576 Kufanya Wajibu Wako Kunamaanisha Kufanya Yote Uwezayo
1 Mwanadamu kufanya wajibu wake ni, kwa uhakika, kutimiza yote yaliyo ya asili yake, yaani, yale yawezekanayo kwa mwanadamu. Hapo ndipo wajibu wake hutimizika. Dosari za mwanadamu wakati wa huduma ya mwanadamu hupunguzwa taratibu kupitia kwa uzoefu uongezekao na mchakato wa uzoefu wake wa hukumu; hayazuii au kuathiri wajibu wa mwanadamu. Wanaoacha kutoa huduma au kuzalisha na kurudi nyuma kwa kuogopa makosa yanayoweza kuwepo katika huduma ndio waoga zaidi miongoni mwa wanadamu wote.
2 Ikiwa mwanadamu haonyeshi anachopaswa kuonyesha wakati wa kutoa huduma au kutimiza kile kilicho katika uwezo wake kiasili, na badala yake huzembea na kufanya tu bila ari yoyote, atakuwa amepoteza majukumu yake ambayo kiumbe anapaswa kuwa nayo. Mwanadamu kama huyu anachukuliwa kuwa mtu hafifu na duni apotezaye nafasi; itakuaje kwamba mtu kama huyu aitwe kiumbe? Je, hao si ni vyombo vya upotovu ving’aavyo kwa nje ila vimeoza kwa ndani?
Umetoholewa kutoka katika “Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili