574 Kutenda Ukweli Katika Wajibu Wako ni Muhimu
Kila mara ni katika harakati ya kufanya wajibu wake ndipo mwanadamu polepole anabadilishwa, na ni katika harakati hii ndipo anapoonyesha utiifu wake. Kwa hivyo, kadiri uwezavyo kufanya wajibu wako, ndivyo ukweli utakaopokea unavyoongezeka, na vivyo hivyo mwonekano wako utakuwa halisi zaidi. Wale ambao hufanya tu mambo bila ari yoyote katika kufanya wajibu wao na hawautafuti ukweli mwishowe wataondolewa, kwani watu kama hao hawafanyi wajibu wao katika utendaji wa ukweli, na hawatendi ukweli katika kutekeleza wajibu wao. Watu kama hao ni wale wanaobaki bila kubadilika na watalaaniwa. Misemo yao haijajaa najisi tu, ila wakitamkacho si kingine bali ni uovu.
Umetoholewa kutoka katika “Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili