nikampinga, na nilikataa wokovu Wake. Lakini licha ya uasi wangu, Mungu hakukata tamaa juu ya wokovu wangu, na kufikia sasa ametumia maneno Yake kunielekeza. Kidogo kidogo, Ameiamsha roho yangu, ambayo hapo zamani ilikuwa imezimwa na maarifa na sayansi. Mimi, ambaye hapo zamani nilikuwa karibu na kifo, sasa nilikuja mbele za Mungu na kupata wokovu wa Mungu.

Mume wangu aliendelea kunisomea maneno ya Mungu kila siku, na siku moja nilisikia maneno haya ya Mungu: “Mungu aliumba dunia hii, Aliumba mwanadamu huyu, na zaidi ya hayo Alikuwa muasisi wa utamaduni wa zamani wa Giriki na ustaarabu wa binadamu. Ni Mungu tu anayemfariji huyu mwanadamu, na ni Mungu tu anayemtunza mwanadamu huyu usiku na mchana. Ukuaji na maendeleo ya binadamu hayatengani na ukuu wa Mungu, na historia na mustakabali wa mwanadamu ni zisizochangulika kutoka kwa miundo ya Mungu. … Iwapo mwanadamu anataka kuwa na majaliwa mazuri, iwapo nchi inataka kuwa na majaliwa mazuri, basi lazima mwanadamu ampigie Mungu magoti kwa ibada, atubu na kukiri mbele ya Mungu, la sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote). Kifungu hiki kilinisaidia nigundue kuwa majaliwa ya watu wote yamo mikononi mwa Mungu na kwamba Mungu ndiye chanzo cha maisha ya mwanadamu. Ni kwa kuja mbele za Mungu, kumfuata Mungu, na kumwabudu Mungu tu ndiyo watu wanaweza kuwa na hatima nzuri. Watu wanapoenda mbali na Mungu, kumpinga na kumwacha Mungu na badala yake wanamtegemea Shetani, wanajiwasilisha kwa Shetani. Kama matokeo, watadhuriwa na kukanyagwa na Shetani, na watakabiliwa na misiba isiyo na mwisho na mateso yasiyo na kikomo. Hivi ndivyo watu hujidhuru na kujiletea maafa. Wakati huo, niligundua jinsi nilivyokuwa mpumbavu, kipofu, na mwenye kuhurumiwa. Niliona kuwa maoni yangu juu ya maarifa na sayansi yote yalikuwa sumu tu, vyombo tu ambavyo Shetani alitumia kunidanganya. Miaka hii yote nilikuwa nikitiwa sumu na ibilisi, na sasa nilijuta sana. Kutoka kwa kina cha moyo wangu, nilihisi hamu ya kweli kwa Mungu. Nilikuwa tayari kutenda kama watu wa Ninawi waliorekodiwa katika Biblia, kujitupa chini mbele za Mungu na kukiri na kutubu. Nilitaka kuachana na njia zangu zote mbaya na kukubali mwongozo na riziki ambayo Mungu hutoa. Nilitaka kumfuata Mungu na kumwabudu, na kwa hivyo niliomba sana nipewe majukumu ya kukaribisha wageni kanisani. Katika maingiliano yangu na ndugu hakuna mtu aliyenidharau au kunishushia hadhi kwa sababu ya ugonjwa wangu. Kwa kweli, walinipa msaada mkubwa na kunitia moyo na kila wakati nilihisi kuwa nimezingirwa na upendo wao wa dhati.

Baada ya muda kupita, ugonjwa wangu bado haukupungua na kwa hivyo nilianza kufanya madai kwa Mungu, nikimuuliza Mungu anisaidie nipatenafuu. Lakini akina dada walishiriki yafuatayo na mimi: “Mungu ndiye Muumba wa vitu vyote na sisi ndio viumbe, kwa hivyo haijalishi jinsi Mungu anavyotutendea lazima tukubali mipango na mipangilio Yake. Tukiomba vitu kutoka kwa Mungu, tunaonyesha tu hali yetu ya kukosa busara. Kuponya magonjwa, kufukuza pepo, na kutenda miujiza ilikuwa sehemu ya kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Neema, lakini sasa tumo katika Enzi ya Ufalme, na kazi kuu ya Mungu sasa ni kukamilisha kila kitu kupitia maneno Yake, kutumia maneno kutasa na kubadilisha tabia za watu wapotovu. Mungu anataka kutugeuza tuwe watu wanaomtii, waaminifu Kwake, wanaomjua, na kumpenda ili aweze kuchukua kikundi cha watu kama hawa katika enzi inayofuata. Kile ambacho Mungu anataka ni upendo na utiifu ambao watu huonyesha kiasili mara tu wamepata kumjua Mungu. Hataki watu wamfuate kwa sababu ya hisia ya shukrani kwa ajili kuponya magonjwa yao. Kama maneno ya Mungu yanavyosema: ‘Watu husadiki kwamba wakati Mungu anapomwokoa mwanadamu Anafanya hivyo kwa kumgusa kwa baraka na neema Zake, ili kwamba waweze kumpa Mungu mioyo yao. Hivyo ni kusema, Yeye kumgusa mwanadamu ni kumwokoa. Aina hii ya wokovu inafanywa kwa kufanya makubaliano. Pale tu ambapo Mungu atampa yeye mara mia ndipo mwanadamu atatiimbele ya jina la Mungu, na kulenga kuwa na mienendo mizuri mbele ya Mungu na kumletea Yeye utukufu. Haya si mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu. Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo katika haya; kama upo, Asingefanya kazi Yake yeye Mwenyewe. Kitambo, mbinu Zake za wokovu zilikuwa kuonyesha upendo na huruma mkuu, kiasi cha kwamba Alijitolea Yake yote kwa Shetani ili naye aweze kuwapata wanadamu wote. Leo haifanani kamwe na kitambo: Wokovu uliopewa leo unatokea wakati wa siku za mwisho, wakati wa uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake; mbinu za wokovu wako si upendo wala huruma, lakini kuadibu na hukumu ili mwanadamu aweze kuokolewa kabisa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu). Kwa hivyo tunapaswa kuchambua na kuelewa jinsi tunavyotiwa moyo na tamaa ya baraka na jinsi uhusiano wetu na Mungu ni wa mabadilishano. Tunapaswa pia kusoma zaidi maneno ya Mungu na kuyatumia maishani mwetu, kukubali hukumu na kuadibu katika maneno ya Mungu, kukubali ushughulikiaji, upogoaji, majaribu, na usafishaji, na kutafuta kupata utakaso na mabadiliko katika tabia zetu potovu. Kama ugonjwa wako utapona limo mikononi mwa Mungu, na tunapaswa kujiwasilisha kwa mipango na mipangilio ya Mungu.”

Kupitia ushirika wa akina dada, nilikuja kuelewa kuwa kufurahia tu neema ya Mungu hakutoshi kubadilisha tabia zetu za kishetani. Ni kwa kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu tu ndipo tunaweza kujiondolea tabia zetu potovu, kurejesha dhamiri na mantiki yetu, na hivyo kupata wokovu wa Mungu na kupatana na mapenzi Yake. Wakristo wote ambao hawakubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho wanaweza kupokea neema nyingi za Mungu, lakini bado wanaishi katika mzunguko wa kutenda na kukiri dhambi. Hii ni kwa sababu tabia zao potovu hazijatakaswa, na kwa hivyo wanasafiri na kujitumia na lengo la kupata baraka na neema za Mungu. Kwa maneno mengine, wanataka kufanya makubaliano na Mungu na, kwa hivyo, hawatapata idhini Yake kamwe. Baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, niliacha kumwomba Mungu aponye ugonjwa wangu na badala yake nikaazimia kabisa kumwamini Mungu na kumwabudu Mungu bila kujali hali yangu ingekuwa nzuri au mbaya namna gani. Nilijitolea kutekeleza wajibu wangu kama mmoja wa viumbe, kufuatilia ukweli na kutafuta kumjua Mungu kwa dhati zaidi, kujiondoa tabia zangu potovu, na kuishi kama mwanadamu wa kweli ili kumridhisha Mungu. Mara tu nilipoanza kuweka yote haya katika vitendo, nilihisi kuachiliwa sana moyoni mwangu na sikuwahi kuhisi kufungwa au kuwazuiliwa na maumivu ya ugonjwa wangu, na sikuwa na hofu kubwa ya kifo tena. Yote niliyotamani yalikuwa kujiwasilisha kabisa kwa Mungu na kutii maagizo na mipango Yake.

Baada ya hapo, niliungana mara kwa mara na ndugu kusoma maneno ya Mungu, kushiriki juu ya ukweli, na kuimba nyimbo za sifa kwa Mungu. Nilihisi kwamba moyo wangu ulikuwa umejazwa sana, na kwa ujazo huu nilipata upungufu katika mateso yangu. La ajabu zaidi ni kwamba, karibu bila kugundua, hisia ya kufa ganzi iliyokuwa miguuni mwangu ilianza kufifia na taratibu nikaanza kupata tena uwezo wa kutembea, mwishowe sikutegemea kiti cha magurudumu hata kidogo. Kitu ambacho hakikutarajiwa kabisa ni kwamba siku moja hisia yangu ilirudi ghafla na niliweza kuona maneno yaliyochapishwa kwenye vitabu vya maneno ya Mungu. Mwishowe niliweza kuona maneno ya Mungu! Sikuweza kuamini, lakini kwa kweli nilikuwa nimeona muujiza. Furaha ambayo nilihisi moyoni mwangu ilikuwa kitu kisichoweza kuelezeka, na kwa hivyo nilimwomba Mungu bila kukoma, nikimshukuru na kumsifu. Nilipomwambia mume wangu habari hiyo njema, alibubujikuwa na hisia. Akiwa na machozi machoni mwake, alilia tena na tena, “Asante Mungu, asante Mungu!” Ndiyo, ni kweli—nilijiwasilisha kwa Mungu kidogo tu na Mungu akanipa baraka hii kuu. Nilihisi sana jinsi hata ingawa kazi ya Mungu ya siku za mwisho haijumuishi kutenda miujiza, mamlaka ya maneno ya Mungu yanazidi mamlaka ya miujiza ya Mungu kwa mbali. Kwa kweli Mungu ndiye mwenyezi Mungu, Mungu anayewapenda watu!

Siku moja, mume wangu alikuwa katika hospitali ya jimbo na akakutana na daktari ambaye alikuwa na jukumu la msingi la kunitibu. Daktari alimuuliza jinsi matibabu ya ugonjwa wa figo yangu yanaendelea na ikiwa matibabu ya usafishaji wa damu kwa mashine ya figo ulikuwa unatumiwa. Mume wangu alijibu: “Hakufanyiwa usafishaji wa damu kwa mashine ya figo lakini hali yake tayari imeimarika. Anaweza kutembea sasa, na pia anaweza kuona!” Daktari alishangaa sana, akasema: “Naam, huo ni muujiza. Nilidhani kwamba tayari alikuwa akifanyiwa usafishaji wa damu kwa mashine ya figo kwa muda sasa.”

Siku hizi ninaishi maisha ya kawaida. Ndugu, marafiki, na majirani zangu daima huonyesha mshangao na kusema vitu kama: “Sikuwahi kufikiria kuwa hali yako ingeimarika haraka sana. Kimwili na kiakili unaonekana kama mtu wa kawaida!” Kila wakati ninaposikia kitu kama hiki ninasema maneno machache ya shukrani kwa Mungu kimoyomoyo: “Mungu, sitasahau kamwe maishani mwangu mwote upendo ambao umenionyesha na wokovu Wako. Ingawa hakuna kitu ninachoweza kukufanyia, ninaazimia kukufuata, kukuabudu na kutekeleza wajibu wangu kama mmoja wa viumbe Wako maisha yangu yote ili nilipe upendo Wako.” Nilikuwa nimepotoshwa sana, mwanzoni sikuwa nimeutambua uwepo wa Mungu, na muda baada ya muda nilikataa wokovu wa Mungu, lakini si tu kwamba Mungu hakuwa na kisasi juu ya makosa yangu lakini aliniokoa kwa njia kubwa sana. Nimepata rehema kubwa za Mungu, na najua kwamba sistahili kabisa neema kama hiyo. Matukio haya ya nguvu na ya kudumu yamenionyesha kuwa sayansi na maarifa haviwezi kuwaokoa wanadamu, lakini itawaletea watu mateso na hofu isiyo na mwishi, na kifo. Ni Muumba na Mtawala wa kila kitu ulimwenguni ndiye anayeweza kuwapa wanadamu uzima na riziki wanayohitaji. Mungu ndiye msingi wa pekee wa kuwepo kwa wanadamu, na ndiye tumaini la pekee la wokovu na ukombozi wa wanadamu. Tumaini la pekee la watu kupata hatima nzuri ni kumwabudu Mungu. Ninamshukuru Mungu kwa kuniokoa—mtu ambaye alifumbwa macho na Shetani na alikuwa karibu kufa—kutokana na ushawishi wa Shetani. Mungu alinirudisha kwenye uzima na akanirudisha mbele Zake, Muumba wa vitu vyote. Mimi sasa naitembea njia ing’aayo ya uzima!

Iliyotangulia: 45. Kurejea Kutoka Ukingoni

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

44. Nimerudi Nyumbani

Na Chu Keen Pong, MalasiaNilimwamini Bwana kwa zaidi ya muongo mmoja na kuhudumu kanisani kwa miaka miwili, na kisha nikaliacha kanisa...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp