208 Yaliyopita Yananichoma Kama Upanga

1 Ninapofikiri juu ya imani yangu katika Bwana hapo zamani, najuta kwa sababu ya kile nilichofanya. Nachukia kukataa kwangu kazi ya Mungu katika siku za mwisho, nimeachwa na majuto ya milele. Niliota kila siku kuhusu kurudi kwa Bwana, nilitamani kwa moyo wangu wote kunyakuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni. Lakini Bwana alipokuja akigonga mlango na wokovu wa wakati wa mwisho ulipoonekana, nilikataa kuukubali. Huku nikifikiria kwamba kumwamini Mungu kulikuwa kuamini katika Biblia, nilimwekea Mungu mipaka ndani ya Biblia. Nilipapaya, nikiihukumu kiholela kazi ya Mungu bila nia ya kutafuta. Nilifanya kazi kulizuia kanisa ili kuwazuia waumini kutafuta na kuchunguza njia ya kweli. Ili kudumisha jina langu na hadhi yangu niliwawekea mipaka waumini ndani ya ufahamu wangu mwenyewe. Sikuwahi kufikiria ningeweza kumtumikia Mungu miaka hii yote lakini kuwa kiongozi wa kumpinga. Dhambi zangu zisizoweza kufutwa huniumiza bila kikomo.

2 Nilikuwa mwasi na mkinzani sana lakini Mungu bado alionyesha rehema na Akajaribu kufanya kila kitu ili kuniokoa. Alikuwa amebisha kwenye mlango wa moyo wangu na maneno Yake mara nyingi kabla moyo wangu mgumu kugeuka. Nimekubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, nimeona jinsi nilivyo mpumbavu na kipofu. Utajiri wa kile Mungu anacho na alicho, wanadamu hawawezi kuelewa kikamilifu. Kazi ya Mungu haizuiwi na sheria yoyote, inaendelea kila wakati. Lakini niliwekea kazi ya Mungu mipaka kwa maneno ya Biblia, jambo la kiburi sana. Waumini wengi walipoteza nafasi yao ya kupata wokovu kwa sababu ya kuzuia kwangu. Huku nikiamini katika Mungu, bado nilishindana na Yeye kwa ajili ya hadhi, kwa kweli nilikuwa Mfarisayo wa siku hizi. Napaswa kuhukumiwa kwa ajili ya matendo yangu, lakini bado Mungu alinipa nafasi ya kutubu. Ninapoona upendo wa kweli wa Mungu ninahisi nina deni Lake kubwa sana.

Kiitikio: Ee Mungu, nilikuamini lakini sikukujua, na nilikupinga na kukuhukumu. Kwa kweli mimi ni wa aina ya Shetani, sistahili rehema na wokovu Wako. Ee Mungu, nitatubu na kukubali hukumu Yako. Nitafuatilia ukweli kwa kila kitu nilicho nacho, kutimiza wajibu wangu na kulipa upendo Wako.

Iliyotangulia: 207 Sitawahi Tena Kujitenga na Mungu

Inayofuata: 209 Kujitafakari Hunipa Njia ya Kufuata

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

83 Upendo wa Kweli

1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki