440 Maisha Ya Kiroho Yanayofaa Yanapaswa Kudumishwa Daima

1 Katika kazi ya Mungu, haijalishi ni nini Anafanya ama nini kinabadilika, kwa uchache sana watu lazima watu wadumishe hali ya chini zaidi ya maisha ya kawaida ya kiroho. Pengine umekuwa mwangalifu katika hatua hii ya sasa ya maisha yako ya kiroho, lakini bado hujapata mengi; hujavuna pakubwa. Katika hali za aina hizi lazima bado ufuate sheria; lazima ufuate sheria hizi ili usipate hasara katika maisha yako na ili uyakidhi mapenzi ya Mungu. Kama maisha yako ya kiroho si ya kawaida, huwezi kuelewa kazi ya sasa ya Mungu, badala yake kila wakati utahisi kwamba hayalingani kabisa na dhana zako mwenyewe, nawe una hiari ya kumfuata, lakini unakosa bidii ya ndani.

2 Kwa hivyo haijalishi ni nini Mungu Anafanya sasa, lazima watu washirikiane. Watu wasiposhirikiana Roho Mtakatifu Hawezi kufanya kazi Yake, na kama watu hawana moyo wa kushirikiana, basi si rahisi wao kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Kama unataka kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu ndani mwako, na kutaka kupata kibali cha Mungu, lazima udumishe moyo wako wa ibada asili mbele ya Mungu. Sasa, si lazima kwako kuwa na maelewano zaidi ya ndani, nadharia ya juu, ama vitu vingi—yote yanayohitajika ni kwamba ushikilie neno la Mungu juu ya msingi asili. Watu wasiposhirikiana na Mungu na wasipofuata kuingia zaidi, Mungu Atachukua kile walichokuwa nacho wakati mmoja.

3 Ndani, watu wana tamaa kila wakati ya kilicho rahisi na afadhali wajifurahishe na kile ambacho kinapatikana. Wanataka kupata ahadi za Mungu bila kulipa gharama yoyote. Haya ni mawazo badhirifu ndani ya wanadamu. Kupata maisha yenyewe bila kulipa gharama—nini kimewahi kuwa rahisi? Mtu anapoamini katika Mungu na kutafuta kuingia katika maisha na kutafuta badiliko katika tabia yake, ni lazima alipe gharama na kufikia kiwango ambapo atamfuata Mungu daima bila kujali Anachofanya. Hiki ni kitu ambacho watu lazima wafanye. Hata kama unafuata haya yote kama sharti, ni lazima uyazingatie, na haijalishi majaribu yako ni makubwa kiasi gani, huwezi kuachilia uhusiano wako wa kufaa na Mungu. Unapaswa kuweza kuomba, udumishe maisha yako ya kanisa, na uishi na ndugu na dada. Mungu anapokujaribu, bado unapaswa kutafuta ukweli. Hiki ndicho kiwango cha chini cha maisha ya kiroho.

Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 439 Mwache Mungu Aingie Moyoni Mwako

Inayofuata: 441 Jinsi ya Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida Na Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp