598 Watu Hawatendi Kabisa Maneno ya Mungu

1 Mungu amemaliza kuonyesha maneno Yake, lakini hawajaenda kwa kasi sawa kabisa, na wamebaki nyuma kabisa, wasiweze kukaa karibu na kila hatua, wasiweze kuzifuata nyayo za Mwana Kondoo kwa karibu. Kile ambacho walipaswa kukitii hawajakitii; kile ambacho walipaswa kukitenda hawajakitia katika vitendo; kile ambacho walipaswa kukiomba hawajakiomba; kile ambacho walipaswa kukiacha hawajakiacha. Bado hawajafanya kitu chochote kati ya hivi. Kwa hiyo, mazungumzo haya ya kwenda kwenye dhifa ni maneno matupu na hayana maana kabisa. Yamo katika fikira za watu tu. Inaweza kusemwa kwamba hadi sasa watu hawajatimiza majukumu yao kabisa. Kila kitu kinategemea Mungu kufanya na kusema vitu Yeye Mwenyewe, wakati kazi ya watu kwa kweli imekuwa ndogo sana. Wote ni taka isiyokuwa na maana ambao hawajui jinsi ya kupatana na Mungu.

2 Mungu amezungumza mamia ya maelfu ya maneno, lakini watu hawajayaweka katika vitendo kabisa—kuanzia kunyima mwili, kuacha dhana, kuwa watiifu kwa Mungu katika mambo yote, kukuza ufahamu na kupata umaizi wakati uo huo, hadi kwa kuachilia hadhi za watu katika mioyo yao, kuondoa sanamu ambazo zinamiliki mioyo yao, kuasi dhidi ya makusudi binafsi ambayo si sahihi, kutotenda kwa msingi wa mihemko yao, kufanya mambo kwa haki bila ubaguzi, kufikiri zaidi juu ya maslahi ya Mungu na ushawishi wao kwa wengine wanapozungumza, kufanya mambo zaidi yanayonufaisha kazi ya Mungu, kukumbuka kunufaisha nyumba ya Mungu katika yote wanayofanya, kutoruhusu mihemko yao kuamua tabia yao, kuacha yale ambayo yanapendeza miili yao wenyewe, kuondoa dhana za zamani za ubinafsi. Lakini watu hawajayaweka katika vitendo kabisa.

3 Kwa kweli watu wanafahamu baadhi ya mambo katika maneno haya yote juu ya kile ambacho Mungu anahitaji kutoka kwao, lakini hawako tayari kuyaweka katika vitendo. Ni kwa namna gani nyingine ambayo Mungu anaweza kufanya kazi na kuwashawishi? Waasi machoni pa Mungu wanawezaje bado kuwa na ujasiri wa kuchukua maneno ya Mungu na kuyastahi? Wanawezaje kuwa na ujasiri wa kula chakula cha Mungu? Dhamiri ya mwanadamu ipo wapi? Hawajatimiza wajibu mdogo kabisa waliopaswa kutimiza, kwa hiyo kuzungumza juu ya kufanya yote wawezayo ni hoja isiyokuwa na maana. Je, wao si watu wa njozi tu? Hakuwezi kuwa na mazungumzo ya uhalisi bila matendo. Huo ni ukweli wa wazi!

Umetoholewa kutoka katika “Sisitiza Uhalisi Zaidi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 597 Kuna Thamani Gani katika Kuthamini Hadhi?

Inayofuata: 599 Mungu Daima Anamsubiri Mwanadamu Kumrudia

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki