473 Ni Ukweli Tu Unaoweza Kuupa Moyo wa Mwanadamu Amani

1 Tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho ambayo tumeweza kushiriki pamoja ni kweli. Haiwezi kupimwa kupitia kwa gharama ya juu ya vifaa vya kimwili wala thamani yake kupimwa kwa pesa, kwa sababu si kifaa cha anasa, na kinatoa mahitaji ya moyo wa kila mmoja. Katika mchakato wa uzoefu wako wa wokovu kupitia kwa Mungu, wakati ukifuatilia mabadiliko katika tabia yako, kama huelewi mapenzi Yake au hujui ukweli ni nini, kama huelewi tabia ya Mungu, huhisi wasiwasi sana? Huhisi njaa na kiu kuu katika moyo wako? Je, hizi hisia hazikuzuii dhidi ya kuhisi pumziko katika moyo wako? Hivyo basi unaweza kufidia vipi njaa hiyo katika moyo wako?

2 Unapohisi tamanio kubwa la kupata nuru kutoka kwa Mungu ili kukuruhusu kujua uhalisi wa ukweli na mapenzi Yake, ni nini unachohitaji kingi zaidi? Kile unachohitaji si mlo kamili, na wala si maneno machache mema. Zaidi ya hayo, si lile tulizo na kutosheka kwa muda kwa mwili—kile unachohitaji ni Mungu kuweza kukueleza moja kwa moja, kwa wazi kile unachofaa kufanya na namna unavyofaa kukifanya, kuweza kukuonyesha wazi ukweli ni nini. Baada ya kuelewa haya, hata kama ni sehemu ndogo tu, huhisi kuwa umetosheka zaidi katika moyo wako kuliko vile ambavyo ungekuwa umekula mlo mzuri? Wakati moyo wako umetosheka, huo moyo wako, nafsi yako nzima, havipati pumziko la kweli?

3 Maana yake ni kwamba kile kinachotoka kwa Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, na kila kitu Chake vyote ni vikuu zaidi kuliko kitu kingine chochote, kikiwemo kile kitu au yule mtu ambaye uliwahi kuamini kuwa unamthamini zaidi. Hivyo ni kusema, kama mtu hawezi kupata maneno kutoka katika kinywa cha Mungu au kama haelewi mapenzi Yake, hawezi kupata pumziko. Kila kitu ambacho Mungu anafanya ni ukweli na maisha. Ukweli kwa mwanadamu ni kitu ambacho hawawezi kukosa katika maisha yao, kitu ambacho hawawezi kuishi bila; unaweza pia kusema kwamba ndicho kitu kikuu zaidi. Ingawa huwezi kukiangalia au kukigusa, umuhimu wake kwako hauwezi kupuuzwa; ndicho kitu cha pekee kinachoweza kukuletea pumziko moyoni mwako.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 472 Ukweli Ni Methali ya Juu Zaidi ya Maisha

Inayofuata: 474 Unapaswa Kuyaacha Yote Kwa Ajili ya Ukweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp