499 Tenda Ukweli na Tabia Yako Itabadilika
1 Kusudi la ushurika wazi kuhusu ukweli ni ili kuwawezesha watu kutenda ukweli na kubadilisha tabia zao; sio tu kwa ajili ya kuwafanya wauelewe. Kama unaelewa ukweli lakini hauuweki katika vitendo, basi kufanya ushirika kuuhusu na ufahamu wa ukweli hautakuwa na maana yoyote. Iwapo unaelewa ukweli lakini kamwe hauuweki katika matendo, utapoteza nafasi ya kuupata ukweli, na pia nafasi yoyote ya kuokolewa. Iwapo umeuweka ukweli unaoelewa katika vitendo, basi utapata ukweli wa mwingi wa kina zaidi; utafikia wokovu wa Mungu, vile vile nuru, mwangaza na uongozi wa Roho Mtakatifu.
2 Baadhi ya watu husema kuwa kutenda ukweli hakuwezi kutatua tabia zao potovu. Wengine huamini kuwa ukweli hauwezi kutatua kikamilifu tabia potovu za mtu. Ukweli ni kwamba shida zote za watu zaweza kutatuliwa; cha muhimu ni kama wao wanaweza kutenda kulingana na ukweli au hapana. Matatizo yanayowakumba sasa sio saratani ama magonjwa yasiotibika. Iwapo mnaweza kuweka ukweli katika matendo, basi matatizo hayo yote yanaweza kubadilishwa, ikitegemea kama unaweza kutenda kwa mujibu wa ukweli. Kama unatembea katika njia ya kufuatilia ukweli, basi bila shaka utafanikiwa; hata hivyo, kama unatembea katika njia mbaya, basi wewe umemalizwa.
3 Watu wengine wanajipata wamebanwa katika shughuli zao wenyewe siku nzima huku wakikosa kuchunguza ama kutenda ukweli unaopatikana tayari. Njia hii ya kutenda ni ya kipumbavu sana; watu wa aina hii ni watesekaji kiasili, kwa kuwa wanazo baraka lakini hawazifurahii! Njia ya kwenda mbele ipo; kinachofaa kufanywa tu ni wewe uitende. Kama umeamua kuuweka ukweli katika matendo, basi udhaifu wako na dosari mbaya vinaweza kubadilishwa. Hata hivyo, lazima kila wakati uchukue tahadhari na mwenye busara na kupitia ugumu zaidi. Kuwa na imani kunahitaji kuwa mwenye busara. Je, unaweza kumwamini Mungu vizuri ukichukua namna hii ya kawaida?
Umetoholewa kutoka katika “Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kusonga Mbele” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo