533 Yeyote Asiyetenda Ukweli Ataondolewa

1 Wale wanaomwamini Mungu kwa kweli ni wale walio tayari kuweka neno la Mungu kwenye matendo, na ni wale walio radhi kutenda ukweli. Wale wanaoweza kwa kweli kuwa shahidi kwa Mungu pia ni wale walio radhi kuweka neno Lake kwenye matendo, na ni wale ambao kwa kweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wanaotumia hila na wale wanaotenda yasio haki wote ni watu wasiokuwa na ukweli na wote huleta aibu kwa Mungu. Wale walio kanisani wanaohusika na mabishano ni vibaraka wa Shetani, na ni mfano mwema wa Shetani. Mtu wa aina hii ni mwovu sana. Wale wasio na ufahamu na wasio na uwezo wa kusimama upande wa ukweli wanahifadhi nia mbovu na kufifisha ukweli. Watu hawa hata zaidi ni waakilishi kamili wa Shetani; wamepita hali ya ukombozi na ni wazi mno kuwa wao wote ni vitu vya kuondolewa.

2 Wale wasiotenda ukweli hawapaswi kuruhusiwa kusalia katika familia ya Mungu, wala wale wanaobomoa kanisa kwa makusudi. Hakuna kazi nyingine ya bure itakayofanywa kwa watu hawa; wale walio wa Shetani hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, ilhali wale wanaotafuta ukweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wasiotenda ukweli hawastahili kusikia njia ya kweli na hawastahili kuwa na ushuhuda kwa ukweli. Kimsingi ukweli si kwa ajili ya masikio yao lakini badala yake unazungumzwa kwa ajili ya masikio ya wale wanaoutenda. Wale wanaotenda ukweli mwishowe wataokolewa na kufanywa wakamilifu kwa kupitia ukweli. Wale wasiotenda ukweli mwishowe watakaribisha maangamizi kwa kupitia ukweli. Hii ndio miisho inayowasubiri wale wanaotenda ukweli na wale wasioutenda.

Umetoholewa kutoka katika “Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 532 Wasioyatenda Maneno ya Mungu Wataondolewa

Inayofuata: 534 Kutofuatilia Ukweli Huishia Katika Kulia na Kusaga Meno Daima

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp