629 Umeacha Fikira Zako za Kidini?
1 Kwa sasa kuna watu wengi ambao huamini kwa njia ya rabsha. Udadisi wenu ni mkubwa mno, tamaa yenu ya kufuatilia baraka ni kubwa mno, na hamu yenu ya kufuatilia maisha ni ndogo mno. Mnafuata tu kwa uzembe, hamtafuti njia ya kweli kamwe, na kwa makusudi hamji kupata uzima. Mna mtazamo wa kutaka tu kuona kitakachotokea. Kwa sababu hamjaziacha dhana zenu za zamani, hakuna yeyote kati yenu ambaye ameweza kujitoa mwenyewe kikamilifu. Baada ya kufika wakati huu, bado mnaendelea kuwa na wasiwasi kuhusu majaliwa yenu wenyewe, fikira zenu zikipinduka mchana na usiku, msiweze kuyaachiilia.
2 Je, unafikiri kuwa Mafarisayo ambao Mimi nawaongelea ni “wazee” katika dini? Je, si nyinyi ni wawakilishi wa Mafarisayo wa kuendelea mbele zaidi wa enzi ya sasa? Je, unafikiri kwamba wale watu Ninaowataja wanaoniangalia Mimi kwa makini dhidi ya Biblia wanarejelea tu wale wataalamu wa Biblia wa nyanja za kidini? Je, unadhani kwamba Ninapozungumza juu ya wale ambao kwa mara nyingine wanamtundika Mungu msalabani Nazungumzia viongozi wa jamii za kidini? Je, si nyinyi ni wahusika bora kabisa ambao mnaigiza wajibu huu? Je, unafikiri kwamba katika maneno yote Ninayoyanena kurudisha pigo dhidi ya dhana za watu ni mzaha kwa wachungaji na wazee wa dini? Si nyinyi pia mmeshiriki katika mambo haya yote?
3 Je, mnafikiri kuwa mna dhana chache tu? Ni kwamba tu nyote mmejifunza kuwa mahiri sana sasa. Hamzungumzii mambo ambayo hamyafahamu ama kusaliti hisia zenu kuyahusu, lakini mioyo yenu ya heshima na mioyo yenu ya utii haipo tu. Kama mnavyoona, kusoma, kuzingatia, na kusubiri ni matendo yenu makuu ya leo. Mmejifunza kuwa mahiri mno. Je! mnajua, hata hivyo, kwamba hii ni aina yenu ya saikolojia ya ujanja? Je, mnafikiri kuwa wakati wa mahiri kwa upande wenu utawasaidia kuepuka kuadibiwa kwa milele?
Umetoholewa kutoka katika “Ni Lazima Muielewe Kazi—Msifuate kwa Rabsha!” katika Neno Laonekana katika Mwili