125 Mungu Ametukuzwa Kikamilifu

1 Yesu Alikuwa duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, Alikuja kufanya kazi ya usulubisho na kupitia usulubisho, Mungu Alipata sehemu moja ya utukufu. Mungu Alipokuja katika mwili, Aliweza kunyenyekea na kujificha, na Aliweza kustahimili mateso makubwa. Japokuwa Alikuwa Mungu Mwenyewe, bado Alipitia kila aina ya fedheha, na kila aina ya matusi, na Alipitia uchungu mkubwa kwa kuangikwa msalabani ili kukamilisha kazi ya ukombozi. Baada ya hatua hii ya kazi kutamatishwa, japokuwa watu waliona kuwa Mungu Alikuwa Amepata utukufu mkubwa, huu haukuwa ukamilifu wa utukufu Wake; ilikuwa tu sehemu moja ya utukufu Wake ambao Alikuwa Amepata kutoka kwa Yesu. Japokuwa Yesu Aliweza kupitia magumu ya kila aina, kuwa Mnyenyekevu na kujificha, kusulubishwa kwa ajili ya Mungu, Mungu Alipata tu sehemu moja ya utukufu Wake, na utukufu Wake ulipatikana Israeli. Mungu bado Ana sehemu nyingine ya utukufu: kuja duniani kufanya kazi na kufanya kundi la watu kuwa wakamilifu.

2 Siku ikija ambayo watu watafanywa wakamilifu na Mungu, na wanaweza kujisalimisha mbele Yake, na kuweza kumtii Mungu kabisa, na kuyawacha matarajio na majaliwa yao mikononi mwa Mungu, basi sehemu ya pili ya utukufu wa Mungu itakuwa imepatikana kikamilifu. Hii ni kusema kuwa wakati ambapo kazi ya Mungu wa vitendo itakapokuwa imekamilishwa kabisa, kazi Yake katika bara ya Uchina itafika kikomo; kwa maneno mengine, wakati wale walioamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mungu watakapokuwa wamefanywa wakamilifu, Mungu Atatukuzwa. Mungu Alisema kwamba Ameleta sehemu ya pili ya utukufu Wake Mashariki, na bado hili halionekani kwa macho. Mungu Ameleta kazi Yake Mashariki: tayari Amekuja Mashariki, na huu ni utukufu wa Mungu. Leo ingawa kazi yake haijakamilika bado, kwa sababu Mungu Ameamua kufanya kazi, bila shaka itakamilika. Mungu Ameamua kuwa Ataikamilishia kazi yake Uchina, na Ameamua kuwafanya kuwa wakamilifu. Hivyo Hawapatii njia nyingine—tayari Ameishinda mioyo yenu, na lazima utaendelea upende usipende, na mnapokubaliwa na Mungu, Mungu Anatukuzwa.

Umetoholewa kutoka katika “Mazungumzo Mafupi Kuhusu “Ufalme wa Milenia Umefika”” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 124 Maana ya Kazi ya Mungu Katika Nchi ya Joka Kubwa Jekundu

Inayofuata: 126 Kristo wa Siku za Mwisho Hufichua Siri ya Mpango wa Mungu wa Usimamizi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp