3. Kufichua Fumbo la Hukumu

Na Enhui, Malasia

Jina langu ni Enhui; nina umri wa miaka 46. Ninaishi Malaysia, nami nimekuwa mwumini katika Bwana kwa miaka 27. Mnamo Oktoba 2015, nilihamia jiji lingine ili kuanza kazi. Wenzangu wageni walikuwa wamejiingiza katika mtandao wa Facebook, walioutumia kwa kuongea, kupata marafiki wapya, na kufanya matangazo. Walipoona kwamba sikuwa na akaunti ya mtandao wa Facebook walinianzishia yangu, na polepole nilijifunza jinsi ya kwenda mtandaoni na kuutumia. Nilipokuwa na wakati, ningetazama matangazo ya baadhi ya ndugu katika Bwana na ningezishiriki na kuzipenda. Mara nyingine ningefanya matangazo kadhaa kuhusu kumsifu Bwana au kushiriki neema ya Bwana pamoja na watu katika kikundi cha rafiki zangu. Kila siku ilikuwa kamilifu kwangu.

Siku moja mnamo Februari 2016 wakati nilipokuwa nikipitia maelezo mafupi ya mmoja wa rafiki zangu wa mtandao wa Facebook, niliona tangazo hili: “Tulijadili suala la hukumu leo katika kikundi chetu. Sote tulisema mambo tofauti lakini tuliakubaliana kuhusu hoja kuu. Mmoja wao alisema: ‘Ikiwa sielewi jambo, siwezi kuthubutu kufoka upuuzi—ni kitu ambacho Mungu atafanya katika siku zijazo na hatupaswi kujaribu kuwa na makisio yasiyowezekana.’ Mtu mwingine alisema: ‘Zaburi 75:2 inasema “Nitakapoupokea mkusanyiko nitahukumu kwa unyofu.” Mungu huzingatia kila kitu ambacho kila mtu hufanya, kwa hivyo Bwana Yesu atakaporejea kuwahukumu wanadamu wote Atafichua matendo yetu kwa watu wote, kama vile kucheza sinema. Kwa hivyo tunapaswa kuwa waaminifu daima katika tabia zetu na hatupaswi kamwe kutenda maovu ili Mungu asituhukumu na kisha Atutupe katika kuzimu.’ Mtu mwingine alisema: ‘Biblia inasema: “Na nikaona kiti kikubwa cha enzi, cheupe, na yeye akiketiye, ambaye kutoka kwa uso wake nchi na mbingu zilitoroka; na hapakupatikana mahali pao. Na nikawaona waliokufa, wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya Mungu; na vitabu vilifunguliwa: na kitabu kingine pia kikafunguliwa, ambacho ni kitabu cha uhai: na waliokufa walihukumiwa kwa mambo yale yaliyokuwa yameandikwa katika vitabu hivyo, kulingana na vitendo vyao(Ufunuo 20:11–12). Kutoka kwa maandiko tunaweza kuona kwamba Bwana Yesu atakaporudi katika siku za mwisho Atatayarisha dawati kubwa mbinguni, Aketi nyuma yake, na kufungua vitabu. Halafu, wanadamu wote wakiwa wamepiga magoti, Ataliita jina la kila mtu na kumhukumu kila mmoja wao kulingana na matendo yake. Watu wazuri watachukuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni na Bwana, ilhali waovu watatupwa katika kuzimu.’”

Baada ya kusoma tangazo hili niliendelea kuketi kwenye kiti changu, na kuchora picha akilini ya Bwana Yesu akiwahukumu wanadamu: Bwana akiwa Ameketi kwenye kiti cha enzi, watu wote wakiwa wamepiga magoti mbele ya dawati Lake wakieleza waziwazi kuhusu dhambi zao zote ili Mungu atoe hukumu, na Bwana akipeleka kila mmoja wao mbinguni au kuzimuni kulingana na matendo yake. Nilifikiria jinsi ambavyo nilikuwa mfuasi mwaminifu wa Bwana kwa zaidi ya miaka 20 na nilivyojaribu kadri ya uwezo wangu kutia mafundisho Yake katika vitendo. Niliamini kwamba Bwana angeona uchaji wangu na kunichukua hadi katika ufalme wa mbinguni. Lakini nilipowaza kuhusu jambo hilo zaidi na zaidi, ghafla wazo lilinijia: Sasa kwa kuwa nilijua jinsi ya kutumia Mtandao kwa nini nisifanye utafiti kuhusu “hukumu” kisha nione kitakachojitokeza? Nilifungua kivinjari na kupiga chapa hilo neno; siwezi kukumbuka ni kiunga kipi nilichobofya lakini kwa mshangao wangu, sentensi hii iliibuka: “Kuadibu na Kuhukumu kwa Mungu Ndiko Mwanga wa Wokovu wa Mwanadamu.” Hii ilichochea ari yangu ghafla, na hivyo nikafungua tovuti hiyo ili nisome zaidi. Wakati ukurasa wa tovuti ilipokuwa ikifunguka nilisikia wimbo uliokuwa wa furahisha na wa kuchochea mawazo: “Kuadibu na Kuhukumu kwa Mungu Ndiko Mwanga wa Wokovu wa Mwanadamu.” Maneno ya wimbo yalihusisha: “… Katika maisha yake, kama mwanadamu anatamani kutakaswa na kufikia mabadiliko katika tabia yake, kama anatamani kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana, na kutimiza wajibu wake kama kiumbe, basi lazima akubali adabu na hukumu ya Mungu, na lazima asiruhusu nidhamu ya Mungu na kipigo cha Mungu kiondoke kwake, ili aweze kujiweka huru kutokana na kutawalwa na ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa Mungu. Ujue kwamba adabu ya Mungu na hukumu ni mwanga, na mwanga wa wokovu wa mwanadamu, na kwamba hakuna baraka bora zaidi, neema au ulinzi bora kwa ajili ya mwanadamu(Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya).

Nilitafakari maneno hayo baada ya wimbo kuisha; niliuona kuwa wa kusisimua. Nilianza kuwaza: “Je, kuadibu na hukumu ya Mungu ndiyo nuru ya wokovu wetu? Je, ni kinga na neema kuu ya wanadamu? Tunaweza kuelewa jambo hili kwa namna gani? Ikiwa watu wanataka kutakaswa na kuishi maisha yenye maana, hiyo inamaanisha kwamba wanapaswa kukubali kuadibu na hukumu ya Mungu?” Nilipokuwa nikiwaza kuhusu maneno ya wimbo huu, maswali mengi yalizunguka akilini mwangu. Niliwaza pia: “Ikiwa Mungu angemhukumu mwanadamu, mwanadamu asingelaaniwa? Na hukumu inakujaje kuwa nuru ya wokovu?” Nilikuwa na hamu na kusisimka kwa sababu sikuwa nimewahi kusikia jambo kama hili hapo awali. Ingawa hukumu iliyozungumziwa kwenye wimbo haikuwa jinsi nilivyoelewa hukumu kuwa, bado nilikuwa na hisia hii tatanishi kuwa hukumu ina umuhimu wenye kina sana, na inafaa kwa hatima na majaliwa ya kila mtu. Nilipochunguza asili ya wimbo huo niliona kwamba ulitoka kwenye Kanisa la Mwenyezi Mungu, kwa hivo nikaenda kwenye tovuti yao. Niliona kuwa riwaya ya ukurasa wa kwanza haikuwa yenye mawazo mapya na ya kupendeza tu, lakini maudhui pia yalikuwa yenye thamani na yenye tofauti nyingi. Kulikuwa na mambo ya kusikiliza, mambo ya kusoma, nyimbo, majadiliano na mambo mengine mengi. Niliwaza: “Mbona hakuna mtu aliyewahi kuniambia kuhusu tovuti hii? Ni nzuri sana, lakini inawezekana kuwa hakuna mtu aliyeishiriki kwa sababu bado hajaiona?” Nilibofya kiunga cha “Vitabu” na nilipokuwa nikiibingiriza orodha hiyo niliona kichwa hiki: Ushuhuda Wa Uzoefu Katika Kuingia Katika Maisha. Nilipokibofya, niliona kwamba zilikuwa shuhuda hasa kuhusu hukumu ya Mungu, kwa mfano: “Hukumu na Kuadibu kwa Mungu Kuliniokoa,” “Hukumu na Kuadibu kwa Mungu Kulikuwa Wokovu Mkubwa Kwangu,” “Niliona Upendo wa Mungu Katika Hukumu na Kuadibu Kwake,” “Hukumu na Kuadibu kwa Mungu Vilisisimua Moyo Wangu Wenye Dhambi,” “Hukumu ya Mungu na Kuadibu Kuliniweka Kwenye Njia Sahihi.” Ilikuwa inakaribia wakati wangu wa kwenda kazini, kwa hiyo nilikuwa tu na wakati wa kusoma kwa haraka baadhi ya shuhuda hizi. Zote zilikuwa zimeandikwa na waumini waliokuwa wakieleza jinsi tabia zao potovu zilivyotakaswa, na pia kuongea kuhusu upungufu, upotovu, maoni yao yasiyofaa katika imani, nk., na jinsi mambo haya yalivyobadilishwa kwa namna fulani kupitia maneno ya hukumu ya Mwenyezi Mungu. Hii ilinifanya nivutiwe zaidi kuhusu “Kuadibu na Kuhukumu kwa Mungu Ndiko Mwanga wa Wokovu wa Mwanadamu.” Inawezekana kuwa hukumu haikuwa kuhusu kulaaniwa? Kwamba haikuwa kuhusu kuamua hatima wa kila mtu? Nilianza kuwa na wasiwasi sana, nami nilijua ilikuwa ni lazima nifichue “Kuadibu na Kuhukumu kwa Mungu Ndiko Mwanga wa Wokovu wa Mwanadamu” ilikuwa inazungumzia nini. Nilifikia uamuzi kuwa Ushuhuda Wa Uzoefu Katika Kuingia Katika Maisha labda kilikuwa kitabu muhimu sana kwa ajili ya watu katika imani yao, na kwamba ninapaswa kukiangalia vizuri. Lakini wakati ulikuwa unayoyoma, kwa hivyo niliizima kompyuta yangu na kwenda kazini.

Usiku huo nilikuwa nikikugeuka-geuka kitandani, nisiweze kulala; picha za tovuti ya Kanisa la Mwenyezi Mungu ziliendelea kuibuka kichwani mwangu. Hasa sikuweza kuelewa sentensi “Kuadibu na Kuhukumu kwa Mungu Ndiko Mwanga wa Wokovu wa Mwanadamu,” nami nilitaka sana kujua maana ya “hukumu” hiyo.

Niliamka mapema asubuhi iliyofuata, nikafungua tovuti ya Kanisa la Mwenyezi Mungu na kuanza kutafuta neno “hukumu.” Niliona nakala yenye kichwa “Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli,” niliifungua, na kusoma maneno haya: “‘Hukumu’ katika maneno yaliyonenwa awali—hukumu itaanza na nyumba ya Mungu—inarejelea hukumu ambayo Mungu anatoa leo kwa wale wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi katika siku za mwisho. Pengine kuna wale wanaoamini katika mawazo ya kimiujiza kama yale, siku za mwisho zitakapowadia, Mungu ataandaa meza kubwa mbinguni, ambako kitambaa cheupe kitatandikwa, kisha, Mungu ataketi kwenye kiti kikuu cha enzi na wanadamu wote wakipiga magoti ardhini, Atafichua dhambi za kila mwanadamu na hivyo kubainisha iwapo atapaa juu mbinguni ama atatupwa chini kwenye ziwa la moto wa jehanamu. Haijalishi mawazo ya mwanadamu yalivyo, kiini cha kazi ya Mungu hakiwezi kubadilishwa. Mawazo ya mwanadamu ni miundo ya fikra za mwanadamu tu na yanatoka kwenye ubongo wa mwanadamu, na yametungwa na kuunganishwa kutokana na mambo aliyoyaona na kuyasikia. Kwa hivyo Nasema, kwa vyovyote vile hata picha zilizowazwa ziwe za hali ya juu kiasi gani, bado ni kama mchoro tu na haziwezi kubadilishwa na mpango wa kazi ya Mungu. Hata hivyo, mwanadamu amepotoshwa na Shetani, sasa atawezaje kuyaelewa mawazo ya Mungu? Mwanadamu huiona kazi ya hukumu ya Mungu kuwa ya ajabu mno. Mwanadamu anaamini kwamba kwa sababu ni Mungu Mwenyewe anayefanya kazi ya kuhukumu, basi lazima iwe ni ya kiwango cha juu zaidi na isiyoeleweka kwa wanadamu wenye mwili wa kufa, na lazima inasikika katika mbingu yote na kutetemesha dunia; vinginevyo itakuwaje kazi ya hukumu ya Mungu? Mwanadamu anaamini kuwa, kwa maana hii ni kazi ya hukumu, basi lazima Mungu ni wa kuvutia na mwenye uadhama Anapofanya kazi, na wale wanaohukumiwa lazima wawe wanalia kwa sauti wakitoa machozi wakiwa kwenye magoti wakiomba msamaha. Onyesho hili lazima ni la kustaajabisha sana na la kusisimua mno…. Kila mtu hudhani kazi ya hukumu ya Mungu kuwa ya u isiyo ya kawaida. Je, unajua, hata hivyo, kwamba Mungu alianza kazi ya kuhukumu miongoni mwa wanadamu kitambo sana na wakati huu wote wewe bado uko katika hali ya kutotambua? Kwamba, wakati ambao unadhani kuwa kazi ya hukumu ya Mungu inaanza rasmi, tayari umewadia wakati ambapo Mungu kuzifanya upya mbingu na nchi? Wakati huo, pengine utakuwa tu umeelewa maana ya maisha, lakini kazi ya adhabu ya Mungu isiyo na huruma itakuleta kuzimu, ukiwa bado usingizini. Hapo tu ndipo kwa ghafla utafahamu kuwa kazi ya hukumu ya Mungu itakuwa imeshahitimika.” Nilishangazwa sana na maneno haya. Yalifichua kwa usahihi mawazo ya ndani kabisa na maoni ya binadamu kuhusu kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho—pia yalikuwa halisi kabisa na yenye manufaa. Nilijiuliza, “Inawezekana kuwa dhana ya hukumu mbinguni ambayo nilikuwa nikishikilia ilikuwa wazo langu tu? Kifungu hiki kinaonyesha kuwa watu hufikiri kazi ya hukumu ya Mungu kuwa ya ajabu na ya miujiza. Inaonyesha pia kwamba kazi ya hukumu ilianza zamani sana na hivi karibuni itahitimishwa, na kinawahimiza watu kutopoteza wakati kutafuta dhihirisho la Mungu. Hiyo inaweza kuwa sauti ya Mungu?” Wazo hilo liliniacha nikiwa na wasiwasi na kwa kweli nilitaka ufafanuzi wa haraka kuhusu maana ya hukumu ya Mungu. Lakini kulikuwa na mambo mengi sana kwenye tovuti ya Kanisa la Mwenyezi Mungu na wakati huo sikujua nianzie wapi kutafuta, kwa hivyo niliamua kuwatafuta washiriki wa kanisa hilo wenyewe na kuona ikiwa wangeweza kunisaidia kuelewa mambo.

Nikitumia mazungumzo mitandaoni kwenye tovuti ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, nilituma ujumbe nikiwaambia kuwa nilikuwa na hamu ya kujifunza zaidi kuhusu hukumu. Mtu alinijibu haraka sana, na kuwatambulisha dada wawili kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu ambao waliungana nami kwenye mtandao: Liu Hui na Li Mei. Kwa kipindi chote cha kushauriana, niligundua kuwa dada hawa wawili walikuwa na mtazamo ulio wazi na wa uaminifu, na walikuwa waziwazi kabisa; nilitaka kuzungumza nao kuhusu mambo yaliyo moyoni mwangu. Niliwaambia: “Ninapenda sana tovuti ya Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kuna kila aina ya vitabu vya kiroho, nyimbo za sifa, video za muziki, sinema za injili, masimulizi ya neno la Mungu, na zaidi. Kwa kweli kuna maudhui mengi, lakini sielewi maana ya hukumu ya Mungu. Nilisoma tu ‘Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli’ ambayo inaonekana kusema kuwa kazi ya hukumu ya Mungu imekwishaanza na kwamba wazo la hukumu mbinguni ni matokeo tu ya mawazo na fikra za binadamu. Hii ni tofauti kabisa na kuelewa kwangu kwa kawaida kuhusu hukumu. Mnaweza kushiriki nami mnavyofahamu kuhusu jambo hili?”

Dada Liu Hui alijibu: “Asifiwe Mungu! Hebu tutafute na kushiriki pamoja! Nilikuwa nikiwaza hivyo pia, nikiamini kwamba kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho ingetekelezwa juu mbinguni. Lakini baada ya kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu na kushiriki na ndugu nilikuja kugundua kuwa kwa kweli hii ilikuwa wazo langu mwenyewe, fikra yangu mwenyewe. Iwapo kazi ya Mungu ya hukumu itafanywa mbinguni au duniani imesemwa waziwazi katika baadhi ya unabii katika Biblia. Kwa mfano, Ufunuo 14:6-7 inasema: ‘Na nikamwona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu, akiwa na injili ya daima kuwahubiria hao wanaoishi katika ulimwengu, na kwa kila taifa, na ukoo, na lugha, na watu, Akisema kwa sauti kuu, Mwogopeni Mungu, na kumpa utukufu; kwa kuwa saa ya hukumu yake imekuja: na mumsujudie yule aliyeziumba mbingu, na ulimwengu, na bahari, na chemchemi za maji.’ Katika Zaburi 96:13 inasema: ‘Kwa kuwa anafika, kwa kuwa anafika kuihukumu dunia: ataihukumu dunia kwa haki, na watu kwa ukweli wake’ Katika Yohana 9:39 inasema: ‘Kwa hukumu nimekuja duniani humu, ili wale wasioona waweze kuona.’ Katika aya hizi za kibiblia inataja ‘akiwa na injili ya daima kuwahubiria hao wanaoishi katika ulimwengu,’ ‘kwa kuwa anafika, kwa kuwa anafika kuihukumu dunia’ na ‘Kwa hukumu nimekuja duniani humu.’ Kutoka kwa hili tunaweza kuona kwamba katika siku za mwisho, lazima Mungu mwenyewe Aje ulimwenguni, naye Atakuja duniani kufanya kazi ya hukumu, kuwahukumu watu wote na mataifa yote. Zaidi ya hayo, kutokana na kusoma Biblia tunajua kuwa kabla ya Mungu kuwaumba wanadamu Aliumba mbingu na ardhi na vitu vyote ili kutayarisha mazingira bora ya kuishi kwa ajili yetu. Kisha Mungu aliwaumba wanadamu na kupanga tuishi duniani, si mbinguni. Kwa hiyo tunawezaje kupanda juu mbinguni? Wanadamu waovu hawana chaguo ila kukubali hukumu ya Mungu hapa duniani. Pia, imeandikwa katika Kitabu cha Ufunuo kwamba Yohana aliona kiti kikubwa cha enzi cheupe angani kwenye kisiwa cha Patmo. Kwa kweli, hii ilikuwa tu moja kati ya maono ya Yohana, lakini watu wengine wametafsiri maono haya kumaanisha kuwa Mungu atakaporudi katika siku za mwisho Atawahukumu watu angani. Haya ni mawazo na fikra zetu wenyewe tu, nayo ni ufafanuzi usiofaa wa unabii huo—si ukweli wa kazi ya Mungu hata kidogo.”

Nilishangazwa na kile nilichosikia: nilikuwa nimesoma vifungu vyote vya Biblia ambavyo dada huyo alikuwa akishiriki nami, kwa hiyo ilikuwaje kwamba sikuwahi kugundua maana ya maneno hayo? Naam! Mungu alikuwa Amewaumba wanadamu ili waishi duniani, kwa hiyo ingewezekanaje sisi kwenda mbinguni? Kwa kweli imani yangu ilikuwa imejaa mashaka na ujinga!

Kisha Dada Li Mei alishiriki jambo hili nami: “Katika siku za mwisho Mungu hajakuwa mwili tu ili Afanye kazi ya hukumu hapa duniani, lakini kazi Yake ilianza zamani sana na hivi karibuni itakamilika. Kazi ya Mungu ya hukumu haifanywi mbinguni kama watu wanavyofikiri, na si kuwalaani watu moja kwa moja kama wanavyoamini. Kwa kweli, kabla ya kazi ya Mungu ya hukumu kukamilika, wale wote wanaokuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu ni wale ambao wanaweza kuhukumiwa, kujaribiwa na kutakaswa kwa maneno ya Mungu. Wote wote wanaokubali hukumu ya Mungu na kutakaswa watachukuliwa na Mungu na kuingia katika ufalme Wake. Lakini kwa wale ambao wanakataa kukubali hukumu ya maneno ya Mungu, kwa kuwa asili zao za dhambi hazitakuwa zimehukumiwa na kutakaswa na Mungu, wataendelea kuishi katika dhambi, wakiendelea kutenda dhambi kila wakati. Watasema uwongo, wadanganye, wamuasi Mungu na kumpinga Mungu. Wataangamizwa katika kuzimu kwa sababu ya dhambi zao—hili ni dhihirisho la kweli la tabia ya haki ya Mungu. Wale kati yetu ambao tumemfuata Bwana kwa miaka mingi na kupata uzoefu wa kina kuhusu hayo ingawa tumekombolewa kutokana na dhambi zetu kwa sababu ya imani yetu, shida ya asili yetu ya dhambi haijatatuliwa. Tunamfuata Bwana, lakini wakati uo huo sisi huenda kinyume na mafundisho ya Bwana na badala yake tunazipa uhuru tamaa zetu za mwili kutenda dhambi kama vile kusema uwongo, kudanganya, kujiingiza katika kula njama, na kupigania umaarufu na utajiri. Tunatamani ubatili mtupu na kufuatilia mienendo mibaya wa ulimwengu halisi. Na kadhalika. Hasa wakati tunakabiliwa na majaribu, ajali, na misiba, tunammwelewa Mungu vibaya, tunamlaumu na hata kumsaliti. Tunaweza kusema kuwa tunaishi katika hali ya kutenda dhambi na kisha kuungama dhambi zetu daima, lakini tusiikung’ute kamwe minyororo ya asili yetu ya dhambi. Katika Biblia inasema: ‘Fuata amani na watu wote, na utakatifu, bila huu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana’ (Waebrania 12:14). Watu ambao ni waovu kama sisi tulivyo wanawezaje kuingia katika ufalme wa Mungu? Mwenyezi Mungu alisema: ‘Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati namna hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho). Kwa hivyo, katika siku za mwisho, Mungu anatekeleza mpango Wake wa usimamizi, Akitekeleza hatua ya kazi ya kuhukumu, kuadibu, na kuwatakasa watu kulingana na kile wanadamu wapotovu wanahitaji. Kusudi ni kutuokoa kabisa kutoka kwa miliki ya Shetani, na kuondoa minyororo ya asili yetu ya dhambi ili tuweze kutakaswa na kuokolewa. Kutokana na jambo hili tunaweza kuona kwamba kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho inahusu utakaso na wokovu. Si kuhusu kutulaani, kama watu wanavyodhani.”

Dada Liu Hui aliendelea kushiriki nami: “Hiyo ni kweli, Dada Enhui. Hebu tufikirie kuhusu jambo hilo, ikiwa kazi ya Mungu ya hukumu ilikuwa kutulaani na kutuadhibu, basi hakuna hata mmoja kati yetu, wote ambao wamepotoshwa kwa kina na Shetani, angewahi kuokolewa au kuweza kuingia katika ufalme wa Mungu. Kama ingekuwa hivyo, msingi wa kazi ya Mungu ya hukumu ungekuwa nini? Maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema wazi kwa nini Mungu hufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, na umuhimu wake ni nini. Hebu tusome vifungu viwili vya maneno ya Mwenyezi Mungu: ‘Maisha yote ya mwanadamu yamekuwa chini ya himaya ya Shetani, na hakuna mtu yeyote anayeweza kujitoa kutoka katika ushawishi wa Shetani yeye mwenyewe. Wote wanaishi katika dunia chafu, kwa upotovu na utupu, bila maana yoyote au thamani; wanaishi maisha ya kutojali kwa ajili ya mwili, tamaa, na kwa ajili ya Shetani. Hakuna maana yoyote kwa kuwepo kwao. Mwanadamu hana uwezo wa kupata ukweli utakaomweka huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Ingawa mwanadamu anaamini katika Mungu na anasoma Biblia haelewi jinsi ya kujitoa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kutoka kitambo, watu wachache sana wametambua siri hii, wachache sana wameielewa. … Mwanadamu asipotakaswa, basi yeye ni wa uchafu; asipolindwa na kutunzwa na Mungu, basi yeye bado ni mfungwa wa Shetani; asipohukumiwa na kuadibiwa, basi hatakuwa na njia ya kuepuka ukandamizaji na ushawishi mbaya wa Shetani. Tabia potovu unayoonyesha, na tabia ya uasi unayoishi kwa kudhihirisha inatosha kuonyesha kwamba bado unaishi katika himaya ya Shetani. Kama akili na mawazo yako hayajatakaswa, na tabia yako haijahukumiwa na kuadibiwa, basi nafsi yako yote bado inadhibitiwa na himaya ya Shetani, akili yako bado inadhibitiwa na Shetani, mawazo yako yanatawaliwa na Shetani, na nafsi yako yote inadhibitiwa na mikono ya Shetani(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu). ‘Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). Kwa hivyo tunaweza kuona nini kutoka kwa maneno ya Mungu? Tukiyaangalia kutoka upande mmoja, tunaweza kuona kwamba maneno ya Mungu ni yenye manufaa sana nayo yanaonyesha kabisa hali yetu ya maisha halisi. Kutoka upande mwingine, tunaweza kuona kwamba lazima kwanza tupitie hukumu na utakaso wa Mungu ili tujiondolee uchafu na upotovu, na kuutoroka ushawishi wa giza wa Shetani. Ni wakati huo tu ndipo tutakapostahili kuchukuliwa na Mungu katika ufalme Wake. Bila kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho hatungeweza kusafishwa vya kutosha ili tuwe watu wanaoupendeza moyo wa Mungu, na hakika hatungeweza kuingia katika ufalme wa Mungu. Hatungeweza kuacha kutenda dhambi na kumpinga Mungu kamwe, na mwishowe, tungeangamizwa na Mungu katika kuzimu. Kwa kweli, kutokana na shuhuda za kweli za ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu tunaweza kuona kwamba hukumu na kuadibu kwa Mungu ni taa ya wokovu kwa wanadamu. Kila mmoja wetu amepotoshwa na Shetani, lakini kwa sababu tunaweza kuja mbele za Mwenyezi Mungu na kupokea hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, tabia yetu ya maisha hubadilika pole pole. Tunabadilika kutoka uasi na kupinga hadi kukubalika na utii; tunabadilika kutoka kiburi, kujihesabia haki na kutokubali kishindwa na mtu yeyote, hadi kuwa tayari kuweka kando ubinafsi wetu wenyewe na kutii kilicho sawa, tukiutii ukweli. Zaidi ya hayo, yote ambayo yameonyeshwa katika hukumu na kuadibu kwa Mungu ni ukweli, na pia ni maonyesho ya tabia ya Mungu iliyo yenye haki na takatifu, kwa hiyo kadri tunavyozidi kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, ndivyo tunavyozidi kumjua Mungu. Na kadri tunavyozidi kumjua Mungu, ndivyo tunavyozidi kuweza kuona wazi ukweli kuhusu watu, vitu, na matukio katika ulimwengu. Ipasavyo, maoni na maadili yetu yanabadilika kwa viwango tofauti. Tunapata uchaji zaidi na utii kwa Mungu. Hiki ndicho hukumu na kuadibu kwa Mwenyezi Mungu kinachofanikisha ndani yetu. Bila hukumu ya nuru ya ukweli katika maneno ya Mungu, sote tungeishi gizani, tukitenda dhambi na na kisha kuziungama, kuziungama na kisha kuzitenda tena kila siku, tusiikung’ute kamwe minyororo ya dhambi. Basi tungewezaje kuchukuliwa na Mungu na kuingia katika ufalme wake?”

Baada ya kushiriki na Dada Li na Liu nilihisi kana kwamba mwanga wenye kung’aa ulikuwa umewashwa moyoni mwangu. Walichosema kilikuwa kweli: Mchungaji, wazee, na ndugu katika kanisa langu wote hawakuweza kujinasua kutoka katika utumwa wa dhambi. Mimi mwenyewe pia nilitenda dhambi mara nyingi ingawa sikutarajia kufanya hivyo na sikuweza kuyatia maneno ya Bwana katika vitendo. Sote tunaishi katika hali ya kutenda dhambi na kisha kuungama—kwa kweli tunahitaji Mungu arudi na kufanya hatua ya kazi ya hukumu na kutakasa. Kama nisingeichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho nisingeweza kuelewa ukweli huu. Nilimshukuru Mungu sana kwa mwongozo Wake. Kwa kuyasoma maneno ya Mwenyezi Mungu na kusikiliza ushirika wa akina dada hao, pamoja na kusoma shuhuda zilizoandikwa za ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu wakielezea jinsi tabia zao potovu zilivyotakaswa kupitia hukumu ya maneno ya Mungu, nilikuwa nimepata ufahamu kidogo kuhusu kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho. Mawazo yangu mwenyewe yalikuwa yameondolewa, na sasa nilijua kuwa hukumu na kuadibu kwa Mungu ni muhimu kwetu ili kuiepuka dhambi na kupata utakaso.

Kisha Liu Hui alisema: “Hebu tusome vifungu viwili zaidi vya maneno ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu alisema: ‘Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli). ‘Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele). Kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu inaweza kuonekana kwamba katika siku za mwisho Mungu amekuwa mwili ili kuonyesha ukweli wote wa kuwatakasa na kuwaokoa binadamu, kulingana na mahitaji ya wanadamu. Yeye hufichua tabia ya Mungu yenye haki ya Mungu ambayo haitavumilia kosa kwa wanadamu. Kupitia maneno Yake, Mungu huonyesha asili na kiini cha watu, na hali halisi ya upotovu wao. Ni kupitia tu kuyakubali maneno ya hukumu ambayo Mwenyezi Mungu ameonyesha ndipo tunaweza kujua kiburi chetu, ujanja, ubinafsi, ubaya wetu wenyewe, n.k., ambavyo vyote ni sehemu ya asili yetu ya kishetani na tabia potovu. Ni kupitia tu kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu ndipo tunaweza kujua hali ya haki ya Mungu na kukuza mioyo ya kumcha Mungu na toba ya kweli. Kwa hivyo tunaweza kupata mabadiliko na utakaso wa tabia yetu potovu. Huu ndio umuhimu wa hukumu ya Mungu, na pia ni njia yetu ya pekee ya kupata wokovu. Dada Enhui, maadamu tunasoma maneno mengi ya Mwenyezi Mungu kwa bidii kadri tuwezavyo, basi umuhimu wa kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho utakuwa wazi kwetu na hata zaidi, tutaona kuwa ni Kristo wa mwisho pekee ndiye Anayeweza kutoa njia ya uzima wa milele juu ya watu.”

Bwana asifiwe! Nilipata kiasi kikubwa kutoka kwa kuzungumza na akina dada hao. Ingawa bado sijapitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, kupitia kushiriki nao na kusoma Ushuhuda Wa Uzoefu Katika Kuingia Katika Maisha, nimehisi kuwa hukumu na kuadibu kwa Mwenyezi Mungu kunaweza kubadilisha watu kwa kweli. Ninahisi pia kuwa ninamhitaji Mungu sana ili Aitekeleze hatua Yake ya kazi ya hukumu na kuadibu ili Anibadilishe na kunitakasa ili nistahili kuchukuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni. Baadaye, baada ya siku kadhaa zaidi za ushirika, nilikuja kuelewa zaidi kuhusu umuhimu wa kazi ya Mungu ya hukumu na ukweli kuhusu majina ya Mungu. Pia nilijifunza ukweli ili nimtambue Kristo wa kweli kutoka kwa wale wa uwongo, na makanisa halisi kutoka kwa yale ya uwongo. Nilijifunza ukweli kuhusu kupata mwili kwa Mungu, tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu, jinsi Shetani huwapotosha wanadamu, jinsi Mungu anavyotuokoa, na zaidi. Nilifikia hitimisho thabiti kuwa Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerejea, nami niliikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho kwa moyo wenye furaha. Mungu asifiwe! Tangu wakati huo nilikuwa na kiu isiyotulizika ya kusoma maneno ya Mungu. Kwa kuishi maisha ya kanisa, kushiriki ukweli pamoja na ndugu, na kukubali kunyunyizia na kula maneno ya Mungu ninahisi kuwa roho yangu inapata mlo mkubwa. Jambo hili limeniwezesha kushuhudia utimilifu kamili wa unabii huu katika Kitabu cha Ufunuo katika Biblia: “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi(Ufunuo 3:20). Nimehisi pia likitimizwa ndani yangu kibinafsi. Maneno ya Mwenyezi Mungu yameufungua mlango wa moyo wangu na kuniwezesha kuisikia sauti ya Mungu, kujua kazi ya hukumu ya Mungu, na kurudi mbele Zake. Asifiwe Mungu!

Iliyotangulia: 2. Njia ya Utakaso

Inayofuata: 4. Mwamko wa Roho Aliyedanganywa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp