702 Mabadiliko Katika Tabia Yanahitaji Kazi ya Roho Mtakatifu

1 Iwapo mtu anatafuta kwa dhati hakuamuliwi na jinsi wengine wanamhukumu ama jinsi wengine karibu wanamwona, lakini kunaamuliwa na iwapo Roho Mtakatifu anamfanyia kazi na iwapo ana uwepo wa Roho Mtakatifu, na kunaamuliwa zaidi na iwapo tabia yake inabadilika na iwapo ana maarifa ya Mungu baada ya kupitia kazi ya Roho Mtakatifu kwa muda fulani; ikiwa Roho Mtakatifu anamfanyia mtu kazi, tabia ya mtu huyu itabadilika polepole, na mtazamo wake wa kumwamini Mungu utakua safi polepole.

2 Bila kujali muda gani mtu anamfuata Mungu, kama wamebadilika, hii inamaanisha kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi kwake. Kama hawajabadilika, inamaanisha kwamba Roho Mtakatifu hafanyi kazi kwake. Hata kama hawa watu wanatoa huduma fulani, wanachochewa na nia zao za kupata bahati nzuri. Huduma ya mara kwa mara haiwezi kuchukua nafasi ya mabadiliko katika tabia yao. Hatimaye, bado wataangamizwa, kwani hakuna haja ya wale wanaotoa Huduma ndani ya ufalme, wala hakuna haja ya yeyote ambaye tabia yake haijabadilika kuwahudumia wale watu ambao wamekamilishwa na walio waaminifu kwa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 701 Mabadiliko Katika Tabia ni Nini?

Inayofuata: 703 Kubadili Tabia Yako Kunaanza na Kuelewa Asili Yako

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp