506 Tenda Ukweli Zaidi, Barikiwa na Mungu Zaidi

1 Mungu hubariki wale ambao wana maono, ambao wana ukweli, ambao wana ufahamu, na ambao wanampenda kwa kweli. Watu wakitaka kuuona upendo wa Mungu, lazima waweke ukweli katika vitendo katika maisha halisi, lazima wawe tayari kuvumilia mateso na kuacha hicho wanachokipenda na kumridhisha Mungu, mbali na machozi kwenye macho yao, lazima waweze kuuridhisha moyo wa Mungu. Kwa njia hii, kwa hakika Mungu atakubariki, na ukivumilia matatizo kama haya, yatafuatiwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kupitia kwa maisha halisi, na kutokana na kupitia maneno ya Mungu, watu wanaweza kuona upendo wa Mungu, na wanaweza kumpenda Mungu kwa ukweli ikiwa tu wameuonja upendo wa Mungu.

2 Kadiri unavyoweka ukweli katika vitendo, ndivyo unavyokuwa na ukweli; kadiri unavyoweka ukweli katika vitendo, ndivyo unavyokuwa na upendo wa Mungu; na kadiri unavyoweka ukweli katika vitendo, ndivyo unavyobarikiwa na Mungu. Kama utatenda kwa njia hii kila mara, upendo wa Mungu kwako utakuwezesha kuona polepole, jinsi tu ambavyo Petro alivyokuja kumjua Mungu: Petro alisema kuwa si kuwa Mungu ana busara ya kuumba mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo pekee, lakini, aidha, kuwa Ana busara ya kufanya kazi halisi ndani ya watu. Petro alisema kuwa Mungu hastahili tu upendo wa watu kwa sababu ya uumbaji Wake wa mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo, lakini, vilevile, kwa sababu ya uwezo Wake wa kuumba mwanadamu, kumwokoa, kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na kutoa upendo wake kwa mwanadamu.

Umetoholewa kutoka katika “Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 505 Kuteseka kwa Ajili ya Kutenda Ukweli Hupata Sifa za Mungu

Inayofuata: 507 Ni kwa Kuishi kwa Kudhihirisha Uhalisi tu Ndiyo Unaweza Kutoa Ushahidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp