121 Kusudi la Kazi ya Mungu Katika Siku za Mwisho
1 Nimezungumza mara nyingi sana kwamba kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kwa ajili ya kubadilisha roho ya kila mtu, kubadilisha nafsi ya kila mtu, ili kwamba moyo wake, ambao umeteseka sana na kiwewe, uwe umebadilishwa, hivyo kuokoa nafsi yake, ambayo imeumizwa kwa kina zaidi na uovu; ni kwa sababu ya kuamsha roho za watu, kuyeyusha mioyo yao baridi, na kuwaruhusu kurudisha nguvu za ujana. Haya ndiyo mapenzi makubwa ya Mungu. Weka pembeni mazungumzo ya ni namna gani maisha na uzoefu wa mwanadamu ni ya kiburi au ya kina; mioyo ya watu itakapokuwa imeamshwa, wanapokuwa wameamshwa kutoka kwa ndoto zao na kujua kikamilifu madhara yaliyoletwa na joka kuu jekundu, kazi ya huduma ya Mungu itakuwa imekamilika. Siku ambayo kazi ya Mungu itakuwa imekamilika pia ni siku ambapo mwanadamu ataanza rasmi kwenye njia sahihi ya kumwamini Mungu. Wakati huu, huduma ya Mungu itakuwa imekamilika: Kazi ya Mungu katika mwili itakuwa imekamilika kabisa, na mwanadamu atakuwa ameanza rasmi kufanya kazi ambayo anapaswa kufanya—atatekeleza huduma yake. Hizi ni hatua za kazi ya Mungu.
2 Maana kazi ya Mungu ni wokovu kamili wa mwanadamu—mwanadamu aliyekombolewa, ambaye bado anaishi chini ya nguvu za giza, na ambaye hajawahi kuzinduka kutoka katika eneo hili la kusanyiko la pepo; ili kwamba mwanadamu aweze kuwekwa huru dhidi ya milenia ya dhambi, na kuwa wapendwa wa Mungu, kumkanyaga kabisa joka kuu jekundu, kuanzisha ufalme wa Mungu, na kuupumzisha moyo wa Mungu mapema, ni kutoa mawazo bila woga, bila kubania, kwa chuki inayovimbisha kifua chenu, kuondoa kabisa vijidudu hivyo, kuwafanya muache maisha haya ambayo hayana tofauti na maisha ya ng’ombe au farasi, ili msiwe watumwa tena, ili msiweze kukanyagwa tena au kuamrishwa na joka kuu jekundu; hamtakuwa tena wa taifa hili lililoanguka, hamtakuwa tena wa joka kuu jekundu lenye chuki, hamtafungwa nalo tena. Kiota cha pepo hakika kitachanwachanwa na Mungu, na mtasimama kando ya Mungu—nyinyi ni wa Mungu, na sio wa milki hii ya watumwa.
Umetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili