426 Unapaswa Kujitahadhari Kutuliza Moyo Wako Mbele za Mungu
1 Ikiwa moyo wako kweli umetulia mbele ya Mungu hutasumbuliwa na chochote kinachoendelea huko nje duniani, na hakuna mtu, tukio au jambo litakalokumiliki. Ikiwa mmeingia katika hili, basi zile hali hasi na mambo yote hasi—fikira za binadamu, falsafa za kuishi, mahusiano yasiyo ya kawaida na watu, na mawazo ndani ya moyo wako yatatoweka kwa kawaida. Kwa sababu kila mara unatafakari maneno ya Mungu, na moyo wako kila mara unasonga karibu na Mungu na kumilikiwa na maneno ya sasa ya Mungu, mambo hayo mabaya huvuliwa bila kufahamu. Mambo mapya mazuri yanapokumiliki, mambo ya zamani mabaya hayatakuwa na nafasi, kwa hiyo usitilie maanani mambo hayo mabaya. Huhitaji kufanya jitihada za kujaribu kuyadhibiti.
2 Tilia maanani kutulia mbele ya Mungu, kula na kunywa maneno zaidi ya Mungu na kuyafurahia, imba nyimbo nyingi zaidi za dini ukimsifu Mungu, na wacha Mungu awe na nafasi ya kukushughulikia, kwa sababu Mungu wakati huu anataka binafsi kuwakamilisha watu, Anataka kuupata moyo wako, Roho Wake husisimua moyo wako, na ukiishi mbele ya Mungu ukifuata uongozi wa Roho Mtakatifu utamridhisha Mungu. Ukitilia maanani kuishi katika maneno ya Mungu na kushiriki zaidi kuhusu ukweli ili kupata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, basi fikira hizo za kidini, kujidai na kujikweza vitatoweka vyote, na kisha utajua namna ya kugharimia rasilmali kwa ajili ya Mungu, kujua namna ya kumpenda Mungu, na namna ya kumridhisha Mungu. Mambo hayo nje ya Mungu kisha husahaulika bila kufahamu.
Umetoholewa kutoka katika “Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili