443 Zingatia Maneno ya Mungu kwa Ajili ya Uhusiano Ufaao na Wengine

1 Ikiwa unataka kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, basi lazima moyo wako umgeukie Mungu. Hili likiwa msingi, pia utakuwa na uhusiano wa kawaida na watu wengine. Iwapo huna uhusiano wa kawaida na Mungu, basi haijalishi unachofanya kudumisha uhusiano wako na watu wengine, haijalishi jinsi gani unafanya kazi kwa bidii au ni nguvu kiasi gani unaweka ndani yake, bado ni ya falsafa ya mwanadamu ya maisha. Unadumisha nafasi yako miongoni mwa watu kupitia mtazamo wa mwanadamu na falsafa ya mwanadamu ili kwamba watu wakupe wewe sifa, lakini hufuati neno la Mungu ili kuanzisha uhusiano wa kawaida na watu. Iwapo huzingatii uhusiano wako na watu lakini unadumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, ikiwa uko tayari kumpa Mungu moyo wako na ujifunze kumtii, basi kwa kawaida sana, uhusiano wako na watu wote utakuwa wa kawaida.

2 Kwa njia hii, uhusiano huu haujengwi kwa mwili, bali juu ya msingi wa upendo wa Mungu. Kwa kiasi kikubwa hakuna ushirikiano uliojengwa juu ya mwili, lakini katika roho kuna ushirikiano na vilevile upendo, starehe, na kutoleana kwa wenza. Haya yote yanafanywa kwa msingi wa moyo unaomridhisha Mungu. Uhusiano huu haudumishwi kwa kutegemea falsafa ya mwanadamu ya maisha, bali unaundwa kwa kawaida kupitia mzigo wa Mungu. Hauhitaji jitihada zilizofanywa na binadamu. Unahitaji tu kutenda kulingana na maadili ya neno la Mungu. Iwapo huzingatii uhusiano wako na watu lakini unadumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, ikiwa uko tayari kumpa Mungu moyo wako na ujifunze kumtii, basi kwa kawaida sana, uhusiano wako na watu wote utakuwa wa kawaida.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 442 Ni Muhimu Kuwa na Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Inayofuata: 444 Una Uhusiano wa Kawaida na Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp