734 Kushikilia Fikira za Kidini Kutakuangamiza tu

1 Kufikia leo, Mungu atawakamilisha kirasmi wale wasiokuwa na fikira za kidini, ambao wako tayari kuweka pembeni nafsi zao za kale, na ambao wanamtii tu Mungu kwa moyo wa kawaida, na kuwafanya kuwa watimilifu wale wanaotamani neno la Mungu. Watu hawa wanafaa kusimama na kumhudumia Mungu. Kwake Mungu kunayo hekima nyingi na isiyoisha. Kazi Yake ya kustaajabisha na matamshi Yake yenye thamani vinasubiri hata idadi kubwa ya watu waweze kuvifurahia. Kama ilivyo sasa, wale walio na fikira za kidini, wanaochukua hali ya ukubwa, na wale ambao hawawezi kujiweka pembeni wanaona vigumu sana kukubali vitu hivi vipya. Hakuna fursa ya Roho Mtakatifu kuwakamilisha watu hawa.

2 Kama mtu hajaamua kutii, na hana kiu ya neno la Mungu, basi mtu huyo hataweza kupokea mambo mapya. Wataendelea tu kuwa waasi zaidi na zaidi, kuwa wajanja zaidi na zaidi, na hatimaye kujipata kwenye njia mbaya. Katika kufanya kazi Yake sasa, Mungu atawainua watu zaidi wanaompenda kwa kweli na wanaoweza kukubali mwangaza mpya. Na Atakatiza kabisa maafisa wa kidini wanaoonyesha ukubwa wao. Wale wanaokataa mabadiliko kwa ukaidi: Hataki hata mmoja wao. Je, unatekeleza huduma yako kulingana na mapendeleo yako, au unafanya kile Mungu anachotaka? Je, wewe ni mmojawapo wa maafisa wa kidini, au wewe ni mtoto mchanga anayefanywa kuwa mtimilifu na Mungu?

3 Fikira za kale za kidini zitayakaba maisha ya mtu. Uzoefu ambao mtu anapata utamwongoza mbali na Mungu, kufanya mambo kwa njia yake mwenyewe. Usipoviweka vitu hivi chini, vitakuwa kikwazo katika kukua kwa maisha yako. Mungu siku zote amewakamilisha wote wanaomhudumia. Hawatupilii mbali kwa urahisi tu. Kama tu utakubali kwa kweli hukumu na kuadibu kwa neno la Mungu, kama unaweza kuweka pembeni matendo yako na sheria za kidini za kale, na kukoma kutumia fikira za kale za kidini kama kipimo cha neno la Mungu hii leo, ni hapo tu ndipo kutakuwa na mustakabali kwako. Lakini kama utashikilia vitu vya kale, kama bado unavithamini, basi huwezi kupata wokovu. Mungu hawatambui watu kama hao.

Umetoholewa kutoka katika “Njia ya Huduma ya Kidini Lazima Ipigwe Marufuku” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 733 Unapaswa Kutafuta Kukubaliwa na Mungu

Inayofuata: 735 Matokeo ya Huduma ya Shauku kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

269 Nitampenda Mungu Milele

1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu...

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki