916 Mamlaka na Nguvu ya Muumba Havina Mipaka

1 “Naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.” Haya ni matamshi ya asili yaliyotamkwa na Muumba kwa mwanadamu. Aliposema matamshi haya, upinde wa mvua ulionekana mbele ya macho ya binadamu, ambapo ulibakia mpaka leo. Upinde wa mvua ni ishara ya agano lilioanzishwa kati ya Muumba na binadamu; hauhitaji msingi wowote wa kisayansi, haukuumbwa na binadamu, wala binadamu hawezi kuubadilisha. Ni maendelezo ya mamlaka ya Muumba baada ya Yeye kuongea matamshi Yake.

2 Muumba alitumia mbinu fulani Yake mwenyewe kutii agano lake na binadamu na ahadi Yake, na hivyo basi matumizi Yake ya upinde wa mvua kama ishara ya agano ambalo Alianzisha ni maelekezo na sheria ya mbinguni yatakayobakia milele hivyo, haijalishi kama ni kuhusiana na Muumba au mwanadamu aliyeumbwa. Ilhali sheria hii isiyobadilika ni, lazima isemwe, maonyesho mengine ya kweli ya mamlaka ya Muumba kufuatia uumbaji Wake wa viumbe vyote, na lazima isemwe kwamba mamlaka na nguvu za Muumba havina mipaka.

3 Hiki kilikuwa kitendo kingine kilichotekelezwa na Mungu kwa kutumia matamshi Yake, na kilikuwa ni ishara ya agano ambalo Mungu alikuwa ameanzisha na mwanadamu kwa kutumia matamshi. Alimwambia binadamu kuhusu kile ambacho Aliamua kuleta, na kwa njia gani kingekamilishwa na kutimizwa, na kwa njia hii suala liliweza kutimizwa kulingana na matamshi kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Mungu pekee ndiye anayemiliki nguvu kama hizo, na leo, miaka elfu kadhaa baada ya Yeye kuongea matamshi haya, binadamu angali bado anaweza kuangalia upinde wa mvua uliozungumziwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu.

4 Kwa sababu ya matamshi hayo yaliyotamkwa na Mungu, kitu hiki kimebakia bila ya kusongezwa na kubadilishwa mpaka hadi leo. Hakuna anayeweza kuuondoa upinde huu wa mvua, hakuna anayeweza kubadilisha sheria zake, na upo kimsingi kutokana na matamshi ya Mungu. Haya kwa hakika ni mamlaka ya Mungu. “Mungu ni mzuri tu kama matamshi Yake, na matamshi Yake yataweza kukamilishwa, na kile ambacho kimekamilishwa kinadumu milele.” Matamshi kama haya kwa kweli yanaonyeshwa waziwazi hapa, na ni ishara na sifa wazi kuhusu mamlaka na nguvu za Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 915 Yote Chini ya Mamlaka ya Muumba ni Mazuri Kabisa

Inayofuata: 917 Vitu Vyote Huishi na Kuangamia kwa Mamlaka ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp