64 Kiini Cha Upinzani wa Mafarisayo kwa Yesu

1

Je, ungependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu?

Je, ungependa kujua kiini chao ni nini?

Walikuwa wamejawa na ndoto kuu kumhusu Masiha,

wakiamini tu katika kuja Kwake, kutotafuta ukweli wa maisha.

Hadi leo bado wanamngoja, bila kujua bado njia ya ukweli ama uzima.

2

Watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wanawezaje kupata baraka za Mungu?

Inawezekanaje wao kumwona Masiha?

Walimpinga Yesu kwa sababu hawakuijua njia ya kweli Aliyozungumzia,

hawakumwelewa Masiha ama kazi ya Roho Mtakatifu.

Kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona ama kuwa na Yeye,

walionyesha heshima tupu kwa jina Lake

huku wakipinga kiini Chake kwa kila njia.

3

Wakaidi, wenye kiburi, walishikilia kwa ukaidi imani hii.

Ingawa mahubiri Yake yalikuwa mazito na mamlaka Yake ya juu,

kama tu Anaitwa Masiha ndiyo wao wangekuwa tayari kukubali.

Lakini haya ni maneno ambayo mwanadamu anafaa kudhihaki na kuyaita ndoto za kujionyesha.

4

Mungu anakuuliza: Je, si wewe utarudia makosa ya Mafarisayo?

Kwa kuwa humwelewi Yesu Kristo,

je, unaweza kuitambua njia ya ukweli na njia ya uzima?

Je, unaweza kufuata kazi ya Roho Mtakatifu?

Je, unaweza kutoa uhakika kuwa hutampinga Kristo?

Kama huwezi, basi uko ukingoni mwa kifo.

Umetoholewa kutoka katika “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 63 Ni Wale tu Wanaokubali Ukweli Ndio Wanaweza Kuisikia Sauti ya Mungu

Inayofuata: 65 Mungu Aomboleza Siku za Usoni za Binadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki