634 Unalindwa Kwa Sababu Unaadibiwa na Kuhukumiwa

1 Leo, ni kwa sababu mnaadibiwa, kuhukumiwa, na kulaaniwa ndiyo mnapewa ulinzi. Ni kwa sababu mmeteseka sana ndiyo mnalindwa. Kama sivyo, mngekuwa tayari mmepotoka. Huku si kufanya mambo yawe magumu kwenu kwa makusudi—asili ya mwanadamu ni ngumu kubadili, na lazima iwe hivyo ili tabia zao zibadilishwe. Leo, hamna hata dhamiri au akili ambazo Paulo alikuwa nazo, wala hamwezi hata kujitambua kama yeye. Lazima mushurutishwe kila wakati, na kila wakati lazima muadibiwe na kuhukumiwa ili roho zenu zichangamshwe. Kuadibu na hukumu ndivyo bora kabisa kwa maisha yenu. Na inapolazimu, lazima pia ukweli unaowafikia uadibiwe; ni hapo tu ndipo mtakapotii kikamilifu.

2 Asili zenu ni kana kwamba bila kuadibu na kulaani, hamngetaka kuinamisha vichwa vyenu, hamngetaka kutii. Bila ukweli ulio mbele yenu, hakungekuwa na matokeo. Ninyi ni duni sana na msio na thamani katika tabia! Bila kuadibu na hukumu, itakuwa vigumu kwenu kushindwa, na itakuwa vigumu kwa udhalimu na kutotii kwenu kushindwa. Asili yenu ya zamani imekita mizizi sana. Kama mngewekwa juu ya kiti cha enzi, hamngefahamu urefu wa mbingu na kina cha dunia, sembuse kujua mnakoelekea. Hamjui hata mlikotoka, hivyo mngewezaje kumjua Bwana wa uumbaji?

3 Bila kuadibiwa na kulaaniwa kwa wakati unaofaa leo, siku yenu ya mwisho ingekuwa imeshawadia kitambo. Hiyo ni kando na majaaliwa yenu—je, hayo hayatakuwa katika hatari ya karibu zaidi? Bila kuadibu na hukumu hii ya wakati unaofaa, ni nani anayejua jinsi ambavyo mngekuwa wenye kiburi, au jinsi ambavyo mngekuwa wapotovu. Hamna uwezo wa kujidhibiti na kutafakari kujihusu wenyewe hata kidogo. Kuadibu huku na hukumu hii vimewafikisha leo, na vimehifadhi kuwepo kwenu. Je, hamfai kufanya vema zaidi katika kukubali kuadibu na hukumu ya leo? Je, mna chaguo gani jingine?

Umetoholewa kutoka katika “Utendaji (6)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 633 Hukumu ya Mungu ni Upendo

Inayofuata: 635 Pitia Hukumu ya Mungu ili Utupilie Mbali Ushawishi wa Shetani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp