Dibaji
Yaliyomo katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya yamegawanywa katika sehemu mbili: Nyimbo za Maneno ya Mungu na Nyimbo za Maisha ya Kanisa.
Nyimbo za maneno ya Mwenyezi Mungu zimetolewa kabisa kutoka kwa vifungu vilivyoteuliwa vya Neno Laonekana katika Mwili na Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo. Kugeuzwa kwa matamshi haya yaliyo bora kabisa kuwa wimbo ni faida kubwa kwa ibada ya kiroho ya wateule wa Mungu, katika kufanya ibada zao za kiroho, kumkaribia Mungu, kutafakari maneno Yake, na kuelewa ukweli. Ni za faida kubwa hata zaidi kwa watu wanaopitia maneno ya Mungu na kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu.
Nyimbo za Maisha ya Kanisa zinajumuisha yale ambayo wateule wa Mungu katika maeneo tofauti wamepata na kujifunza kutoka kwa kupitia kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho. Uzoefu huu halisi unashuhudia kikamilifu matokeo ambayo kazi ya Mungu ya hukumu hutimiza ndani ya watu. Unashuhudia kwamba ukweli ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu umewaokoa watu kabisa kutoka kwa nguvu za Shetani, kwamba umewatakasa na kuwaletea wokovu. Unashuhudia kwamba Mungu amefanyiza kundi la washindi nchini China, Amemshinda Shetani, na Ametukuzwa kabisa. Nyimbo hizi huwaletea watu imani na nguvu, na kuwatia moyo ili watafakari juu yao wenyewe, waone kasoro zao, watatue shida zao na mitazamo iliyochanganyikiwa—jambo hili likithibitisha kwamba ni wale tu wanaoelewa ukweli ndio wanaoweza kujikomboa kutoka kwa ushawishi wa Shetani, kamba ukweli unaweza kuwaweka watu huru. Nyimbo nzuri ni rafiki katika maisha, na zipo hapo kusaidia wakati wowote zinapohitajika. Ni chanzo cha ujenzi mkuu wa maadili. Nyimbo hizi za maisha ya kanisa ni ushuhuda wa wateule kupitia kazi ya Mungu.
Novemba 13, 2018