667 Mwanadamu Haelewi Nia Njema za Mungu

1 Watu mara nyingi wanakuwa na wasiwasi kuhusu na wana uoga wa majaribio ya Mungu, ilhali siku zote wanaishi katika mtego wa Shetani na kuishi katika maeneo hatari ambapo wanashambuliwa na kunyanyaswa na Shetani—lakini hawaogopi na hawashangazwi. Nini kinaendelea? Imani ya binadamu katika Mungu ni finyu mno kwa mambo anayoweza kuona. Hana shukrani hata chembe kuhusu upendo na kujali kwa Mungu kwa binadamu, au wema Wake na utiliaji maanani kwa binadamu. Lakini kwa hofu na wasiwasi kidogo kuhusu majaribio, hukumu na kuadibu kwa Mungu na adhama na hasira Yake, binadamu hana hata chembe cha uelewa wa nia nzuri za Mungu.

2 Kwa kutajwa kwa majaribio, watu wanahisi ni kana kwamba Mungu anazo nia nyingine zisizo wazi na hata baadhi wanasadiki kwamba Mungu ana mipango ya maovu, wasijue hata kile ambacho Mungu atawafanyia; hivyo, wakati huohuo kutaka kuwa watiifu kabisa kwa ukuu na mipangilio ya Mungu, wanafanya kila wawezalo kuzuia na kupinga ukuu wa Mungu juu ya binadamu na mipangilio kwa binadamu, kwani wanasadiki kwamba kama hawatakuwa makini watapotoshwa na Mungu, na kama hawatakuwa na mshikilio thabiti wa hatima yao binafsi, basi kila kitu walicho nacho kinaweza kuchukuliwa na Mungu, na maisha yao huenda hata yakaisha.

3 Binadamu yumo kwenye kambi la Shetani, lakini hawi na wasiwasi kamwe kuhusu kunyanyaswa na Shetani, na ananyanyaswa na Shetani lakini haogopi kamwe kutekwa nyara na Shetani. Siku zote anasema kwamba anaukubali wokovu wa Mungu, ilhali hajawahi kumwamini Mungu au kusadiki kwamba Mungu atamwokoa kwa kweli kutoka kwenye makucha ya Shetani. Kama, sawa na Ayubu, binadamu anaweza kunyenyekea kwa mipango na mipangilio ya Mungu na anaweza kuitoa nafsi nzima kwa mikono ya Mungu, basi hatima ya binadamu haitakuwa sawa na ile ya Ayubu—kupokea baraka za Mungu? Kama binadamu anaweza kukubali na kunyenyekea Sheria ya Mungu, nini kipo cha kupoteza?

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 666 Kujaribiwa na Maneno ya Mungu ni Kubarikiwa

Inayofuata: 668 Usafishaji wa Mungu wa Mwanadamu Ni Wa Maana Zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp