103 Sala ya Watu wa Mungu

Watu wa Mungu wanarudi mbele ya kiti Chake cha enzi.

Tunatoa sala zetu kwa Mungu.

1

Mungu awabariki wote wanaotamani kuonekana Kwake.

Mungu awabariki wote waisikie sauti Yake hivi karibuni.

Na wale wote ambao Mungu amewachagua kabla wafuate nyayo za Mwanakondoo.

Mungu awape nuru wale wanaotafuta.

Mungu awape nuru wale wanaosubiri na kutazama.

Na wote wamwone Mkombozi, waone kwamba Amerejea, waone ukweli ambao Ameleta

Watu wa Mungu wanarudi mbele ya kiti Chake cha enzi.

Tunatoa sala zetu kwa Mungu.

2

Na wanadamu wavunje minyororo ya fikira zao wenyewe.

Na wanadamu watafute na kujifunza njia ya kweli.

Na wanadamu wapate lishe ya maneno ya Mungu, ili roho zao zisione kiu tena kwa siku nyingi.

Na binadamu wajifunze kuwa na utambuzi, wasidanganywe tena na uwongo wa kina wa Shetani.

Na Mungu atuongoze tuhubiri injili, tumshuhudie, na Awaweke watu wake katika upendo Wake daima.

Watu wa Mungu wanarudi mbele ya kiti Chake cha enzi.

Tunatoa sala zetu kwa Mungu.

3

Na Mungu atupe nuru ili tuelewe, ili tuweze kulifahamu neno Lake, mapenzi Yake.

Na watu wote walithamini neno la Mungu na kuishi kulingana nalo.

Na Atuhukumu na kutufunza nidhamu ili wajibu wetu utimizwe.

Na Mungu atuongezee majaribu yabadilishe tabia zetu.

Na watu wote wajue mema kutoka kwa mabaya.

Na watu wote waweke ukweli katika vitendo na kutii amri zote za Mungu.

4

Na Mungu awaadhibu watenda maovu wote, ili maisha ya kanisa yasikatizwe.

Na Mungu awakamilishe watu zaidi wawe wenye mawazo sawa na Yeye.

Na watu watoe upendo wao wa kweli kwa Mungu wa kweli na anayependeza.

Na Mungu awabariki wale wanaorejea Kwake.

Na sote tuishi katika nuru.

Watu wa Mungu wanarudi mbele ya kiti Chake cha enzi.

Tunatoa sala zetu kwa Mungu.

Tunatoa sala zetu kwa Mungu.

Iliyotangulia: 102 Tunapaswa Kukimya Mbele za Mungu Daima

Inayofuata: 104 Nataka Kupenda Mungu Zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

115 Nimeuona Upendo wa Mungu

1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki