302 Watu Wanamchukulia Kristo kama Mwanadamu wa Kawaida

1 Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na wote hutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mnaweza kuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mmemwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka.

2 Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo. Nyinyi mnamchukua Kristo kama asiyekufa au mhenga, lakini hakuna anayemchukulia kama mwanadamu wa kawaida mwenye kiini kitakatifu. Kwa hivyo, wengi wa wale ambao wanatamani usiku na mchana kumwona Mungu ni hasa maadui wa Mungu na hawapatani na Mungu. Je, haya si makosa kwa upande wa mwanadamu? Hii ni kwa maana katika wakati uliopita, uliopo na ujao, wengi wa wale ambao hupatana na Kristo wameanguka au wataanguka; wao wote wamechukua jukumu la Mafarisayo. Sababu yenu ya kushindwa ni nini? Ni kwa sababu hasa katika fikra zenu kuna Mungu mkubwa, Atamanikaye.

3 Lakini ukweli si kama vile mwanadamu atakavyo. Kristo si mkubwa tu, bali Yeye ni mdogo hasa; Yeye si mtu tu, bali ni mtu wa kawaida; Hana uwezo wa kupaa mbinguni tu, bali hana pia uhuru wa kuzunguka ardhini. Na kwa hivyo, watu humtendea kama mtu wa kawaida; wao humtendea kikawaida wanapokuwa pamoja naye, na kusema maneno kiholela Kwake, wakati huu wote wakingojea kurudi kwa “Kristo wa kweli.” Mnamchukua Kristo aliyekuja tayari kama mtu wa kawaida na neno Lake kama lile la mtu wa kawaida. Kwa hivyo, hamjapata chochote kutoka kwa Kristo na badala yake mmeonyesha ubaya wenu kwenye mwangaza kabisa.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 301 Watu Hawajui Sura ya Kweli ya Mungu

Inayofuata: 303 Una Imani ya Kweli Katika Kristo?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp