323 Watu Hawamtendei Mungu kama Mungu

1 Kila mtu kila wakati hufanya hesabu kama hizi ndani ya moyo wake, na yeye hutoa madai yake kwa Mungu yanayoonyesha motisha yake, malengo na mawazo ya mabadilishano. Hii ni kusema, ndani ya moyo wake mwanadamu siku zote humweka Mungu majaribuni, siku zote anaunda njama kumhusu Mungu, akijitetea kwa Mungu kila wakati kwa sababu ya mwisho wake binafsi na kujaribu kumfanya Mungu atoe kauli, aweze kuona kama Mungu anaweza kumpa kile anachotaka au la. Wakati huohuo akimfuata Mungu, binadamu hamchukulii Mungu kama Mungu. Siku zote mwanadamu amejaribu kufanya mipango na Mungu, akitoa madai bila kusita kwake Yeye na hata akimsukuma Yeye katika kila hatua, akijaribu kupiga hatua ya maili licha ya kupewa inchi moja.

2 Wakati huohuo akijaribu kufanya mabadilishano na Mungu, binadamu pia anabishana na Yeye, na wapo hata watu ambao, wakati majaribu yanawapata au wanapojipata katika hali ya kuteketea, mara nyingi wanakuwa wanyonge, wananyamaza na kuzembea katika kazi yao, na wanajaa malalamiko kumhusu Mungu. Tangu wakati ambapo mwanadamu alianza kumwamini Mungu, amemchukulia Mungu kama alama ya pembe inayoonyesha wingi wa neema, kisu cha Kijeshi cha Uswisi, na amejichukulia yeye mwenyewe kuwa mdaiwa mkubwa zaidi wa Mungu, ni kana kwamba kujaribu kupata baraka na ahadi kutoka kwa Mungu ni haki na jukumu lake la asili, huku jukumu la Mungu likiwa ni kumlinda na kumtunza mwananadamu na kumruzuku. Huu ndio ufahamu wa kimsingi wa “imani katika Mungu” wa wale wote wanaomwamini Mungu, na ufahamu wao wa kina zaidi wa dhana ya imani katika Mungu.

3 Kutoka katika kiini cha asili ya mwanadamu hadi katika ufuatiliaji wake wa kibinafsi, hakuna kitu chochote kinachohusiana na kumcha Mungu. Nia ya mwanadamu katika kumwamini Mungu huenda isiwe na uhusiano na kumwabudu Mungu. Hivi ni kusema kwamba, mwanadamu hajawahi kufikiria wala kuelewa kwamba imani katika Mungu inahitaji kumcha Mungu, na kumwabudu Mungu. Ni kwamba moyo wa mwanadamu ni mwovu, unaficha udanganyifu na ujanja, haupendi mambo ya kutopendelea na haki na kile kilicho chanya, nao ni wenye kustahili dharau na ulafi. Moyo wa mwanadamu umemfungia Mungu nje sana, hajampa Mungu moyo wake kabisa. Mungu hajawahi kuona moyo wa kweli wa mwanadamu, wala hajawahi kuabudiwa na mwanadamu.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 322 Mungu Apata Nini Kutoka kwa Mwanadamu?

Inayofuata: 324 Nia za Kustahili Dharau za Mwanadamu Kumwamini Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp