452 Kanuni ya Kazi Ya Roho Mtakatifu

1 Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa kanuni hii: kupitia ushirikiano na watu, kupitia kwa wao kuomba kimatendo, kumtafuta na kusonga karibu na Mungu, matokeo yanaweza kupatikana na wanaweza kupata nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu. Si kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi kivyake, au mwanadamu anafanya kazi kivyake. Wote ni wa muhimu, na jinsi wanadamu wanavyoshiriki zaidi na jinsi wanavyotaka zaidi kufikia viwango vya mahitaji ya Mungu, ndivyo kazi ya Roho Mtakatifu inaimarika. Ni ushirikiano halisi tu wa wanadamu, kupitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndivyo vinaweza kutoa matukio halisi na ufahamu wa kweli wa kazi ya Mungu. Hatua kwa hatua, kupitia kwa mazoea kwa njia hii, mwanadamu mkamilifu hatimaye huzalishwa.

2 Mungu hafanyi vitu vya miujiza; katika dhana za mwanadamu, Mungu ni mwenye uweza, na kila kitu kinafanywa na Mungu—na hutokea kwamba watu wanasubiri tu bila kufanya chochote, hawasomi maneno ya Mungu au kuomba, na wanasubiri tu kuguswa na Roho Mtakatifu. Walio na ufahamu sahihi, hata hivyo, wanaamini hili: matendo ya Mungu yanaweza kufikia pale ambapo ushirikiano wangu umefikia, na athari ya kazi ya Mungu kwangu inategemea namna ninavyoshirikiana. Mungu anenapo, ninapaswa kufanya lolote niwezalo na kuyaelekea maneno ya Mungu; hili ndilo ninapaswa kufanikisha.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Uhalisi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 451 Kazi ya Roho Mtakatifu ni ya Kawaida na ya Vitendo

Inayofuata: 453 Kazi ya Roho Mtakatifu ina Kanuni Zake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp