117 Nitalipa Upendo wa Mungu

1

Miaka mingi nimeishi bila mpango wala mwelekeo duniani, upotovu wangu ukiongezeka.

Shukrani kwa Mungu kunena ukweli na kuniokoa, nimerudi kwa familia ya Mungu.

Kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu nimeona utu wangu halisi.

Nimepotoshwa sana na Shetani, sina mfano wa binadamu hata kidogo.

Nikiishi kwa falsafa na sheria za Shetani, nilijitahidi kupata umaarufu na mafanikio.

Nikiwa nimezama dhambini, hatimaye nilijifunza kutafuta njia ya kweli.

Nikimfuata Mungu, nimevumilia mateso na shida nyingi, nimeona shina la uovu wa mwanadamu.

Ninachukia upotovu wangu wa kina na ninaamua kufuatilia ukweli, kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu.

2

Katika enzi hii ovu, wanadamu wote wanaishi katika giza.

Ukweli wa Mungu ni kama nuru inayongaa iangazayo ulimwengu huu wa giza.

Sasa nimeokolewa na Mungu, bado ninapaswa kutafuta mabadiliko ya tabia.

Bila uhalisi wa ukweli ningewezaje kustahili kwa matumizi ya Mungu na kuwa na ushuhuda Kwake?

Bila kujali ni kiasi gani cha kusafishwa au maumivu ninayopaswa kupitia, nitatafuta kukamilishwa na Mungu.

Hukumu ya Mungu imenitakasa, sasa ninaishi kwa kudhihirisha mfano wa kweli wa binadamu.

Ninajua Kristo ni ukweli, njia, na uzima, nitamfuata Mungu kwa uthabiti hadi mwisho.

Neema ya wokovu wa Mungu ni kubwa sana, nitatoa maisha yangu kulipia upendo Wake.

Iliyotangulia: 116 Upendo wa Mungu Huuamsha Moyo Wangu

Inayofuata: 118 Ukweli wa Maneno ya Mungu ni wa Thamani Sana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki